Waziri Ummy: Marufuku Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuingiza Siasa kwenye taaluma ya Uuguzi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,799
141,696
Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu amesema ni marufuku kwa wanasiasa kuingilia taaluma ya Uuguzi.

Waziri Ummy amesema tabia ya Wakuu wa Mikoa au Wilaya kuwakamata Wauguzi na Madaktari na kuwaweka ndani haikubaliki kabisa na atakayethubutu kuwachezea watumishi wa afya yeye kama Boss wao atawashughulikia ipasavyo.

Waziri Ummy amesema hayo mkoani Manyara.

Chanzo: ITV habari
 
Huyo waziri Ummy anapiga siasa za kichovu na kuchekesha walionuna. Kwa taarifa yake hakuna Mkuu wa mkoa wa wilaya anamuogopa, maana wao ndio waliratibu na kusimamia uchaguzi uliowaingiza ccm madarakani.

Sasa kama walijiingiza kwenye siasa, hadi yeye akawa mbunge hatimaye waziri, ni kipi atawazuia kufanya? Isitoshe huyo waziri Ummy sio aliyewateua hao wakuu wa mikoa na wilaya, hivyo hana lolote anaweza kuwafanya.
 
Huyo waziri Ummy anapiga siasa za kichovu na kuchekesha walionuna. Kwa taarifa yake hakuna Mkuu wa mkoa wa wilaya anamuogopa, maana wao ndio waliratibu na kusimamia uchaguzi uliowaingiza ccm madarakani. Sasa kama walijiingiza kwenye siasa, hadi yeye akawa mbunge hatimaye waziri, ni kipi atawazuia kufanya? Isitoshe huyo waziri Ummy sio aliyewateua hao wakuu wa mikoa na wilaya, hivyo hana lolote anaweza kuwafanya.
Ngoja tuone!
 
Mara ya mwisho mkuu wa wilaya kukamata Daktari ilikuwa lini? Halafu hayo mambo yalikuwa kawaida yeye alipokuwa waziri wa afya, sikuizi kukiwa na shida viongozi wa serikali za mitaa wanakimbilia kwa Dr Gwajima.

Ummy ziara zake mikoani anatembelea vituo vya akikaa akiamka anawaza wizara ya afya huyo dada inabidi aelewe katika shughuli za TAMISEMI wizara ya afya ina waziri anayeimudu. Ajikite kukamalisha majengo, kupeleka vifaa tiba na wafanyakazi mambo ya operation amuwachie Dr Gwajima.

TAMISEMI ina matatizo luluki yeye kila siku afya tu, wakati alipokuwepo hapo kila siku alikuwa anaangaika na MDS huko kwenye operation wala alikuwa ajali.

Pilipili asoila inamuwashia nini.
 
Back
Top Bottom