Waziri Ummy: Michango ya kujiunga kidato cha tano kwa shule za Serikali isizidi Tsh. 188,000

Vipi mlinzi, mpishi, sabuni ya chooni, rimu, jembe, fyekeo, ndoo ya lita 10, ndoo ya lita 20, kitambulisho, taaluma......nk.nk.nk.......
Fagio ,kukodishwa godoro,jengo,masomo ya jioni nk.Kuna michango kibao yaan,dogo anaingia six michango ni laki 4 kasoro,kuna michango yakulipia benki na kuna yakukabidhi kwa mkononi.
Hiyo five tulitumia milioni+.
 
Yaani ile bure ya O-level inafidiwa A-level. Inaonekana serikali haina mpango wa kuhakikisha hao inaowapa elimu bure wafike A level.Just imagine mzazi ni maskini mtoto aliingia secondary sababu ilikuwa ni bila ada,halafu anapopasi kuenda five inageuka kuwa mateso kwa mzazi

sasa sh188,000 huyu maskini ataitoa wapi?
Mwaka jana tulilipa hiyo 188,000
Lakini kuna mamichango hapo siyo ya kitoto,afu ni Mwaka wa kwanza.
 
Fyekeo , ndoo . Rim aende navyo.
Taaluma una maanisha nini?
Taaluma mbona ni mchango ulioasisiwa kitambo sana tangu enzi za nyerere, wanauita 'academic' kuna sehemu mwanaJF kasema wamelipa elf 20......wee acha tu.
 
Watanzania tuache masihara kweli karne hii ada ni 70,000 kisha mnakataa kutoa michango ili watoto wako wawe comfortable?
Naelewa kwa wazazi wasio na ajira kweli wanastahili kulipa hivyo, hata sisi wengine ambao watoto wetu wengine wamesoma private, this dependency is too much jamani...Hivi watanzania lini tutakuja elewa maana ya kufanya kazi na kujitegemea?
Hapa umeandika kitu gani wewe? Unafikiri wananchi wengi kuwa maskini ndio inamaanisha kwamba wanazaa watoto wasio na akili?

Ni jukumu la serikali kuwezesha watoto wengi kusoma ilimradi wana vigezo, kwa mantiki hiyo mahitaji mengine serikali ndio inawajibika kugharamia kama chakula, ulinzi wa shule, upishi, madaftari, karatasi, vitanda nk. Mzazi pia atawajibika kuchangia kwa baadhi ya mahitaji sio kugharamia kila kitu mpaka vitabu vya tahasusi hapo kuna namna wakuu wa shule na bodi husika wanajaribu kupunguza gharama kwa kuwabwagia wazazi wakati inawezekana serikali kuu haijui ujanja wanaofanya kujinufaisha ili kwamba pesa wanazotumiwa na serikali watumie kidogo kwa kuwa wametengeneza nafuu.
 
Miaka nenda rudi hayo majembe, mafyekeo sijui ndoo na masufuria hayajawahi kutosha? elimu ya A-level unahimizaje wanafunzi wakalime mashamba ya shule na kufyeka majani? halafu utarajie hao vijana wa cocentrate kwenye masomo wafaulu vizuri....
Una elimu gani ndugu na ulisomea wapi?
 
Wa jirani yangu amepewa bili kubwa ya ajabu mpaka amekata tamaa kumpeleka mwanae MPANDA GIRL
FACTS AND TRUTH MUST TOLD.
 
Ni shida aisee.....na wanashupaza misuli ya shingo wanakwambia elimu bure.....hovyo sana hawa watu.
Elim bure ni kuanzia darasa LA kwanza mpaka form 4 , Advanced hakuna elim bure mkuu ada ipo pale pale na michango mingine, sema michango imekua mingi tu ,
 
Amesema mkuu yeyote wa shule atakayebainika kukiuka agizo hilo, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Ummy alitangaza katazo hilo jana alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Bihawana mkoani Dodoma kukagua utayari wa shule za serikali kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2021.

Alisema kiasi hicho kinajumuisha ada ya Sh. 70,000.
Tupe namba ya wazi ya kutolea taarifa kwa watakaokiuka agizo lako
 
Mh mbona kama utapeli sasa huo.. Unaweza kuichanganua hiyo 430k?
Suruali 3@55,000/=
Rim 12000/=
Blanket
Masweta 2@ 18000/=
Mashati 2
Track suit za michezo
Viatu vya shule
Raba za michezo
Godoro 35000/=
NIMECHOKA KUANDIKA
 
Back
Top Bottom