Waziri Ummy: Michango ya kujiunga kidato cha tano kwa shule za Serikali isizidi Tsh. 188,000

Mh mbona kama utapeli sasa huo.. Unaweza kuichanganua hiyo 430k?
1. Rake
2. Kwanja
3. Jembe na Mpini
4. Soft broom
5. Ufagio wa Nje
6. Ndoo 20L
7. Ndoo 10L
8. ID 6,000=
9. Ream paper 1
10. Taaluma 20,000=
11. Ukarabati 15,000=
12. Mpishi, Mlinzi, Vibarua 30,000=
13. Mock 20,000=
14. Nembo 2,000=
15. Matibabu 10,000=
16. Tahadhari 5,000=

Vichache nikumbukavyo
 
Miaka nenda rudi hayo majembe, mafyekeo sijui ndoo na masufuria hayajawahi kutosha? elimu ya A-level unahimizaje wanafunzi wakalime mashamba ya shule na kufyeka majani? halafu utarajie hao vijana wa cocentrate kwenye masomo wafaulu vizuri....
Ndio maana nimesema elimu sio kipaumbele mnafanyiwa geresha tu
 
Kama kichwa kinavyoeleza, kwa sasa shule nyingi hasa zile za Serikali kwa wanafunzi wanaoenda kuanza kidato cha tano zinaenda kufunguliwa. Lakini nilichogundua mbali na ada kuainishwa kwenye fomu za kujiunga, michango ni mingi sana inayofika karibia mara tano ya ada.

Waziri ingilia kati kuwanusuru wazazi na huu utitiri wa michango ikiwa tayari ada ambazo wazazi wanaweza kujitahidi kuzilipa zimeshawekwa. Huu ni sawa na upigaji kwa wakuu wa shule.
Mkuu,

Umesema ukweli mtupu,

Kidato cha tano ada ni shilingi 70,000/= kwa mwaka lakini mahitaji yanayotakiwa kuambatana na mwanafunzi yanafikia 1,400,000/= hii sio sahihi kabisa na ni mateso yasiyokuwa ya msingi. Kuna tofauti gani na shule binafsi ambazo ukilipa kiasi hicho mahitaji yote unahudumiwa?

Vitabu vyote vya tahasusi unanunua mzazi, unifomu, godoro, jembe, kwanja, vifaa vya kusaficha vyoo, bafu, darasa na bweni, vyombo vya chakula, nguo za michezo, madaftari, karatasi za mazoezi na mitihani, pesa ya ulinzi, pesa ya kulipia upishi nk ni kero tupu na hakuna nafuu yoyote ile.

Halafu walimu na elimu inayotolewa kwenye shule za serikali hasa za kata ni changamoto maana kila kitu unalipia
 
Ni ujanja ujanja wanaofanya waonekane wanatoza ada kidogo, ni bora tu watoze kama ada za private ili tujue moja.....
 
Watanzania tuache masihara kweli karne hii ada ni 70,000 kisha mnakataa kutoa michango ili watoto wako wawe comfortable?
Naelewa kwa wazazi wasio na ajira kweli wanastahili kulipa hivyo, hata sisi wengine ambao watoto wetu wengine wamesoma private, this dependency is too much jamani...Hivi watanzania lini tutakuja elewa maana ya kufanya kazi na kujitegemea?
 
Ni ujanja ujanja wanaofanya waonekane wanatoza ada kidogo, ni bora tu watoze kama ada za private ili tujue moja.....
Ona aibu basi, dunia ya leo ada ya 70,000 unaitoa wapi? Ebu piga hesabu hizo pesa mtoto ale alale aoge kwa mwaka, kweli? Something must be wrong in our attitudes!
 
Miaka nenda rudi hayo majembe, mafyekeo sijui ndoo na masufuria hayajawahi kutosha? elimu ya A-level unahimizaje wanafunzi wakalime mashamba ya shule na kufyeka majani? halafu utarajie hao vijana wa cocentrate kwenye masomo wafaulu vizuri....
Unataka wakasome tu bila kufanya hata usafi wa smart area...hao watakuwa watoto au vilema? Ndiyo maana wanakuja kuwa raia waajabu ajabu...Acha wakalime smart area, wafagie, wamwagilie maua na wasome, hiyo ndiyo kumfanya mtoto awe kamili siyo kusoma tu na kukaririshwa kama parrots
 
Ona aibu basi, dunia ya leo ada ya 70,000 unaitoa wapi? Ebu piga hesabu hizo pesa mtoto ale alale aoge kwa mwaka, kweli? Something must be wrong in our attitudes!
Kwa hiyo elfu sabini nimeipanga mimi, au serikali......vipi kule ambapo hawalipi kabisa ada, unajifanya hujui sera ya serikali ya elimu bure hadi kidato cha nne? au unajifanya zwazwa....
 
