Waziri Ummy aagiza kuapishwa wakuu wa Wilaya kesho

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,645
2,000
ummypicc

Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu ameagiza wakuu wa mikoa kuwaapisha Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa kuanzia kesho Jumatatu Juni 21, 2021.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Jumapili Juni 20, 2021 muda mchache baada ya kumaliza ziara yake yake ya kukagua ujenzi wa stendi ya mabasi ya Mwenge.

“Kesho Jumatatu wote waanze mchakato wa kuwaapisha Wakuu hawa wa Wilaya. Kusiwe na kisingizio chochote, kama kuna sababu basi Jumanne mchakato huu ukamilike ili Jumatano waanze kazi mara moja.

“Waende wakaripoti kwenye vituo vyao vya kazi kwanza kisha baadaye warudi kwa ajili ya utaratibu wa kuhama. Wakuu wa Mikoa wote warudi kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya kuwaapisha Wakuu Wilaya wamechelewa sana basi wafanye Jumanne,” alisema Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, wakuu walioteuliwa jana ni 139 kati yao 56 wapya na 83 wamebaki. Alifafanua kwamba waliobaki 83 kati 26 wamebakishwa kwenye vituo vyao huku wengine wakihamishwa katika maeneo mbalimbali ili kuimarisha utendaji.

“Wote walioteuliwa wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa kasi, uadilifu, uaminifu na ubunifu kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Lakini kubwa lililonifurahisha katika hii orodha kuna Wakuu Wilaya 44 wanawake sawa na asilimia 31 namshukuru Rais kwa kuendelea kutoa nafasi kwa kundi hili.

MWANANCHI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom