Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashashu Kijaji, amesema kasi ya serikali yake katika ukusanyaji wa kodi inaweza kufanikisha kukusanya hada Shs. 22 trilioni, ambazo ni sawa na bajeti yam waka 2015/2016.
Akizungumza wakati wa kuzindua Programu ya Uboreshaji Mapato kwa udhamini wa Serikali ya Norway leo hii, Dk. Kijaji amesema serikali yake kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejipanga kufikia malengo yake iliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato kila mwezi.
“Nadhani umeona katika kipindi hiki kifupi tangu serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani, kila mwezi tumefikia malengo ya ukusanyaji wa kodi, sasa kama tukiendelea na kasi hii, sioni kwa nini mapato yetu yasifikie Shs. 22 trilioni, ambazo ni sawa na bajeti yetu yam waka huu wa fedha,” alisema.
INGIA HUKU UISOME KWA UREFU