Waziri Sophia Simba - Mwenyekiti Mpya UW-CCM (Taifa)

Wakulu,

Bado hakieleweki huko ufisadini UWT? tupeni updates wakuu tunazisubiri kwa hamu.

Natanguliza shukurani.
 
Mkuu Mtu Wa Kawaida, nimekumbuka kale kamwimbo ka marehemu Mbaraka Mwinshehe na Moro Jazz...

hilo woo woo
ulijidai wewe mbabe sana
leo umepigwa na kijana mdogo
aibu imekupata

kiko wapi
ulichokuwa ukijidi nacho
je ungepambana na mimi sasa
kilema ungekipata

Ooho kebehi na majivuno yako, yako wapi sasa
aibu imekupata.....

Wadau mpambano huu ataimbiwa mtu, maana siku hizi hakuna sera ni bifu!

....Ooho NGEBE na majivuno yako,
yamekwisha sasa heshima iko wapi,
Ulipotoka shamba kuingia mjini,
mimi nimekuona huwezi kunishinda
kujitia mikogo na kudharau wenzio,
leo umefundishwa adabu na heshimaa,


...........those were the dayz!
 
- Unajua ndio maana nilisema mapema sana kwamba wote wagombea wawili walitakiwa kuondolewa, yaliyojiri kwenye huu uchaguzi ni aibu kubwa sana kwa taifa letu, mapesa ni mengi mno yaliyotumika kwa sababu ya uwt tu? Na haya mapesa yametolewa na wagombea wote wawili sio siri! Tena Mama Janet ndiye ametumia hela nyingi mno shame kwa wote wawili, lakini zaidi kwa Mama Janet shame on you!

- Yaani uenyekiti wa Umoja wa wanawake ambao zamani hata hatukujua kama huwa unagombewa maana mimi nilidhani Mama Sophia Kawawa ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kudumu, sasa all over sudden imekua patashika mpaka wakuu wa taifa kuhusika, kulikoni? Haya mapesa kina Sophia na Mama Janet ya kutupa namna hii wanayatoa wapi? Ninasema hivi hizi hela za kumwaga namna hii kama karanga wanatoa wapi?


Mkulu FMES,
Toka mwanzo niliapa kutozungumzia chaguzi Mbili,Hii ya UVCCM na UWT kwa sababu kuu Mbili.

1.Ni kwa magogoni kuhusika na hizi Kampeni,nimekuwa nikiona watu wa magogoni wamkeuwa mstari wa mbele kuhsuiak na hizi kampeni na nafikia kusema kwamba inawezekana pesa ya kasma ilitumika katika kufanikisha ushindi wa Benno na wa huyu mama Simba

2.Kitendo cha mama Salma kumpigia kampeni sophia nacho kilinishtua sana na nilifadhaika sna kusikia familia ya mkulu nayo imejiingiza katika siasa.Hivyo hivyo riz alikuwa katika kampeni za kijana benno

Nachoogopa ni kuwa kwanini Familia ya mkulu imeamua kuingia katika kampeni za siasa ??au mkulu alishaona kuwa kuna watu wanataka kumungusha(Yes we know that).Ila tuendeko ni kule masikini watakuw masikini zaidi na according to the dataz ni kuwa Riz atagombea ubunge 2010 katika moja ya majimbo ya ukanda huu wa Pwani!
 
Once you are the chairperson of UWT, you are automatically Mbunge. 2010 huna expense`yeyote ya kutafuta kura. Uko assured kuwa "employed " mpaka 2015.
 
Hata kama automatically anakuwa mbunge, je mshahara na marupurupu ya ubunge wake pamoja na yale ya UWT yanaweza kurudisha 2billion. Ama kuna biashara zingine. Hebu nielewesheni wakuu!
 
I can confirm kuwa SOFIA SIMBA kashinda pamoja na Janet Kahama kutumia zaidi ya dola milioni 2 lakini looks like fitna ya Sofia ilikuwa si mchezo...

Anyway kuja jambo lilitokea mle ndani na ni kosa la wasimamizi wa Janet ambalo atakuja kulijutia sana


ES hebu nicheki

Mkuu GT, asante ktuhabarisha.

Mwenzake naye ametumia ngapi?
 
Wadau,

Hivi Sophia Simba atapata wapi muda wa kufanya kazi zote kama Mbunge, waziri na mwenyekiti wa UWT?

Wakati mamilioni ya watu hawana kazi, hawa wengine wanahodhi vyeo na kushindwa ku deliver.
 
Mkuu FMES umenikuna sana kwa hili infwakti hata mimi nilijua hivyo, nimeshangazwa sana eti kuna kampeni ya mtu kuwa mwenyekiti UWT........... Bado nacheka nikisoma post yako. Ni mambo ya aibu............ waziri anayesimamia uwt nyingine anatoa rushwa kama karanga. Hv huo uenyekiti UWT ni zadi ya uwaziri???????

Uchaguzi UWT: Nguvu ya fedha, makundi kuamua mshindi

Uchaguzi UWT: Nguvu ya fedha, makundi kuamua mshindi

Mwandishi Wetu
Januari 7, 2009

UWEZO wa mgombea katika kuongoza ni kigezo kilichopigwa teke ndani ya chaguzi mbalimbali za jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Badala yake, nguvu za makundi na fedha ndivyo vigezo vinavyokumbatiwa zaidi kwa ushirikiano baina ya wagombea na wapiga kura.

Hayo ndiyo mazingira yanayougubika mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa CCM. Na wakati wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika mazingira hayo, wana-CCM nje ya mkutano huo wanajiuliza nani Mwenyekiti mpya wa UWT?

Ndiyo! Nani mwenyekiti mpya wa UWT hili ni swali ambalo hata wewe msomaji unasubiri jibu. Jibu ambalo litapatikana baada ya kukamilika kwa mkutano huo mkuu wa umoja huo unaoanza leo mjini Dodoma.

Wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa niaba ya wana-UWT wenzao wanajukumu kubwa la kumtafuta mrithi wa Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Anna Abdallah (68).

Mwenyekiti wa UWT, Anna Abdallah

Mwenyekiti wa UWT, Anna Abdallah

Anna Abdallah aliyezaliwa Julai 26, mwaka 1940 alikuwa na sifa za kutosha za kuwa kiongozi, ni msomi wa kiwango cha chuo kikuu, aliyewahi kuongoza wizara mbalimbali nchini. Wizara hizo ni pamoja na Wizara ya Afya, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Kazi.

Katika uongozi wa kisiasa, Anna Abdallah ameshika nyadhifa mbalimbali ukiwamo uenyekiti wa UWT Taifa, aliokuwa nao tangu mwaka 1994. Nyadhifa nyingine alizowahi kushikilia ni ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu wa Wilaya wa TANU na Katibu wa Mkoa wa TANU.

Tunaweza kusema Anna ni kiongozi mwenye mafanikio katika medani ya uongozi. Sifa zake hizo ni changamoto nyingine ya ziada kwa wapiga kura katika kumsaka mrithi wake katika UWT.

Bila shaka, hilo ni jukumu zito kwa wajumbe wapiga kura na hasa kwa kuzingatia mazingira magumu yanayogubika uchaguzi huo kama hali inavyoonyesha.

Namna wajumbe wanavyoshawishiwa katika kumchagua mwenyekiti mpya, ndiyo msingi wa ugumu wa mazingira ya uchaguzi huo utakaomuibua mshindi atakayemrithi mtu aliyeongoza umoja huo kwa takriban miaka 14.

Mazingira hayo magumu yanatokana na matakwa ya ukweli yanayobainisha kuwa katika hali ya kawaida, kiongozi bora wa kuchaguliwa hupatikana kwa msisitizo wa sifa bora, hata ufisadi ni sifa kwa washirika wa mafisadi, lakini si sifa bora mbele ya umma na kwa mtu anayetakiwa kuwa kiongozi.

Sifa za kiongozi bora ni pamoja na uwezo binafsi wa kufikiri kwa maslahi ya wengi, na pia uwezo binafsi katika kushirikisha au kushirikiana na wadau wengine ili hatimaye kuharakisha mafanikio yanayokidhi matarajio ya umma.

Lakini katika uchaguzi huu wa UWT, kama ilivyo kwa chaguzi nyingine za jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama Umoja wa Vijana (UVCCM), kinachojidhihirisha ni mshindi kutafutwa kwa mizengwe.

Mizengwe inayopuuza sifa ya uwezo binafsi wa mgombea na kukumbatia maslahi ya makundi ya kisiasa na mbinu nyingine za kifisadi, hususan matumizi ya fedha.

