Waziri Ummy: Michango ya kujiunga kidato cha tano kwa shule za Serikali isizidi Tsh. 188,000

Hata hivyo Waziri katoa ufafanuzi haizidi 188,000...Ila mimi nitatoa zaidi maana naona kama napewa favour mwanangu kusoma shule ya sekondari tena special kwa ada ndogo kama hiyo, I feel so bad kwakweli...
Watu wanatofautiana uwezo, wewe unayoona ndogo wengine ni mlima, ndo maana serikali inahangaika kubeba gharama zote za elimu ili isitokee hata kwa bahati mbaya vijana wenye uwezo wa kusoma washindwe kwa wazazi/walezi kukosa ada......nchi nyingine serikali kwa kuzingatia umuhimu wa elimu kwa watu wake inatoa elimu hadi chuo kikuu......
 
Kuna shule moja anakwenda mwanangu, maelekezo yanamtaka kila mwanafunzi wa kidato cha 5 na 6 aende na SABUNI YA CHOONI Lita 5...!!

Sasa hebu fikiri hili, kwamba kama shule ina mwanafunzi 300 maana yake shule inakusanya gallons za lita tano tano 300 sawa...

Maana yake hizi shule za umma hazipati fedha toka serikalini ili kujiendesha ikiwemo kununua sabuni za chooni kwa ajili ya vyoo vya mwanafunzi...???????
Na ukifuatilia hizo galoni zitaishia kwenye maduka ya watu binafsi, jamaa wanajaribu kutetea lakini serikali kuweka hiyo ada ndogo inajaribu ku subsidize elimu, na inalenga hasa kuifanya elimu iwe bure ukizingtia umuhimu wake.......sasa wajanja wanataka wajiongeze na vimichango vyao.
 
Kama kichwa kinavyoeleza, kwa sasa shule nyingi hasa zile za Serikali kwa wanafunzi wanaoenda kuanza kidato cha tano zinaenda kufunguliwa. Lakini nilichogundua mbali na ada kuainishwa kwenye fomu za kujiunga, michango ni mingi sana inayofika karibia mara tano ya ada.

Waziri ingilia kati kuwanusuru wazazi na huu utitiri wa michango ikiwa tayari ada ambazo wazazi wanaweza kujitahidi kuzilipa zimeshawekwa. Huu ni sawa na upigaji kwa wakuu wa shule.
Yaani ile bure ya O-level inafidiwa A-level. Inaonekana serikali haina mpango wa kuhakikisha hao inaowapa elimu bure wafike A level.Just imagine mzazi ni maskini mtoto aliingia secondary sababu ilikuwa ni bila ada,halafu anapopasi kuenda five inageuka kuwa mateso kwa mzazi

sasa sh188,000 huyu maskini ataitoa wapi?
 
Yaani ile bure ya O-level inafidiwa A-level. Inaonekana serikali haina mpango wa kuhakikisha hao inaowapa elimu bure wafike A level.Just imagine mzazi ni maskini mtoto aliingia secondary sababu ilikuwa ni bila ada,halafu anapopasi kuenda five inageuka kuwa mateso kwa mzazi

sasa sh188,000 huyu maskini ataitoa wapi?
Ni shida sana, angalau hiyo 188 waziri kaitamka.......lakini kuna shule wana michango hadi laki nne, hapo bado ada elfu 70....
 
Ukiwa unajali Elimu ya unaemsomesha hutohoji kuhusu michango..its Either husomesh au unasomesha kwa kulazimishwa...unaijua Sera ya maendeleo ya Elimu ya Msingi na secondary hasa katika kipengele cha Uwezeahaji shuleni pamoja na miundombinu?!achana na maneno ya wanasiasa wanaokuambia elimu ni bure...kama Elimu ni ghali Jaribu ujinga.
Kuna elimu gani wanapata siku hizi?
 
Hahaha....jamaaa kumbe wewe zwazwa namna hiyo, haya matusi unaendelea kudhirisha uzwazwa wako.......sijawahi kutana na jita lijinga namna hii....kutiki mkaruka.
Kumbe majita ni majinga, sikujua aisee.

Mijamaa iinaonekana inakupelekra moto wa hatari. Unapulizwaaaaa🤣
 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, amepiga marufuku wakuu wa shule zote za serikali kutoza michango ya kujiunga na kidato cha tano zaidi ya Sh. 188,000.

ummy.jpg

Amesema mkuu yeyote wa shule atakayebainika kukiuka agizo hilo, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Ummy alitangaza katazo hilo jana alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Bihawana mkoani Dodoma kukagua utayari wa shule za serikali kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2021.

Alisema kiasi hicho kinajumuisha ada ya Sh. 70,000.

Waziri Ummy alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa mwaka huu ni 87,663 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule 476 na kutoa wito kwa wazazi ambao wataamua kuwapeleka watoto wao kwenye shule za binafsi kutoa taarifa kupitia mfumo, ili kutoa fursa kwa wengine.

Aidha, aliwataka wakuu wa shule kuandaa mazingira mazuri ya kuwapokea wanafunzi na kuwapo na mahitaji yote muhimu.
Aliwataka wanafunzi wa bweni kuripoti Julai 3 na wa kutwa Julai 5.

Kadhalika, alisema katika ajira mpya za walimu hivi karibuni hakuna shule itakayokosa mwalimu wa Fizikia wala Hisabati.

Alifafanua kuwa walimu wa Fizikia walioajiriwa ni 1,360 wakati shule ambazo hazikuwa na mwalimu ni 1,100 na walimu wa Hisabati walioajiriwa ni 459 wenye shahada na stashahada 140 wakati uhaba ulikuwa kwa shule 400.

Chanzo: NIPASHE
MICHANGO au ADA? TULIAMBIWA ELIMU bure kuna MICHANGO
 
Back
Top Bottom