Waziri Ummy ametoa siku 60 hospitali zote nchini kufunga mfumo wa kielectroniki wa mahudhulio

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Waziri Ummy Mwaimu ametoa muda wa siku 60 hospitali za Serikali nchi nzima wawe wamefunga mfumo wa kieletroniki wa mahudhulio kwa Wafanyakazi.

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo Leo Jumatano Disemba 5, 2018 alipotembelea hospitali ya Tandahimba iliyopo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara ambapo anahimiza Wananchi kujiunga na huduma ya mfuko wa Bima ya afya na pia amekagua utolewaji wa huduma ya afya hospitalini hapo.
FB_IMG_1543992803311.jpeg
 
Hiyo mbona ipo hospital nyingi sana.. Mpaka taasisi na vyuo
Labda huko mbwinde ndo hakuna
 
*"Nawapongeza Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba kwa kuweka kifaa maalum cha kielektroniki cha kusaini mahudhulio ya Watumishi. Wilaya ya Tandahimba ni mfano bora wa kuigwa. Natoa siku 60 Hospitali zote za Serikali za mikoa na wilaya ziwe zimefunga kifaa hiki"*

- Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Disemba 5, 2018 Wilayani Tandahimba)
FB_IMG_1544026847053.jpg
 
Back
Top Bottom