Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya Dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa

Huyu ni waziri au kopo? siamini kama anaweza kuwa na akili ya kipuuzi kama hiyo, kwanini asiulize hizo Hospitals kwanini hawana dawa kuliko kuvamia biashara za watu? Watu wanataka huduma nzuri sio siasa na misifa ya kijinga, sasa wanachoenda kufanya ni kuharibu biashara za watu na ajira za watu
 
Pale akili ndogo zinapotawala akili kubwa...Aisee...sijaelewa lengo la huyu Mama eti waziri ni lipi hapa? Kwani wakipeleka hata mita 1,000 dawa zitapatikana Hospitali au itakuwa ndio mbaya zaidi kwa wagonjwa kutembea hayo makilomita kutafuta dawa? mwizi ni mwizi tu na dawa yake ni kumzuia asiibe na sio vinginevyo..
Amna anayeiba dawa ndugu hizo porojo tu za wanasiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni waziri au kopo? siamini kama anaweza kuwa na akili ya kipuuzi kama hiyo, kwanini asiulize hizo Hospitals kwanini hawana dawa kuliko kuvamia biashara za watu? Watu wanataka huduma nzuri sio siasa na misifa ya kijinga, sasa wanachoenda kufanya ni kuharibu biashara za watu na ajira za watu
Waziri wa elimu: “ maduka yote yanayouza vitabu na madaftari karibu na shule ya fungwe , maana wao wana-vitabu lakini shuleni havipo”
Waziri wa kilimo : maduka yote ya pembejeo yasitoe huduma karibu na mashamba ....

TUNA VIONGOZI WENYE UWEZO MDOGO sana wa kufikiria , sijui tumemkosea nini MUNGU... kuanzia Rais mpka baadhi ya mawaziri
 
Ukisikiliza yanayoendelea mahospitalini na madawa utashangaa sana

Hakuna watu wanaiba dawa kama hao
Kudhibiti ni vigumu sana hizo dawa kwani wanatuibia hata sisi tunaponunua utapewa vidonge pungufu kwa bei ile ile sasa hivyo vilivyobaki wanapeleka wapi
 
Hapo maana yake wagonjwa wameongezewa umbali wa kwenda kuchukua dawa..
Ikitokea dawa ya dharura inahitajika basi ndio uwezekano wa mgonjwa kwenda ahera mapema unavyokuwa Karibu..
Najua wengi watafurahi lakini kuna hatari kwa wagonjwa wa dharura
Au ni mita 500 ili watu wafanye mazoezi
 
Hapo anaemkomoa nimgonjwa mana wanachofanya nikuongeza mwendo wakwenda kununua hizo dara zaid yamita 500 ila mahospitalin dawa hazijawai kutosha
 
Screenshot_20220124-233008_1.jpg
 
Kwamba:-
1) uwepo wa maduka ya dawa karibia na Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati unasababisha Ukosefu wa dawa kwenye vituo hivi !!??
2) uwepo huo unasababisha wizi wa dawa !!?? Basi huo wizi utakuwa ni wa kiwango cha hatari !!!

Na kama vituo hivyo vya kutolea huduma za afya vinatimiziwa mahitaji maana yake ni Kwamba:-

1) Bajeti inayotolewa na GOV ni inayotosheleza mahitaji hivyo kupelekea MSD kuwa na shehena ya dawa, vitendanishi, vifaa na vifaa
tiba kama vyenye kutosheleza mahitaji;

2) Mgao wa fedha za manunuzi ni wa kutosha na unapelekwa kwa wakati katika vituo vya kutolea huduma za afya vyeny kupata mgao huo;

3) Dawa/Vitendanishi/Vifaa/Vifaa Tiba vinapelekwa kwa wakati kwenye vituo hivyo na mfumo wa ugavi/usambazaji uko imara (Timely
delivery);

4) Vyanzo vya mapato ya ndani ya vituo vya kutolea huduma za afya vinatumika ipasavyo kwa ajili ya uwepo wa mahitaji ya dawa N.k
kulingana na miongozo, kanuni na taratibu zilizopo;

5) Taarifa zinazotumika kufanyia maamuzi hii ikiwa ni pamoja na mifumo ya Tehama ya uendeshaji/ugavi ya vituo hivyo iiko safi kabisa kiasi
cha kupelekea Maoteo/Forecasting za mahitaji ya dawa N.k. ambazo ni halisia na zenye tija;

6) Kwa kuzingatia (5) ni kuwa Shehena za Dawa N.k zinaagizwa kulingana na mahitaji ya wakati husika na zenye kutosheleza (Timely
procurement);

7) Taratibu na mchakato wa manunuzi katika vituo vya kutolea huduma ni wa haraka na unaopelekea utoaji huduma rafiki na kwa wakati;

8) Timu za Usimamizi katika ngazi mbalimbali (Wizara, Mikoa/RHMT, Wilaya/CHMT, Vituo vya kutolea huduma/Internal Audits &
Assessment) zinafanya kazi za usimamizi na ukaguzi ipasavyo;

9) Mfumo ama utaratibu wa kutumia Mshitiri/Prime Vendor kwa vituo vya kutolea huduma vinavyoguswa na mpango huu uko safi na ni rafiki
kabisa maana huo ndio unatakiwa uzibe pengo la mahitaji hasusani yale yanayokosekana MSD;

10) Kama kila kitu kiko sawa na safi kabisa-kabisa ni wazi pia hakuna Uagizaji wa Mahitaji kwa njia ya dharura/Emergency Ordering.