Tunaweza kusema ile misingi iliyokuwa inatawala chaguzi za CCM katika kumpata kiongozi bora ndani ya chama imepoteza mwelekeo. Upotezaji huu wa mwelekeo umewahi kuthibitishwa mara kadhaa na viongozi waandamizi wa chama hicho, akiwamo Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete.

Itakumbukwa kuwa wakati anafungua Mkutano Mkuu wa UVCCM mwishoni mwa mwaka jana, Rais Kikwete alidokeza kuhusu uchaguzi uliopita wa viongozi wa umoja huo kutiwa mikono na wanasiasa nje ya umoja huo na baadhi wakipenyeza rupia.

Hivyo si makosa kusema kuwa chaguzi za chama hicho na jumuiya zake zimekuwa zikipoteza mwelekeo. Ni chaguzi, zisizovutia na wala si darasa bora la kupigiwa mfano kwa wasomi wanaopata fursa ya kuwasilisha mada katika mihadhara maeneo mbalimbali ya nchi, au nje ya nchi.

Ni chaguzi zinazoambatana na hoja zilizobobea katika kupandikiza fitina, chuki na kusambaratishana. Hoja zenye mwelekeo wa kuhatarisha upendo na kuabudu mifarakano. Ni chaguzi zinazoimarisha tofauti za makundi ya kisiasa.

Katika chaguzi hizo hoja zinazotawala ni uimarishaji wa kambi za kisiasa. Haya yote ni mazingira magumu yanayogubika mkutano mkuu wa UWT mjini Dodoma.

Sasa imekuwa jambo la kawaida wapiga kura katika chaguzi ndani ya CCM kupiga kwa misingi ya kambi za kisiasa, badala ya misingi inayozingatia kumpata kiongozi bora.

Kwa bahati mbaya, wajumbe ambao ni wapiga kura wengi hawaoni tatizo hili. Eti utawasikia baadhi yao wakidai mkono mtupu haulambwi. Wajumbe wa mikutano ya uchaguzi katika CCM na jumuiya zake nao wamekuwa tatizo, wanashiriki kuua ustaarabu wa chaguzi katika chama chao.

Hivyo ni dhahiri kuwa baadhi ya wapiga kura ndani ya chaguzi hizi za CCM, ukiwamo huu wa UWT wamo waliopoteza mwelekeo. Na inawezekana nao walichaguliwa kuwakilisha wenzao katika mkutano huo baada ya kushiriki ufisadi, kwa njia ya kuhonga wajumbe.

Na ukweli ni kwamba kuna kila dalili kuwa katika uchaguzi wa UWT mkoani Dodoma watakuwapo wapiga kura waliokwishapoteza mwelekeo. Hata hivyo, jambo la kuomba ni kwamba idadi ya wajumbe wapiga kura waliopoteza mwelekeo isizidi ya wale wenye mwelekeo.

Kama ikitokea waliopoteza mwelekeo ni wengi basi UWT itakuwa na kiongozi aliyepoteza mwelekeo kabla hata ya kuanza kutimiza majukumu yake kama kiongozi mpya.

Lakini mbali na hayo, yapo mazingira mengine ya changamoto katika mkutano huo mkuu wa uchaguzi wa UWT, Dodoma.

Kwa mfano, unapozungumza na baadhi ya wapiga kura kwa maana ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT utawasikia wakisema mgombea fulani tunamuunga mkono kwa sababu ni wa kambi yetu.

Na ikibidi, utawasikia wakikueleza mgombea fulani ni wa kambi ya wale na yule ni wa kambi ile. Jambo la kusikitisha hapa ni kwamba kambi hizi zimegeuka kuwa za kudumu. Si kambi za muda tu, zenye malengo ya kuendesha kampeni nyakati za kampeni, la hasha!

Ni kambi za kudumu, na matokeo ya hali hii ni kuwapo kwa baadhi ya wapiga kura wanaomnyima kura mgombea mwenye sifa za kuwa kiongozi bora, eti si wa kambi yao. Huku nako ni kupoteza mwelekeo.

Wanaogombea nafasi hiyo ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora; Mbunge wa Viti Maalumu, Janet Kahama na Mbunge mwingine wa Viti Maalumu, Joyce Masunga.

