Waziri Ummy Mwalimu azitaka Hospitali za Rufaa kuboresha huduma ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa Muhimbili

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,764
4,330
Waziri Ummy Mwalimu amezitaka Hospitali za Rufaa kuboresha huduma ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Amesema hospitali za kanda, rufani, mikoa na wilaya huwa wanawahamisha wagonjwa wenye matatizo wanayoweza kuyatibu kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Agizo hilo alilitoa baada ya kutembelea MNH jana na kubaini kuwapo kwa mrundikano wa wagonjwa wanaotoka hospitali hizo kwa matatizo ya kawaida.

Akiwa katika kitengo cha dharura, alipokea malalamiko kutoka kwa watoa huduma ya kuwapo kwa mrundikano wa wagonjwa ambao miongoni mwao matatizo yanaweza kutibiwa walipotoka.

“Jambo ambalo limemleta ni la kuelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa hapa MNH. Hospitali za wilaya, mkoa, rufani na kanda, nyingi hazitimizi wajibu wake ni lazima zitoe huduma bora ili kuipunguza mzigo Muhimbili, inashangaza kuona hata mgonjwa ambaye hana damu anahamishiwa hapa huu ni uzembe,” alisisitiza Ummy.

Alisema katika kukabiliana na mrundikano wa wagonjwa MNH hasa kitengo cha dharura, wanaandaa mpango mkakati wa kuboresha hospitali hiyo, iliyojengwa zaidi ya miaka 60 iliyopita ili iweze kudumu kwa miaka 50 ijayo.

“Tutaiboresha ili sasa iendane na wakati ulioko, haipendezi kuona wagonjwa wanalala kwenye kona na majengo yamechakaa,” alisema Ummy.

Kadhalika alisema ipo haja ya kuwapo kwa Hospitali ya Kanda ya Dar es Salaam na Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kupunguza mzigo wa wagonjwa kwa hospitali hiyo ya taifa.

Ummy pia alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Prof. Lowrance Museru, kushughulikia changamoto alizopokea kutoka kwa wagonjwa kama kukaa wodini zaidi ya mwezi kusubiri matibabu.

Alitaja changamoto nyingine ni daktari kupita kwa awamu moja badala ya mbili, lugha mbaya kwa wagonjwa na kukosa huduma stahiki ilhali serikali imewekeza fedha za kutosha kuboresha mazingira na kuweka vifaa tiba vya kisasa.

Akijibu hoja za Ummy, Prof. Museru alisema katika kushughulikia lugha chafu kutoka kwa watumishi, tayari wametoa semina ya huduma kwa wateja kwa watoa huduma wa MNH na Mwananyama na wanaendelea kufanya hivyo.

Prof. Museru alisema wagonjwa wanaokaa muda mrefu bila matibabu, wanakuwa wanaandaliwa kusubiri kufanyiwa upasuaji, na kuahidi kama kuna changamoto nyingine asizozifahamu atazifanyia kazi.

Kuhusu madaktari kupita mara moja, alisema daktari bingwa mmoja anapita mmoja ili kutoa maelekezo ya aina ya matibabu ya kupatiwa na awamu nyingine wanapita madaktari wa kawaida wakiwamo wanafunzi.

Alisema wanakabiliwa na changamoto ya wananchi kukimbilia kueleza kero zao kwenye mitandao ya kijamii, badala ya kutumia njia za kuwaona wahusika.

“Hili ni tatizo waziri, tuna hii shida mgonjwa hawezi kuja kulalamika anaenda kwenye mitandao kuandika na hata tunapotatua changamoto hawezi kurudi kusema alikosea anabaki kimya,” alisema Prof. Museru.

 
Huduma za afya ngazi ya hospitali za Wilaya, Zahanati, nk ni tia maji tia maji.... hata pamba na mipira ya kuvaa mikononi hakuna!

Wekeni siasa tuone sasa, labda kama na takwimu za vifo mtaficha kama ambvyo mnapika takwimu za chanjo ya Uviko!
 
Sijaelewa vyema ila naomba nijitahidi kidogo...

Mimi nina fahamu madaktari kadhaa pale mnh wapo wanafanya pia hosp zingine kubwa na za kati za binafsi na majina yao yapo ktk mabango ya hosp hizo...

Hosp nne kubwa tu hapo mjini zilizopo karibu na mnh zina wafanyakazi waajiriwa wa mnh... Na bado kuna hosp za pembezoni na ndio maana mloganzila ni kama hawapataki maana pana wafanya kuwa kosesha ulaji...

Mkulu aliyepita na walio pita walishindwa dhibiti hii hosp hasa hawa watumishi
 
Kusema sawa, lakini ameweka utaratibu gani kuhakikisha kweli wanaokwenda Muhimbili wanatakiwa kwenda muhimbili...na huko watokako kweli wameshindikana...
 
Huko Tamisemi hakuna kitu majority wa hizo hospitali wanaita za rufani hazina vigezo hata vya kufanya upasuaji Theater zimechoka hizo EMD ni vituko watu wanapambana kwenye mazingira magumu.
 
... ule mtambo wa kimataifa wa rufaa za nyungu uliogunduliwa na wataalamu wazalendo bado upo pale MNH? Waziri alitakiwa autolee neno badala ya kujifanya hajui chochote; mbona la maduka ya madawa pembezoni mwa hospitali kalikumbuka anasahauje mtambo wa aina yake kama ule?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom