Waziri Ummy Mwalimu, changamoto zinazohitaji kutatuliwa bado ni nyingi TAMISEMI

CAG Mtiifu

Member
Apr 16, 2021
6
2
Wanasema wajuzi, "Charity begins at home"

Mh. Ummy Mwalimu umebebeshwa majukumu mazito kuliko uliyokua nayo awali. Hongera sana

Changamoto ni nyingi hata mtangulizi wako anajua.

Umeanza vyema kwa kupaza sauti dhidi ya wabadhirifu walio ibuliwa na CAG.

Nimeona eti kuna mke wa kigogo mmoja hivi amelamba zaidi ya m.300. Hata sasa ninasubiri kuona unafanyaje maana chombo ya kiranja wako eti imezingua.

KUBWA ZAIDI, hakuna dawa kwenye hospitali ndani ya Halmashauri nyingi hususan Tanga Jiji. Kituo cha afya Ngamiani wanashinda wanacheka tu pale hawatoi huduma zinazotakiwa zaidi ya watumishi(hasa wanawake baadhi)kufanya masihara kwenye kazi. Nenda kaangalie wazee wanavyohudumiwa.Tazama watu wa hicho wanachokiita Mfumo,ni hatari balaa.

Nenda Korogwe na Mkinga huko. Achilia mbali Tanzania nzima nimekupatu habari za nyumbani kwako. Nyumba yako mama inavuja viongozi na wakuu wa idara (baadhi) ni wanyanyasaji. Wengine wanachukua wake za watu.

Wengine wanakula tu fedha za umma hebu fanya ufuatiliaji.

Kwa sasa hebu Mh. Rais avunje hii timu iliyopo watenganishwe hawa ma RC, RPC, RAS, DC, DAS na ma DED. Tena siotu wabadilishwe lakini pia Mh. Rais wachanganye wapoteane,wazingue wazunguke na wasizinguke ili wapumzike na waingie wengine ambao wanafanya kazi bila kuogopa kuzinguliwa
 
Hawa wanalindana, unadhani Ummy atamfanya nini mke wa Ndugai? Umechemsha hapo, sema mengine

Halafu Ndugai anawaita vijana wezi! Ummy hapo kwa mkewe Ndugai ana mtihani mkubwa; Rais amemtegea kuona kama anaweza kuutafuna huo mfupa uliomshinda Jaffo, rais yeye kasema hama muhari na mtu!
 
Suluhisho ni CCM kuondoka madarakani, kama imegoma kuondoka kwa sanduku la kura tutaitoa kwa njia mbadala.
The only problem is, y'all a bunch of cowards.

So, we'll stick with CCM chama cha wazee wetu na tutarekebishana tu.
 
Wengine wanachukua wake za watu.Wengine
Hili pia ni jukumu la waziri⁉️⁉️‼️‼️⁉️⁉️‼️‼️⁉️⁉️‼️‼️🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔

Hebu mhudumie mkeo, acha visingizio
 
Halafu Ndugai anawaita vijana wezi!!! Ummy hapo kwa mkewe Ndugai ana mtihani mkubwa; Rais amemtegea kuona kama anaweza kuutafuna huo mfupa uliomshinda Jaffo, rais yeye kasema hama muhari na mtu!
Ummy yaishe kwa kishindo cha mtu kuchapa lapa yakisha kimya kimya hutaeleweka kazi kwako H/works.
 
Suluhisho ni CCM kuondoka madarakani, kama imegoma kuondoka kwa sanduku la kura tutaitoa kwa njia mbadala.
Njia badala hakuna & jibu ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi & watanzania wakitaka kujivunia utanzania wao na watoto wetu kupata elimu bora jambo muhimu ni kuondoa hiki chama cha majambawazi ccm
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom