Waziri Ummy ahimiza viwanda vya dawa zenye ubora,salama na ufanisi

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
*Waziri Ummy Mwalimu ahimiza Viwanda vya Dawa Zenye Ubora, Salama na Ufanisi*

Katika kuunga mkono Sera ya Uchumi wa Viwanda ya Mh. Rais Dkt. John Magufuli, Wawekezaji wa ndani watakiwa kujenga viwanda vya dawa huku wakihimizwa kufuata vigezo vya uzalishaji wa dawa ili kuweza kupata soko la ndani la bidhaa zao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua *Maabara hamishika 10 za kudhibiti ubora na usalama wa dawa mapema leo katika viunga vya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) jijini Dar es salaam* . Mhe Ummy amesema Wizara ya Afya inaunga mkono azma ya Mhe Rais ya ujenzi wa Viwanda na hivyo anawahimiza wawekezaji kujenga viwanda vya dawa na kwamba Wizara yake ipo tayari kununua dawa hizo zitakazozalishwa ila tu pale ambapo zitakuwa zimekidhi vigezo vya ubora, usalama na ufanisi.

Aidha, Mhe Ummy ameeleza kuwa Serikali kupitia TFDA itaongeza jitihada za kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa dawa nchini hasa kwa kuimarisha mpango mahususi wa uchunguzi wa awali wa Dawa unaohusu uchunguzi wa Dawa muhimu za Kifua Kikuu, Dawa za ARV, Dawa za Malaria pamoja na Viuwa sumu. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha dawa zote zinazozalishwa au kuingizwa nchini ni bora, salama na zenye ufanisi.

Akiongea katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo alisema kuwa kutokana na kuongezeka kwa Maabara hamishika itasaidia kuwabaini na kuwakamata wahalifu wanaoingiza na kuuza dawa duni na bandia. Sillo aliongeza kuwa mwaka 2005 wastani wa dawa bandia ulikuwa 3.7% wa dawa zilizokuwepo nchini huku takwimu za 2017 zinaonyesha kushuka kwa dawa bandia kwa chini ya 1% jambo ambalo ni mafanikio kwa taasisi hiyo. TFDA imenunua Maabara Hamishika 10 zenye thamani ya shilingi milioni 100 ili kuongeza nguvu ya kuhakikisha dawa zinazoingizwa na kuuzwa nchini zinakidhi vigezo vya ubora, usalama na ufanisi.
 
Viwanda Ni mzimu unao haunt viongozi na blindly utasikia viwanda vya wanyamapori, viwanda vya vifaa vya elimu, viwanda vya madawa, viwanda vya samaki na mifugo etc. Tunajenga viwanda kwa midomo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom