Waziri Ummy ataka wanafunzi wasisome masomo ya ziada wakati wa likizo

Pre form one na pre form five zina tatizo gani?

Kwanza sio lazima ni maamuzi ya mzazi ampeleke mtoto wake au asimpeleke.

Alichokataa waziri ni ile tabia inayoota mizizi siku hizi shule zikifungwa mwezi wa 6 au 12 kuna baadhi ya shule za serikali na private wanawazuia wanafunzi wasipumzike inakuwa ni lazima kwenda shule kwa kigezo cha masomo ya ziada tena wazazi wanashurutishwa kuchangia pesa za hiyo program.

Hiko nafkiri ndo alichokikataza waziri.
Ndugu zetu wanashindwa kututembelea likizo kwa sababu ya upuuzi wa kusoma likizo shuleni.

Ni upuuzi kuwapeleka watoto shule likizo kama siku za kawaida.
 
Pre form one na pre form five zina tatizo gani?

Kwanza sio lazima ni maamuzi ya mzazi ampeleke mtoto wake au asimpeleke.

Alichokataa waziri ni ile tabia inayoota mizizi siku hizi shule zikifungwa mwezi wa 6 au 12 kuna baadhi ya shule za serikali na private wanawazuia wanafunzi wasipumzike inakuwa ni lazima kwenda shule kwa kigezo cha masomo ya ziada tena wazazi wanashurutishwa kuchangia pesa za hiyo program.

Hiko nafkiri ndo alichokikataza waziri.

Zina tatizo kwa sababu wanalazimisha.Hivi pre form five inasaidia nini hasa???
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote nchini kuhakikisha wanasimamia suala la wanafunzi kupumzika wakati wa likizo ili kuwapatia watoto muda wa kujifunza masuala mengine ya Kijamii.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo baada ya kupata maelekezo ya kisera kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia Profesa Joyce Ndalichako ambaye amemtaka kulisisitiza suala hilo ili wanafunzi hao waweze kupata muda wa kupumzika kipindi cha likIzo

Akihutubia kwenye Mahafali ya 29 ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo Waziri Ummy amesema watoto wanatakiwa kupumzika majumbani kipindi cha likizo ili waweze kusaidia kufanya kazi ndogondogo nyumbani, kusoma dini na kusaidia kufanya biashara ndogo za kuwasaidia wazazi pale wanapokuwa likizo.

“Sasa hivi elimu imegeuzwa kama biashara, watoto wamekuwa wakisoma masomo ya ziada mpaka kipindi cha likizo, hawapumziki, pia wazazi huchangia fedha fedha kwa ajili ya masomo hayo, ya ziada, watoto hawafaulu kwa kusoma muda mrefu, hivyo nawaagiza wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanalisimamia hili” amesisitiza Waziri Ummy

Amesema Serikali imepanga muda wa vipindi wa masaa nane, ikiamini muda huo wanafunzi wataweza kujifunza kwa kina masomo yote yaliyopangwa kwa siku, hivyo amewataka Wakurugenzi kuwaelekeza wakuu wa shule kusitisha masomo ya ziada mpaka saa mbili usiku, jumatatu hadi jumapili naagiza kusitishwa mara moja kwa kuwa hatuwajengi watoto,tunawaharibu kwa kuwachosha kusoma muda wote bila kupata muda wa kupumzika.

MICHUZI BLOG
Yote ni baada ya wadau kutiririka hapa JF kwani walikuwa hawalijui hilo.
Nut!!
 
Ingawa kipindi Cha magufuli matamko mengi ya viongozi yalikuwa yanafuatiliwa na yanatekelezwa ila kwa Sasa sijui kama hili litafuatiliwa ili Hali itendeke
 
Duuh hii hatari.

Pesa inatafutwa kwa kila njia.

Watoto wanachoka sana.Tuwasemee!
Kweli darasa la 4 anasoma toka saa 12 alfajiri hadi saa 11 jioni plus jumamosi!Sidhani kama elimu ni ngumu hivyo.Wanataka akae boarding na ukikataa adhabu yako inakuwa kumpeleka mapema/ na jumamosi umpeleke asubuhi na kumchukua mchana.
Elimu yetu inahitaji regulation kuwasaidia watoto
 
Kweli wanachoka sana kama unavo waona hapo chini
Screenshot_20211127-203603_WhatsApp.jpg
 
Hongera ummy Mwalimu, wewe ni Mwalimu kweli umenifuraisha Sana. Hongera Tena watoto walikuwa wanasoma mpaka saa 2 usiku na wanakwenda mpaka Jumamosi mpaka 10 jioni. Watoto ufika nyumbani saa 4 usiku. Watoto wamekupenda Sana Ummy.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom