Waziri TAMISEMI tusaidie Tabora, Walimu hawafundishi

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,146
884
Mh, Waziri, Tabora Walimu hawafundishi, wanavunja vipindi kwa kulazimishwa kwenda kupanda miti, wiki mbili za mwanzo mwezi Januari zimekwenda na maji kazi kupanda miti.

Wiki hii tena Mkuu wa Mkoa kaanzisha tena Watumishi wote wapande miti na Walimu hakuna kufundisha ni kupanda miti, tena hakuna kutumia wanafunzi, yani Walimu wanaacha vipindi wanapanda miti.

Halafu watasema Syllabus haijaisha.

Chukua hatua haraka Mh Waziri kuokoa Elimu Tabora.
 
Duuh! Kumbe ni kote, nami nilipita huko Ijumaa ya wiki iliyopita nikakutana na wanafunzi wamezagaa barabarani kama saa 3 hivi au 4 asubuhi wakipanda miti wilayani Nzega
 
Ni lazima tufanikishe azimio la Mkuu Wa Mkoa madarasa hapo tu kwani yanabomoka. Wataka aondolewe kwenye uteuzi halafu utampa kula weyee..(jocking mtoa mada;);)).
 
Siasa kila mahali hata pasipo stahili , lengo la kupanda miti ni zuri ila njia zinazotumika sio sawa, zina athari kubwa sana katika elimu, Mwalimu akikosa vipindi kwa wiki mbili mfululizo kwa kupanda miti badala ya kufundisha ni kosa na pia inawanyima haki watoto wanaostahili kufundishwa.
Ila kwa kuwa nchi inaongozwa kwa matamko bila kufuata katiba, kanuni, taratibu na sheria, TUSUBIRI NA TUONE.
 
Umemchongea RC bure, kwanza Tabora na Elimu wapi na wapi? Naelewa hamumpendi kwasababu kawabana sana wanywa kahawa na kushinda vibarazani na zile tabia zenu za kiswahili kuiba iba sasa mnamtafutia zengwe. Mie niko Tabora na naikubali sana kasi ya mshua. Tabora ni wavivu sana kwa mtu kama Mwanri ni lazima apigwe vita tu, hamtafanikiwa kwa hila zenu
 
Back
Top Bottom