Waziri:Ugonjwa wa nguruwe uliua 4,476 mwaka jana

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
UGONJWA wa homa ya nguruwe uliojitokeza mwaka jana umeua nguruwe 4,476 katika wilaya nane hapa nchini na kusababisha baadhi ya wilaya kuwekewa karantini.

Hayo yalibainishwa bungeni jana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo David wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2012/13.

Dk Mathayo alizitaja wilaya ambazo zilikumbwa na ugonjwa huo na idadi ya nguruwe waliokufa ikiwa kwenye mabano ni pamoja na Makete (80), Sumbawanga (1,933) na Njombe (803).

Kwa mujibu wa Dk Mathayo ambaye pia ni Mbunge wa Same Magharibi, wilaya nyingine na idadi ya vifo ni Kilombero (715), Mufindi (250), Kilosa (70), Iringa (296), Kilolo (329).

Katika kukabiliana na ugonjwa huo, hatua mbalimbali zilichukuliwa ikiwa ni pamoja na kuweka karantini, kudhibiti usafirishaji wa nguruwe na mazao yake pamoja na kutoa elimu kwa umma.

Dk Mathayo ambaye aliliomba Bunge kuidhinisha Sh54.5 bilioni za matumizi ya kawaida na maendeleo,alisema Serikali imeanza kuainisha maeneo huru ya magonjwa ya mifugo ya milipuko.

Alisema milipuko hiyo ya magonjwa imekuwa ni kikwazo katika biashara ya mifugo na mazao yake kimataifa ili kuwawezesha wafugaji kufuga kibiashara na kuwaongezea kipato.

Alisema katika mwaka uliopita wa fedha (2011/12), Serikali iliziainisha Wilaya za Sumbawanga na Nkasi mkoani Rukwa kuwa za kunenepesha mifugo.

“Wilaya hizo zitatumika kunenepesha mifugo, kuchinja na kuuza nyama bora ndani na nje ya nchi na ramani ya maeneo huru ya magonjwa katika
wilaya hizo imekamilika,” alisema.

Wakati huo huo, Dk Mathayo aliliambia Bunge kuwa, Serikali imedhamiria kuvirudisha Serikalini vitalu namba 287/1 ,287/3 na 287/7 huko Misenyi
ambavyo vimekuwa na migogoro ya muda mrefu kutokana na kuvamiwa na wafugaji na mifugo kutoka nchi jirani.

Waziri alisema vitalu hivyo vitatolewa kwa taasisi za umma na kwamba wawekezaji waliokuwa katika vitalu hivyo watagawiwa maeneo mbadala
yanayomilikiwa na Narco.

Katika hatua nyingine, Serikali imezindua mpango wake wa kuwalipa kifuta machozi, wafugaji katika mikoa ya kaskazini ambao mifugo yao ilikufa mwaka 2008/09 kutokana na ukame.

Waziri Mathayo alisema chini ya mpango huo tayari Rais Jakaya Kikwete aliikabidhi Wilaya ya Longido Ng'ombe 500 na Mbuzi 30 wenye thamani ya
Sh213 milioni Februari mwaka huu.

Dk Mathayo alisema , mpango huo uliendelea ambapo kwa kuanzia Wilaya ya
Monduli ilipewa Sh205.63 milioni na Wilaya ya Ngorongoro Sh218 huku ununuzi wa ng'ombe 500 kwa kila wilaya ukiendelea.

Waziri:Ugonjwa wa nguruwe uliua 4,476 mwaka jana
 
Hizi takwimu si sahihi Mh. Mathayo. Mimi nilipoteza nguruwe 68 shambani kwangu kwa ugonjwa huo lakini hakuna hata ofisa ughani mmoja aliyekuja kuniuliza. Naomba uongezee hao 68 kwenye hesabu yako.
 
Back
Top Bottom