Kwani hao ni kidato cha nne? Au umesahau kuwa unaongelea kidato cha tano?
 
Kwa hiyo ada ya elfu 70 wamepangiwa nani hasa?
Tumia akili ada elfu sabini mwaka mzima unaona mchango kutoa ni hasara? Wameweka ada ndogo ili wenye uwezo wa saidie hao wachache ambao hawana uwezo kwa michango....Kuwa muungwana, hapa unatumia kiasi gani cha pesa kusogoa mitandaoni kisha unaona vibaya kulipia mwanao michango kuwasaidia ambao hawajawahi ona hata key board...Utakufa masikini kwakuwa bahili
 
Tumia akili ada elfu sabini mwaka mzima unaona mchango kutoa ni hasara? Wameweka ada ndogo ili wenye uwezo wa saidie hao wachache ambao hawana uwezo kwa michango....Kuwa muungwana, hapa unatumia kiasi gani cha pesa kusogoa mitandaoni kisha unaona vibaya kulipia mwanao ada...Utakufa masikini kwakuwa bahili
Kwa hiyo mnahujumu nchi, mnachukua michango ya wanafunzi mnatia mifukoni halafu mnaipa mzigo serikali kuhudumia elimu kwa ada ndogo. Kwa nini hiyo michango isiwekwe kwenye ada...
 
Usi panic basi, mimi ni raia kama wewe na mzazi na ninalipa ada na michango, ninaishukuru serikali sana kwakua naona hii ada ni ndogo sana na nipo tayari kwa hiari yangu kutoa michango hata mara kumi ili wale ambao hawana uwezo nao watoto wao wapate masufuria ya kupika etc
 
Mbona mnaorodhesha michango lukuki kwenye fomu mnatuma kwa kila mwanafunzi, aliyekwambia wote wana uwezo wa kulipa ni nani? BTW wewe ni mwalimu mkuu wa shule gani.....
 
Umeambiwa ni michango, kwahiyo michango unahiari ya kutoa pale unapoweza siyo lazima yote
 
Hata hivyo Waziri katoa ufafanuzi haizidi 188,000...Ila mimi nitatoa zaidi maana naona kama napewa favour mwanangu kusoma shule ya sekondari tena special kwa ada ndogo kama hiyo, I feel so bad kwakweli...
 
Kama kichwa kinavyoeleza, kwa sasa shule nyingi hasa zile za Serikali kwa wanafunzi wanaoenda kuanza kidato cha tano zinaenda kufunguliwa. Lakini nilichogundua mbali na ada kuainishwa kwenye fomu za kujiunga, michango ni mingi sana inayofika karibia mara tano ya ada.

Waziri ingilia kati kuwanusuru wazazi na huu utitiri wa michango ikiwa tayari ada ambazo wazazi wanaweza kujitahidi kuzilipa zimeshawekwa. Huu ni sawa na upigaji kwa wakuu wa shule.
Kuna shule moja anakwenda mwanangu, maelekezo yanamtaka kila mwanafunzi wa kidato cha 5 na 6 aende na SABUNI YA CHOONI Lita 5...!!

Sasa hebu fikiri hili, kwamba kama shule ina mwanafunzi 300 maana yake shule inakusanya gallons za lita tano tano 300 sawa...

Sasa mtu anaweza kujiuliza swali hili, kwamba, ina maana hizi shule za umma hazipati fedha toka serikalini ili kujiendesha ikiwemo kununua sabuni za chooni kwa ajili ya vyoo vya mwanafunzi...???????

Kazi ya serikali inayoongeza kodi kila mwaka na kuzikusanya kwa maumivu makubwa kwa wananchi itakuwa ni nini sasa kama kutoa huduma hii muhimu ya elimu kwa wananchi wake inakuwa ngumu hivi..?
 
Back
Top Bottom