Waziri Tamisemi aonya wakuu wa mikoa, wilaya wanaoweka watu kizuizini ovyo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Dodoma. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia vibaya madaraka yao ya kukamata watu walio kwenye himaya zao.

Ametoa onyo hilo leo (Ijumaa) alipojibu maswali ya wabunge waliotaka kufanyika marekebisho ya sheria inayowapa mamlaka wakuu hao ya kuwakamata na kuwaweka ndani wananchi wanaowatuhumu kwa lolote.

Licha ya kubainisha kwamba sheria hiyo haina tatizo, waziri amesisitiza: "Ukamataji unatakiwa ufanywe kwa mtu aliyetenda kosa la jinai au anayehatarisha usalama. Isiwe kwa show-off tu. Na mhusika anatakiwa kufikishwa mahakamani mara moja, asishikiliwe tu."

Amesisitiza kwamba wakuu hao ni wawakilishi wa Serikali kwenye maeneo yao, hivyo hawatakiwi kutumia vibaya madaraka waliyokasimiwa.

Katika siku za karibuni wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakilalamikiwa kuwaweka watu kizuizini pasipo kuwa na sababu za msingi, miongoni mwao wakiwamo waandishi wa habari.
 
Anataka kutumbuliwa,Magu wakati anawaapisha alisema mna yale mamlaka ya kuwaweka watu ndani,sasa nendeni mkayatumie!
 
Makonda alisema kimadaraka na kimshahara RC na WAZIRI wanalingana tu,hahah.Simbachawene atawapiga mkwara ma RC wote lkn yule mtoto mpendwa wa Baba atajifanya kama hajamuona vile.
 
simba%283%29.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Mhe.GEORGE SIMBACHAWENE amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia mamlaka yao vibaya ya kuwaweka ndani viongozi,watumishi wa umma na wananchi wengine kwa uonevu kwa kisingizio cha sheria kuwapa mamlaka hayo.

Kauli hiyo ya Waziri SIMBACHAWENE ameitoa bungeni ikiwa ni baada ya wabunge kuhoji uwepo wa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kutoa amri ya kukamatwa kwa watu bila sababu ya msingi hivyo ni hatua gani serikali inachukua dhidi yao kukomesha tabia hiyo.

Amesema licha ya sheria kuwapa viongozi hao mamlaka hayo wanapaswa kuwa makini wanapoitumia kama sheria inavyotamka kwa kuzingatia mipaka yao ya kazi katika kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa.

Sheria ya tawala za mikoa ya mwaka 1997 sura ya 97 inawapa mamlaka wakuu wa mikoa na wilaya kumweka ndani mtu ye yote kwa muda wa saa48 ikiwa itathibitika kuna hatari ya uvunjifu wa amani na usalama au mtu huyo ametenda kosa la jinai.chanzo; ITV
 
Tangu tuanze kupiga kelele alikuwa hajui au ni kujitoa akili.

Nasubiri kuona hilo agizo linatekelezwa, huku Bashite kwenye jiji lake nasikia vilema wamekamatwa kisa walikatazwa kuingia mjini na baiskeli zao
 
Wa dar ameshasema analingana na mawaziri na waziri hana mamlaka ya kumuwajibisha kwani wote wameteuliwa na mtu mmoja.

Mliokuwa nae karibu huyo waziri mumkumbushe kuwa kama anaitaka hiyo kazi aache iyo mikwara
 
"Ukamataji unatakiwa ufanywe kwa mtu aliyetenda kosa la jinai au anayehatarisha usalama. Isiwe kwa show-off tu. Na mhusika anatakiwa kufikishwa mahakamani mara moja, asishikiliwe tu''.

Hivi sheria inasemaje kama itathibitika mkuu wa Mkoa/Wilaya labda alitoa amri ya kumuweka mtu ndani kwa show-off tu? au hawaguswi hawa?
 
Back
Top Bottom