Waziri Ummy: Kuna upendeleo Taasisi ya mifupa (MOI)

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
1470300244738.jpg

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, Watoto na Walemavu, Ummy Mwalimu amesema kuwa amebaini katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kuna upendeleo na hakuna utaratibu wa wazi katika kutoa huduma za matibabu.

Jana, Mwalimu alifanya ziara ya kushtukiza MOI na kuagiza kambi za upasuaji zilizokuwa zikifanyika mwishoni mwa wiki zirudi mara moja ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaosubiri upasuaji.

“Nimewaambia waweke wazi utaratibu wa upasuaji, kama siyo majina basi watumie hata namba ili mgonjwa ajue, lingine wanatakiwa kurudisha utaratibu wa kambi za upasuaji maana wodi zimejaa wagonjwa wanaosubiri huduma hiyo,” amesema Ummy.

Chanzo: Mwananchi
 
Zoezi la kuhakiki watumishi lifike mwisho;Watumishi Afya wamelemewa.Unaongeza Kambi-- bila labour force!!Na hiyo iliyopo haipo motivated,what do you expect??Yaani....
 
huko muhimbili kuna jipu kubwa sana, kuna mtu aliumia mwezi wa saba kaambiwa atafanyiwa operation mwezi wa 9! eti kuna foreni!
 
Hilo sio jipu, muhimbili kuna population kubwa ya wagonjwa tena wengine wamepangiwa tarehe lkn wapo majumbani. Hospitali imezidiwa, tuache kuhukumu, tutafute suluhisho la kudumu kwa kuziwezesha hospitali za mikoa kwa wataalam na vifaa. Masuala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari hayaleti afya wala motivation kwa watoa huduma. Cha msingi ni kukaa pamoja na kuangalia utatuzi, kuelekeza sio tiba bali kujadili na kufikia muafaka ndio tiba. Naamini Serikali inatazama masuala haya kwa mapana yake, huenda Hospitali ya Mloganzila itapunguza tatizo hili.
Watanzania tumezidi kulalamika mno hadi inakera. Doctors are human like you they cant work 24/7. Vifaa ni vichache, vyumba vya upasuaji ni vichache na mahala pa kuwalaza wagonjwa wa upusuaji hapatoshi!!! Utatuzi wa changamoto hizi si kuongeza vitanda muhimbili bali kuzipa uwezo hospitali za mikoa au kuanzisha hospitali za kanda zenye uwezo wa kiwango cha juu kabisa hii itasaidia kupunguza msongamano muhimbili. Nimekuwa miongoni mwa waathirika wa tatizo la muhimbili mgonjwa wangu hakupata matibabu kwa wakati mwanzoni nilikuwa mlalamishi ila baadaye nilielewa. Hatukatai uzembe, huo upo kila sehemu.
 
sasa kama tatizo ni kubwa hivyo yule naibu waziri mbona anakomaa na docta mwaka badala ya kuadress hizi ishu nyeti!!!!???
 
Kwani Magufuli hakuyamaliza matatizo ya Muhimbili?
Teh teh ndo mana JK alipofikia kipengele cha Muhimbili wakati wa makabidhiano ya ofisi kwa Magu alicheka?
 
huko muhimbili kuna jipu kubwa sana, kuna mtu aliumia mwezi wa saba kaambiwa atafanyiwa operation mwezi wa 9! eti kuna foreni!
Wewe ulitaka iweje?
Kama mnaparamia mapiki piki kama vichaa kwa siku mnavunjika mpaka 50 au 60 lakin uwezo wa hospital uko vile vile unategemea nn?
 
Nilitegemea kuna mtu flan mahari flan a-act accordingly
Wewe ulitaka iweje?
Kama mnaparamia mapiki piki kama vichaa kwa siku mnavunjika mpaka 50 au 60 lakin uwezo wa hospital uko vile vile unategemea nn?
Nilitegemea kuna mtu flan mahari flan a-act accordingly
 
Hilo sio jipu, muhimbili kuna population kubwa ya wagonjwa tena wengine wamepangiwa tarehe lkn wapo majumbani. Hospitali imezidiwa, tuache kuhukumu, tutafute suluhisho la kudumu kwa kuziwezesha hospitali za mikoa kwa wataalam na vifaa. Masuala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari hayaleti afya wala motivation kwa watoa huduma. Cha msingi ni kukaa pamoja na kuangalia utatuzi, kuelekeza sio tiba bali kujadili na kufikia muafaka ndio tiba. Naamini Serikali inatazama masuala haya kwa mapana yake, huenda Hospitali ya Mloganzila itapunguza tatizo hili.
Watanzania tumezidi kulalamika mno hadi inakera. Doctors are human like you they cant work 24/7. Vifaa ni vichache, vyumba vya upasuaji ni vichache na mahala pa kuwalaza wagonjwa wa upusuaji hapatoshi!!! Utatuzi wa changamoto hizi si kuongeza vitanda muhimbili bali kuzipa uwezo hospitali za mikoa au kuanzisha hospitali za kanda zenye uwezo wa kiwango cha juu kabisa hii itasaidia kupunguza msongamano muhimbili. Nimekuwa miongoni mwa waathirika wa tatizo la muhimbili mgonjwa wangu hakupata matibabu kwa wakati mwanzoni nilikuwa mlalamishi ila baadaye nilielewa. Hatukatai uzembe, huo upo kila sehemu.
Hela ya kuhamia Dodoma ingepelekwa kuboresha hospitali z wilaya...tmk, mwananyamala, mnazimmoja, vijibweni n.k.n.k

Kisha kuboresha vifaa tiba na posho na mishahara ya madaktari.

Malalamiko yasingekuwepo
 
Hilo sio jipu, muhimbili kuna population kubwa ya wagonjwa tena wengine wamepangiwa tarehe lkn wapo majumbani. Hospitali imezidiwa, tuache kuhukumu, tutafute suluhisho la kudumu kwa kuziwezesha hospitali za mikoa kwa wataalam na vifaa. Masuala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari hayaleti afya wala motivation kwa watoa huduma. Cha msingi ni kukaa pamoja na kuangalia utatuzi, kuelekeza sio tiba bali kujadili na kufikia muafaka ndio tiba. Naamini Serikali inatazama masuala haya kwa mapana yake, huenda Hospitali ya Mloganzila itapunguza tatizo hili.
Watanzania tumezidi kulalamika mno hadi inakera. Doctors are human like you they cant work 24/7. Vifaa ni vichache, vyumba vya upasuaji ni vichache na mahala pa kuwalaza wagonjwa wa upusuaji hapatoshi!!! Utatuzi wa changamoto hizi si kuongeza vitanda muhimbili bali kuzipa uwezo hospitali za mikoa au kuanzisha hospitali za kanda zenye uwezo wa kiwango cha juu kabisa hii itasaidia kupunguza msongamano muhimbili. Nimekuwa miongoni mwa waathirika wa tatizo la muhimbili mgonjwa wangu hakupata matibabu kwa wakati mwanzoni nilikuwa mlalamishi ila baadaye nilielewa. Hatukatai uzembe, huo upo kila sehemu.
Pamoja na wingi wa wagonjwa lkn ruswa imetawala kuna wagonjwa wanaingia pale na siku hiyo hiyo wanafanyiwa upasuaji wanaondoka na kuwaacha waliokuwepo muda mrefu na matatizo kama yake
 
Ndo maana Ummy akasema kuna upendeleo.. haiwezekani watu wanasubiri foleni lakini wengine hawasubiri..!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom