Waziri Tibaijuka awafutia vigogo hati za ardhi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,868
1,225
Thursday, 08 September 2011 19:54
prof%20anna%20tibaijuka.jpg
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka​
Fidelis Butahe

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ameanza kuchukua hatua kali, kukabiliana na uvamizi, uporaji na rushwa katika sekta ya ardhi nchini na kisha kutangaza kufuta hati za viwanja 42 jijini Dar es Salaam.

Mbali na kufuta hati hizo, Profesa Tibaijuka pia ametangaza kwamba halmashauri za majiji, Manispaa na miji nchini ambazo zimekithiri kwa migogoro ya ardhi, zitanyang’anywa madaraka yake na kurudishwa chini ya wizara yake.

Profesa Tibaijuka alitangaza mpango huo jijini Dar es Salaam jana huku akisisitiza: “Tunaanza kwa kasi zaidi na nguvu zaidi na kurejesha hali salama katika miji yetu”.

Hati zafutwa Dar
Akizungumzia hali ilivyo katika Jiji la Dares Salaam, Profesa Tibaijuka alisema katika wilaya zake tatu, wilaya ya Kinondoni inaongoza kwa kuwa na maeneo ya wazi 88 yaliyovamiwa kati ya 110 yaliyochunguzwa.

Waziri Tibaijuka alisema; “Kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyote haruhusiwi kufanya maendeleo mjini bila kibali cha maandishi kutoka mamlaka za mipango miji”.

Alisema hati za viwanja zilizofutwa mpaka sasa ni 42 ambazo viwanja 12 vipo eneo la Mikocheni mabwawa ya maji na viwanja 30 vipo Mbezi.

Tibaijuka alisema eneo la bwawa la maji lililopo Mikocheni limevamiwa na kupimwa viwanja 12(namba 1116-1127). Alisisitiza kuwa viwanja hivyo ni batili na vimefutwa.

“Hivi sasa hakuna atakayeweza kuishi kwa ujanjaujanja jijini Dar es Salaam, kama una hati yako, lakini una mashaka nayo nenda kamuone Kamishna wa Ardhi mapema,” alisema Tibaijuka,

Aliongeza: “ Kama una kiwanja umeshindwa kukiendeleza kwa miaka mitatu kitachukuliwa, ila kwa sasa Wizara ya Ardhi haitapima viwanja mpaka kuwe na barabara ili kuwezesha maeneo hayo kuwa na huduma muhimu za jamii jambo ambalo litawafanya wananchi kujenga nyumba kwa wingi,”.

Profesa Tibaijuka alisema mpango huo umebarikiwa na Rais Jakaya Kikwete na kwamba, amemuhakikishia kuwa kila kitu lazima kitatekelezwa kwa kufuata sheria.

“Hati miliki zote zilizotolewa kinyume na sheria zitafutwa kama ilivyofanyika katika eneo la Ocean Road, Palm Beach, Jangwani Beach na Mbezi Beach,” alisema Tibaijuka.

Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi Duniani (UN-HABITAT), alisema ametoka katika shirika hilo kwa lengo la kufanya kazi katika wizara hiyo, hivyo kitendo cha kukithiri kwa migogoro ya ardhi kinamnyima nafasi ya kutekeleza majukumu yake.

Alisema kwamba, uchunguzi uliofanywa katika maeneo ya wazi 153 ya manispaa tatu za Jiji la Dar es Salaam na Kamati iliyoundwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, William Lukuvi, ulibaini kuwapo kwa udanganyifu mkubwa.

“Maeneo 88 sawa na asilimia 80 kati ya maeneo 110 ya wazi yaliyopo Manipsaa ya Kinondoni yamevamiwa,” alisema Tibaijuka.

Alisema katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala maeneo ya wazi yaliyokaguliwa ni 30 ambapo kati ya hayo 11 yamevamiwa sawa na asilimia 37.

“Manispaa ya Temeke inaonekana kuwa na asilimia ndogo ya uvamizi ambapo yalibainika maeneo matano sawa na asilimia 30 ya maeneo 14 yaliyotembelewa,” alisema Tibaijuka.

Waziri Tibaijuka alisema wananchi wanaoishi katika maeneo ya wazi na kando ya Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam, wanatakiwa kuondoka.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Goodluck ole Madeye, alisema jijini Dar es Slaam eneo la Kawe ndio linaongoza kwa kuwagawa maeneo kiholela.

“Haturidhiki na utendaji huo mfano ni Mto Kawe ambao hivi karibuni ulivamiwa huku uongozi wa Serikali ya Mtaa ukilifumbia macho suala hilo,” alisema Ole Madeye.

Ulikokithiri ufisadi
Katika hatua nyingine, Profesa Tibaijuka amesema wizara yake itaendelea na mpango wake wa kuzinyang’anya madaraka halmashauri zilizokithiri kwa migogoro ya ardhi na kurudisha jukumu hilo Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tibaijuka alitoa angalizo kuwa, mamlaka za upangaji miji zikikiuka sheria waziri mwenye dhamana ya ardhi ana mamlaka ya kutengua uamuzi wa mamlaka hizo.
“Halmashauri hizo zitatajwa hivi karibuni…, hapa nataka wananchi watambue kwamba kukasimu madaraka kwa halmashauri hizi sio kigezo cha wao kufanya watakavyo,” alifafanua.

Alisisitiza; “Mtu yoyote anayejijua kuwa hati yake si halali ajue wazi kuwa amepoteza haki yake, hatutakuwa na huruma hata kidogo kama ataona kaonewa aende kufungua kesi mahakamani,” alisema Tibaijuka.

Alisema miji huendelezwa kwa kufuata mipango ya jumla mitatu, ambayo ni mipango kabambe ya muda na mipango ya kina.

“Mipango kabambe ipo 21 ya muda 29 na mipango ya kina ni 5,000,” alisema Tibaijuka.

Alisema kumekuwa na tabia ya ubadilishaji wa matumizi ya ardhi kiholela, yakiwemo maeneo ya wazi na yale ya umma yaliyotengwa kwa matumizi ya huduma za jamii.

Alisema maendeleo hayo husimamiwa na halmashauri za jiji, manispaa, miji na wilaya chini ya usimamizi wa Wizara ya Ardhi.

“Huu ni mpango maalum kuhusu uvamizi wa ardhi na mabadiliko holela ya matumizi ya ardhi na mpango huu tayari umeshaanza kazi,” alisema Tibaijuka.

Awaonya wananchi
Tibaijuka aliwaonya wananchi kuwa macho ili wasitapeliwe na baadhi ya maofisa wa wizara hiyo wasiokuwa waadilifu.

“Pamoja na hayo, kama itadhihirika kuwa kuna watumishi wa wizara wasiokuwa, waadilifu watachukuliwa hatua,” alisema Tibaijuka.

Alisema ardhi ya kijiji haiwezi kuchukuliwa kienyeji na mtu yoyote, bila idhini ya Rais na kuwataka wananchi kutoamini maneno yanayozunguzwa mitaani kuwa ardhi za vijiji zimeuzwa.

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,356
2,000
Turudie sera za uwazi na ukweli: Viwanja vilivyofutwa na wamiliki wake vitangazwe hadharani ili wananchi wote tuone na kujua. Na kama kuna majumba yavunjwe mbele ya waandishi wa habari ili tujuzwe. Hii ya kutoa takwimu tu bado sijaikubali.
 
mKaLI_mOkO

Member
Aug 6, 2011
25
20
Ni lini Tanzania tutaexercise transparency ya kweli...waziri atujuze hivo viwanja na wamiliki wao waliofutiwa hati.
 
Morinyo

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
2,782
2,000
Sijajua anaposema kua ukichukua kiwanja ukashindwa kukiendeleza kwa mda wa miaka mitatu kinachukuliwa anamanisha viwanja vya aina gani.Kwa watumishi wa kawaida unaweza ukanunua kiwanja na ikapita miaka mitatu mpaka minne kabla hujajenga hata msingi kutokana na kipato kua kidogo. Ukimlazimisha mtu kama huyu kukiendeleza anaweza akaingia ktk njia ambazo si nzur( mfano ufisadi) ili kukiendeleza.
 
Mambina

New Member
Sep 9, 2011
2
0
Prof. Rejea swali la nyongeza la Mhe. kangi mbunge wa Mwibara, wapo waliojenga viwanda vinaning'inia majini kando kando ya ziwa Victoria. Na hao vipi?
 
Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
3,969
2,000
Hebu mama piga kazi kama anavyopiga kazi kaka yako magufuli hata ile value ya doctorate yake inaonekana,sasa nawe tunataka tuone value ya huo uprofesor wako.
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,434
2,000
mbona hasemi kuwafutia walio katika makazi ambayo wizara yake imeshindwa kuyapima na watu wamejenga kiholela eg sala sala, mbagala, kimara. mezi louis etc???!!! Na hao wizara yake ina mpango gani nao??
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,362
2,000

Thursday, 08 September 2011 19:54
prof%20anna%20tibaijuka.jpg
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka​

Fidelis Butahe

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ameanza kuchukua hatua kali, kukabiliana na uvamizi, uporaji na rushwa katika sekta ya ardhi nchini na kisha kutangaza kufuta hati za viwanja 42 jijini Dar es Salaam.

Mbali na kufuta hati hizo, Profesa Tibaijuka pia ametangaza kwamba halmashauri za majiji, Manispaa na miji nchini ambazo zimekithiri kwa migogoro ya ardhi, zitanyang'anywa madaraka yake na kurudishwa chini ya wizara yake.

Profesa Tibaijuka alitangaza mpango huo jijini Dar es Salaam jana huku akisisitiza: "Tunaanza kwa kasi zaidi na nguvu zaidi na kurejesha hali salama katika miji yetu".

Hati zafutwa Dar
Akizungumzia hali ilivyo katika Jiji la Dares Salaam, Profesa Tibaijuka alisema katika wilaya zake tatu, wilaya ya Kinondoni inaongoza kwa kuwa na maeneo ya wazi 88 yaliyovamiwa kati ya 110 yaliyochunguzwa.

Waziri Tibaijuka alisema; "Kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyote haruhusiwi kufanya maendeleo mjini bila kibali cha maandishi kutoka mamlaka za mipango miji".

Alisema hati za viwanja zilizofutwa mpaka sasa ni 42 ambazo viwanja 12 vipo eneo la Mikocheni mabwawa ya maji na viwanja 30 vipo Mbezi.

Tibaijuka alisema eneo la bwawa la maji lililopo Mikocheni limevamiwa na kupimwa viwanja 12(namba 1116-1127). Alisisitiza kuwa viwanja hivyo ni batili na vimefutwa.

"Hivi sasa hakuna atakayeweza kuishi kwa ujanjaujanja jijini Dar es Salaam, kama una hati yako, lakini una mashaka nayo nenda kamuone Kamishna wa Ardhi mapema," alisema Tibaijuka,

Aliongeza: " Kama una kiwanja umeshindwa kukiendeleza kwa miaka mitatu kitachukuliwa, ila kwa sasa Wizara ya Ardhi haitapima viwanja mpaka kuwe na barabara ili kuwezesha maeneo hayo kuwa na huduma muhimu za jamii jambo ambalo litawafanya wananchi kujenga nyumba kwa wingi,".

Profesa Tibaijuka alisema mpango huo umebarikiwa na Rais Jakaya Kikwete na kwamba, amemuhakikishia kuwa kila kitu lazima kitatekelezwa kwa kufuata sheria.

"Hati miliki zote zilizotolewa kinyume na sheria zitafutwa kama ilivyofanyika katika eneo la Ocean Road, Palm Beach, Jangwani Beach na Mbezi Beach," alisema Tibaijuka.

Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi Duniani (UN-HABITAT), alisema ametoka katika shirika hilo kwa lengo la kufanya kazi katika wizara hiyo, hivyo kitendo cha kukithiri kwa migogoro ya ardhi kinamnyima nafasi ya kutekeleza majukumu yake.

Alisema kwamba, uchunguzi uliofanywa katika maeneo ya wazi 153 ya manispaa tatu za Jiji la Dar es Salaam na Kamati iliyoundwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, William Lukuvi, ulibaini kuwapo kwa udanganyifu mkubwa.

"Maeneo 88 sawa na asilimia 80 kati ya maeneo 110 ya wazi yaliyopo Manipsaa ya Kinondoni yamevamiwa," alisema Tibaijuka.

Alisema katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala maeneo ya wazi yaliyokaguliwa ni 30 ambapo kati ya hayo 11 yamevamiwa sawa na asilimia 37.

"Manispaa ya Temeke inaonekana kuwa na asilimia ndogo ya uvamizi ambapo yalibainika maeneo matano sawa na asilimia 30 ya maeneo 14 yaliyotembelewa," alisema Tibaijuka.

Waziri Tibaijuka alisema wananchi wanaoishi katika maeneo ya wazi na kando ya Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam, wanatakiwa kuondoka.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Goodluck ole Madeye, alisema jijini Dar es Slaam eneo la Kawe ndio linaongoza kwa kuwagawa maeneo kiholela.

"Haturidhiki na utendaji huo mfano ni Mto Kawe ambao hivi karibuni ulivamiwa huku uongozi wa Serikali ya Mtaa ukilifumbia macho suala hilo," alisema Ole Madeye.

Ulikokithiri ufisadi
Katika hatua nyingine, Profesa Tibaijuka amesema wizara yake itaendelea na mpango wake wa kuzinyang'anya madaraka halmashauri zilizokithiri kwa migogoro ya ardhi na kurudisha jukumu hilo Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tibaijuka alitoa angalizo kuwa, mamlaka za upangaji miji zikikiuka sheria waziri mwenye dhamana ya ardhi ana mamlaka ya kutengua uamuzi wa mamlaka hizo.
"Halmashauri hizo zitatajwa hivi karibuni…, hapa nataka wananchi watambue kwamba kukasimu madaraka kwa halmashauri hizi sio kigezo cha wao kufanya watakavyo," alifafanua.

Alisisitiza; "Mtu yoyote anayejijua kuwa hati yake si halali ajue wazi kuwa amepoteza haki yake, hatutakuwa na huruma hata kidogo kama ataona kaonewa aende kufungua kesi mahakamani," alisema Tibaijuka.

Alisema miji huendelezwa kwa kufuata mipango ya jumla mitatu, ambayo ni mipango kabambe ya muda na mipango ya kina.

"Mipango kabambe ipo 21 ya muda 29 na mipango ya kina ni 5,000," alisema Tibaijuka.

Alisema kumekuwa na tabia ya ubadilishaji wa matumizi ya ardhi kiholela, yakiwemo maeneo ya wazi na yale ya umma yaliyotengwa kwa matumizi ya huduma za jamii.

Alisema maendeleo hayo husimamiwa na halmashauri za jiji, manispaa, miji na wilaya chini ya usimamizi wa Wizara ya Ardhi.

"Huu ni mpango maalum kuhusu uvamizi wa ardhi na mabadiliko holela ya matumizi ya ardhi na mpango huu tayari umeshaanza kazi," alisema Tibaijuka.

Awaonya wananchi
Tibaijuka aliwaonya wananchi kuwa macho ili wasitapeliwe na baadhi ya maofisa wa wizara hiyo wasiokuwa waadilifu.

"Pamoja na hayo, kama itadhihirika kuwa kuna watumishi wa wizara wasiokuwa, waadilifu watachukuliwa hatua," alisema Tibaijuka.

Alisema ardhi ya kijiji haiwezi kuchukuliwa kienyeji na mtu yoyote, bila idhini ya Rais na kuwataka wananchi kutoamini maneno yanayozunguzwa mitaani kuwa ardhi za vijiji zimeuzwa.

watu hamna shukrani, angalau huyu amaenza. Waliopita wote ilikuwa babaisha tu. Mwache jamani aende taratibu. Wavamizi ni watu highly placed lazima ku-deal nao kisheria kuliko kukurupuka.
 
dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,726
1,500
Mbona maafisa ardhi walijimilikisha viwanja vingi katika mpango wa viwanja 20,000 jijini Dar na sasa leo ni mapori wakiviuza bei mbaya. Matokeo yake ni maarufu kwa majambazi na wachache waliojenga wanaishi kwa hofu. Huyu mama sioni anachofanya pale wizarani. mkataba wa offer unasema kiwanja kinatakiwa kimeendelezwa kwa muda wa Miaka mitatu. sasa hivi ni takribani miaka 7 ni mapori tu. HAna analofanya huyu mama. Kuna watu wanataka viwanja lakini maafisa ardhi wamevishikiria kwa tamaa ya utajiri.
 
AirTanzania

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
1,139
2,000
Siiamini Serikali ya Magamba, Wanajua sana kuhadaa Wadanganyika Wataje viwanja na Majina sio kutututangazia ukiwa nawaweza kupitisha Bajeti kwa Kutumia Bahasha watashindwajwe kudanganya
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,012
2,000
Tibaijuka naye siasa zitamshinda very soon kwa sababu zifuatazo:

1. Utendaji wake tangu ameingia madarakani ni wa Dar es Salaam tu. Mikoa mingine kwake yeye haiexist.

2. Utendaji wake ni wa kubomoa tu. Anakiri kuwa watu wamepewa hati feki, lakini asemi toka wapi. Jiu ni kwamba wamepewa hati feki na wizara yake. Kitakachofuata ni mlolongo wa kesi. Tukumbuke kesi hizo zina gharama.

3. Anashindwa kuelewa kuwa, kimsingi hakuna anayetaka kujenga kiholela. Kinachofanya watu kurisk pesa zao kujenga kiholela ni kwamba ofisi yake iko corrupt mno. Ukitaka kufuata hatua za kihalali utatumia mamilioni kabla hujapata karatasi inayokuruhusu kuchimba msingi.

4. Anajisahau kuwa jukumu kubwa lililo mbele yake ni kuplan sehemu ambazo bado hazijaguswa. Wakati yeye anapoteza muda na maeneo yaliyokwisha vamiwa, anaacha sehemu kubwa ya jiji na nchi kwa ujumla haijapimwa. Hii inasababisha makazi kuwa shaghala baghala na yatakuwa hayapimiki tena. Hivyo basi, kwa sasa aende Goba, Majohe, Kijichi etc ambako hakujapimwa.

5. Hata katika sehemu chache zinazopimwa anashindwa kuhakikisha kuwa ugawaji wa viwanja hivyo unakuwa wa haki. Viwanja vyote vinachukuliwa na maofisa wa ardhi, then wanawauzia wananchi kwa beio kubwa zaidi. Sasa kama anashindwa kuwadhibiti watu wachache walio chini yake, ataweza kudhibiti wafanya biashara?

6. Anashindwa kujua kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siyo UN Habitat.
 
Anheuser

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
1,947
1,225
Ukitaka kufuata hatua za kihalali utatumia mamilioni kabla hujapata karatasi inayokuruhusu kuchimba msingi.
Hii kali. Na ukitaka kupitia njia zisizo halali ni bure?

Ni kitu gani kinagharimu mamilioni kupata building permit kihalali?
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,012
2,000
Hii kali. Na ukitaka kupitia njia zisizo halali ni bure?