Ni wazi kuna kitu hakijakaa sawa.
 
VIGEZO VYA KUZINGATIA KABLA KUFANYA MAOMBI YA KUFUNGUA FAMASI
(Made under Regulation 4&5 of the Pharmacy (Premises Registration) Regulations GN 269, 2020)
1.0 REJAREJA/COMMUNITY PHARMACY
(i) Hakikisha kuwa ukubwa wa jengo si chini ya mita za eneo 30 (30m2
).
(ii) Hakikisha kuwa umbali kutoka famasi ya karibu ya rejareja si chini ya mita 150 (150m)
(iii) Hakikisha kuwa eneo unalotaka kufungua lipo umbali wa mita 100 kutoka sehemu
zisizofaa kwa huduma za famasi, mfano: - bar, kituo cha mafuta, mifereji ya maji taka
iliyowazi, madampo, gereji na umbali wa mita 50 kutoka maabara.
(iv)Hakikisha kuwa umbali kutoka vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali unakuwa
kama ifuatavyo;-
 500m kutoka Hospitali ya Taifa au Hospitali ya Kanda
 400m kutoka Hospitali ya Mkoa
 300m kutoka Hospitali ya Wilaya
 200m kutoka Kituo cha afya au Zahanati
(v) Ukijiridhisha jaza fomu ya maombi ya ukaguzi wa awali kwa umakini approval of
location form – PCF.5a.
(vi)Lipia TZS 100,000 kwa njia ya Control number kwa ajili ya ukaguzi na upewe risiti ya
Baraza.
2.0 JUMLA/WHOLESALE PHARMACY
(i) Hakikisha kuwa ukubwa wa jengo si chini ya mita za mraba 60 (60m2
).
(ii) Fuata hatua (iii) – (vii) kama ilivyo hapo juu.
3.0ZINGATIA YAFUATAYO;-
(i) Hutakiwi kufanya matengenezo yeyote kabla haujafanyiwa ukaguzi wa awali.
(ii) Baraza lina mamlaka ya mwisho kuamua eneo linalofaa kwa biashara ya famasi,
na ni jukumu la mwombaji kuhakikisha kuwa anazingatia vigezo vilivyoweka na
Baraza.
(iii)Hakikisha namba za simu unazojaza zinapatikana muda wote.


 
Kuyaondoa hayo maduka siyo haki kwani unakuta mgonjwa wako anahitaji dawa kwa haraka hospitali hakuna unakwenda hapo nje hakuna umbali mrefu unapata dawa wakati mwingine ni usiku mwingi kama duka lingekuwa mbali na ni usiku kuifuata dawa huko mbali
si unaweza kabwa na vibaka suluhisho la hilo tatizo ni kuweka wasimamizi wazuri wapeni mishahara mizuri wafanye kazi kwa ufanisi na msiruhu wahudumu wa hospitali hata kama awe daktari asiwe pharmacy hii ndo inachangia sana upotevu wa dawa
 
Huyu Dada ummy nampenda sana,sura na lugha (kiswahili) chake Bora kabisa, leo naona nitofautiane naye,dawa zikiwa kilomita nzima kutoka hospitali huo utakuwa msaada kwa mgonjwa? hapa tafuteni namna nyingine ya kumaliza tatizo lililopo,siyo kusogeza dawa mbali na hospitali.
 
Mi nafikiri wange focus kwenye kwanini dawa hakuna hospitali. Then wakisha jua tatizo liliko walitatue kama ni wizi basi wahusika wawajibishwe. Kama kweli ni uhaba wa madawa serikali iweke bajeti dawa zipatikane.

Sioni mantiki ya kuyaondoa maduka. Kuna wakati dawa zinakua hamna kutokana na uzembe wao wenyewe basi uo mda hayo maduka hugeuka mkombozi iweje yatolewe?
MSD yenyewe haina dawa za kupeleka mahospitalini, je ukikataza maduka yasiwepo jirani unawatakia mema wagonjwa wetu? Huyu Ummy ni Waziri wankutaka KIKI kama wasanii
Nawashangaa watu wanaomlaumu Ummy Mwalimu, hiyo ni Sheria ilitungwa Na Bunge yy anaitekeleza tu kwahiyo hapo walaumiwe wabunge Wa Ccm
Hiyo solution ya Ummy Mwalimu haiwezi kuongeza upatikanaji wa dawa mahospitalini. Kwanza angetupa ushahidi wa dawa na vifaa tiba vya Serikali alivyovikuta kwenye hizo pharmacy zikizopo 500 metres
 
Nawashangaa watu wanaomlaumu Ummy Mwalimu, hiyo ni Sheria ilitungwa Na Bunge yy anaitekeleza tu kwahiyo hapo walaumiwe wabunge Wa Ccm
Watu wanataka aeleze mantiki na tija ya hiyo sheria. Inaendaje kuondoa tatizo. watu kama wewe ambao huwa hamjiulizi WHY ndio mnashangaa
 
Hamna haja ya kuondoa yanasaidia sana mfano hospitali gloves hamna za kumzalishia mama MTU anenda nje chap chap ananunua kwenda nusu kilomita ni mbali mno

Sehemu zingine mawilayani miji midogo ukihesabu mita 500 toka hospitali ya serikali ilipo ni porini machakani kusikoishi watu kwenye majoka
 
Back
Top Bottom