Waziri Ummy: Masoko na Stendi zote zinazomilikiwa na TAMISEMI kujengewa Visima vya Maji ili kukabiliana na moto

Hakuhitajiki kauli za kukurupuka. Badala uake kunatakiwa kuwa na mpango maalum wa kuangalia namna ya kushughulikia majanga. Janga siyo moto pekee yake.

Wanatakiwa watu wenye uwezo wa kuyaona majanga kabla hayajatokea. Hao ndio wanaweza kutengeneza action plan ya kushugjulikia majanga ya aina mbalimbali.
 
Matokeo ya kuwa na viongozi vilaza.

Hilo soko la kariakoo tu liko KM zisizo tatu kutoka makao makuu ya Polisi kitengo cha fire nchini. lakini wameshindwa kuzima moto usiku kucha.
Hapo zilizo ofisi za fire ni kama km moja kutoka jangwani ambako unapita mto ambao ni chanzo cha maji. solo lenyewe la kariakoo liko umbali usio zidi km tatu kutoka kiwanda kikubwa kabisa cha pombe nchi cha TBL, ambao wana water resevoir kubwa sana kwa ajiri ya uzalishaji wa byere. kutokea ofisi hizo za fire pamoja na soko la kariakoo ni kama km nne kufika kwenye ufuko wa maji bahari hindi.

Bado, wameshindwa kuzima moto usiku kucha.

Sad.
 
Waziri wa Tamisemi mh Ummy Mwalimu amesema Serikali itajenga visima vya maji kwenye masoko na stendi za mabasi zote zinazomilikiwa na Halmashauri ili kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza.

Chanzo: Radio One
Visima hapana, wasije kuzimia moto na maji ya kutoka vyoo vya sokoni.

Wanashindwa kuweka pipes hata za nchi 4 kutoka Mamlaka za maji????

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Hakuhitajiki kauli za kukurupuka. Badala uake kunatakiwa kuwa na mpango maalum wa kuangalia namna ya kushughulikia majanga. Janga siyo moto pekee yake.

Wanatakiwa watu wenye uwezo wa kuyaona majanga kabla hayajatokea. Hao ndio 5t wanaweza kutengeneza action plan ya kushugjulikia majanga ya aina mbalimbali.
Sasa yeye hapo umi anaona katimiza wajibu wake katika kukabiliana na hilo janga, utasikia mpaka mawaziri ya mambo ya nje, elimu na michezo watatoa matamko yao
 
Waziri wa Tamisemi mh Ummy Mwalimu amesema Serikali itajenga visima vya maji kwenye masoko na stendi za mabasi zote zinazomilikiwa na Halmashauri ili kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza.

Chanzo: Radio One
Bora hivyo visima vichimbwe kwenye vituo vya zima moto ili upatikanaji wa maji kwa magari yao uwe rahisi, na si kila moto unataka uzimwe na maji.
 
Back
Top Bottom