Ni kitu gani kinagharimu mamilioni kupata building permit kihalali?

Rushwa si kingine.
Rushwa hiyohiyo ndio iliyolegitimize tabia ya kujenga kiholela. Mark my words, Tibaijuka hawezi kubomoa asilimia 80 ya nyumba alizozitaja.
Majengo hayaoti kama uyoga, yanajengwa kwa jitihada kubwa za siku nyingi. Na hayajengwi kwa siri, yanajengwa mchana kweupe. Kama si rushwa ni nini kingine kinachoweza kulegitimize tabia hiyo?
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,012
2,000
Hii kali. Na ukitaka kupitia njia zisizo halali ni bure?

Ni kitu gani kinagharimu mamilioni kupata building permit kihalali?

Ukipitia njia ambazo sio halali si bure, ndio maana watu wanajenga.
Tibaijuka anaongea tu lakini hakuna atakachofanya. Approach yake imekaa ki UN Habitat na si Ki Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tofauti kati ya hivi viwili ni kwamba UN Habitat mkikubaliana jambo, wote mnashirikiana kulitekeleza na anayekiuka anapata fair treatment whereas katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkikubaliana kitu kwenye kikao watu wanakitumia kama mtaji wa kukusanyia rushwa na hakuna anayeadhibiwa kwa hilo.
Hii kauli ya Tibaijuka ni mtaji kwa maafisa ardhi, sasa wanaenda kukusanya rushwa tena kwa waliowapa hizo hati feki. Na narudia tena, Tibaijuka hana uwezo wa kubomoa nyumba zilizo kwenye asilimia 80 ya open space.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,602
2,000
Hebu mama piga kazi kama anavyopiga kazi kaka yako magufuli hata ile value ya doctorate yake inaonekana,sasa nawe tunataka tuone value ya huo uprofesor wako.
<br />
<br />
anakuwa prof. wa ukweli kisa kafuta hati! ccm imetutenda mpaka tumekuwa wapumbavu, bora tungebaki wajinga. eti hawatapima viwanja mpaka barabara zijengwe, zilizopo hakuna budget ya matengenezo, mpya ndiyo zina fungu, mama akumbuke maneno yake, kasi ya maendeleo ya serikali ni ndogo kuliko kasi ya maendeleo ya wananchi,
 
marregal

Member
May 8, 2011
77
70
anapiga kazi kwa makini, hakurupuki, matunda tutayaaona baada kama magufuli alivofanya bila utanii
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,012
2,000
<br />
<br />
anakuwa prof. wa ukweli kisa kafuta hati! ccm imetutenda mpaka tumekuwa wapumbavu, bora tungebaki wajinga. eti hawatapima viwanja mpaka barabara zijengwe, zilizopo hakuna budget ya matengenezo, mpya ndiyo zina fungu, mama akumbuke maneno yake, kasi ya maendeleo ya serikali ni ndogo kuliko kasi ya maendeleo ya wananchi,

Nimeipenda hiyo. Huo ndio ukweli.
Huyu mama hajui how much watu wanastruggle to make ends meet, yeye anazungumzia kubomoa. What about kujenga, we should start with that.

Maeneo yenyewe ya wazi yamejaa ofisi za matawi ya CCM, ofisi za serikali za mitaa, vituo vidogo vya polisi etc. Hii inathibitisha kuwa tatizo ni la mfumo na hulitatui kwa kuanza kubomoa wakati as we speak kuna maeneo mengine ya wazi ndio kwanza yanajengwa na hakuna stop order iliyotolewa. Later atakuja kusema na hayo nayo anayabomoa, kazi ya wizara itakuwa kubomoa tu, mpaka lini?

Mama pima viwanja, wauzie wananchi. Kama wameweza kujenga kwenye maeneo ya wazi then wanaweza kujenga kwenye viwanja halali kama vipo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom