Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa Corona nchini waliobaki kwenye vituo vya matibabu imepungua mno.

Akizungumza Leo mkoani Tanga wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani humo amesema:

“Tanga hatuna mgonjwa wa Corona, Amana wamebaki 3, Mloganzila 1, Kibaha 0, Mwanza 0”.

Ummy amesisitiza kuwa Corona bado ipo na kuwataka watanzania kuendelea kujikinga.

“Na mimi nilisema pale Dodoma, katika Uwaziri wangu sikuwahi kupitia kipindi kigumu kama hiki cha Corona kwakweli nilihenya” amesema Waziri Ummy Mwalimu.
 
Hivi inawezekana ikawa tumetumia mbinu gani kulishinda hili janga hivi, Kwa mbinu yoyote tuliyotumia kwanini tusi share na ulimwengu ili kunusuru dunia na hili janga

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulimwengu walidharau sana.Wasipotubu kwa dhihaka zao kipindi kile taifa letu linamlilia Mungu,sasa si waendelee kutumia hizo mbinu za kisayansi walizosema sisi tumeziacha.Hii kitu itawasumbua sana.wacha sisi tuendelee kupiga kazi.Watanzania pigeni kazi kipindi cha kutajirika ndiyo hiki.majirani watakuwa na njaa.mitaji yao itakuwa imekata by the time wanapata akili
 
So kilichotuponya watanzania ni maombi na sala? Sasa tufunge basi na kusali kwa ajili ya dunia. Tuwaombee na wao basi
 
Mungu Ameturehemu Watanzania. Mungu ni Mwema. Ee Muumba wa Mbingu na Dunia.... Tunasema Asante kwa Rehema hii KUU katika ardhi ya Tanzania. Asante kwa kutulinda na kutuponya Gonjwa hili Novel COVID - 19
 
Hivi inawezekana ikawa tumetumia mbinu gani kulishinda hili janga hivi, Kwa mbinu yoyote tuliyotumia kwanini tusi share na ulimwengu ili kunusuru dunia na hili janga

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi umeona kinachoendelea marekani..?
Korona ingekuwa bado ni tishio nani angeenda kuandamana kiasi kile..?
Watu hawajali uhai wao kisa mtu mmoja!! He he! Tutajionea mengi.
 
Back
Top Bottom