Mbunge wa Viti Maalumu, Joyce Masunga

Mbunge wa Viti Maalumu, Joyce Masunga

Wagombea hawa wanakwenda kupigiwa kura ndani ya mazingira hayo magumu kama ilivyoelezwa awali.

Dalili zinaonyesha kuwa, wagombea Janet Kahama na Sophia Simba ndiyo wanaoonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda, hasa kwa kuzingatia mwenendo wa kampeni zao.

Kampeni zao zimekuwa na mvutano mkali. Itakumbukwa kuwa Septemba 15, mwaka jana baadhi ya magazeti nchini yaliripoti mvutano baina ya wagombea hawa wawili. Baadhi ya vichwa vya habari vitakavyokumbukwa ni Waziri Simba, Kahama wagombana.

Ilidaiwa kuwa ugomvi huo ulizuka wakati wa kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es Salaam, kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoani humo, John Guninita.

Ikadaiwa pia kuwa wajumbe wa kikao hicho walijikuta katika kazi ya ziada kutuliza jazba za akina mama hao. Kikao hicho kilikuwa mahsusi kupitisha majina ya wagombea mbalimbali za nafasi za uongozi katika UWT.

Chanzo cha ugomvi kilidaiwa kuwa ni uamuzi wa Waziri Sophia Simba kudai katika kikao hicho kuwa mshindani wake (Kahama), amekuwa akimtukana na kumchafulia jina kwa wajumbe kwamba hatosheki na nafasi za uongozi alizonazo.

Inadaiwa kuwa Waziri Simba aliendelea kusema yeye ni mtoto wa mjini na kwamba Mama Kahama hawezi kushindana naye kwa lolote lile, huku akitumia lugha ya mitaani iliyomfanya Mama Kahama ashindwe kujizuia.

Kutokana na vijembe hivyo, ikadaiwa kuwa Janet Kahama alishindwa kuvumilia na kuamua kujibu mapigo.

Gazeti la moja nchini lilinukuu chanzo chake cha habari katika kikao hicho kikisema; “Wakati Waziri Simba akiendelea kusema, Mama Kahama alisimama na kuanza kusema: ‘Sijakutukana, sijakutukana, hizi nafasi ni za Mungu, kwa nini tuvunjiane heshima.”

“Kuona hivyo, wajumbe tuliamua kuingilia kati kwa kuwashika, huku wengine wakimsaidia Mama Kahama, kwani alikuwa amepandisha presha.”

Inadaiwa kuwa Waziri Simba amekuwa akijinadi kuwa wametumwa na Rais Jakaya Kikwete kuwania kiti hicho.

Faida za mshindi wa kiti hicho ni kuwa mjumbe wa vikao vya juu vya CCM, vya Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC).

Wagombea hao waliulizwa kuhusu taarifa za kulipuka kwa ugomvi wao, kila mmoja akawa na majibu yake.

Kahama alikataa kuzungumzia akitaka aachwe. Lakini Waziri Simba akasema; “Kikao chetu kilikuwa cha siri, habari hizo umezipata wapi? Mimi ni kiongozi makini, najua ninachokifanya, siwezi kutoa siri ya kikao, labda umfuate huyo aliyekuambia.”

Lakini kwa mujibu wa gazeti hilo, Waziri huyo alipobanwa zaidi alisema yaliyotokea ndani ya kikao hicho ni mambo ya kawaida ya vikao vyao na kusisitiza yaliyojadiliwa ni siri ya kikao na hayapaswi kutoka nje.

Mbali na Waziri Simba na Janet Kahama, waombaji wengine wa awali katika nafasi ya uenyekiti wa UWT Taifa ni pamoja na Joyce Masunga, Halima Mamuya, Odina Lujaji na Zerulia Maneno.

Hata hivyo, wengine walienguliwa na waliobaki ni Janet Kahama, Sophia Simba na Joyce Masunga.

Baada ya kuripotiwa kwa mvutano huo, Mwenyekiti wa CCM, ambaye ndiye aliyekuwa akiongoza kikao kilichoshuhudia mvutano wa Kahama na Simba, John Guninita, akakanusha kuwapo kwa ugomvi, akisema wagombea hao walilumbana tu kikaoni.

Kwa mujibu wa Guninita, kikao hicho cha Kamati ya Siasa Dar es Salaam kilikutana Septemba 12 mwaka huu, kujadili majina ya wagombea uongozi wa UWT ngazi ya mkoa.

"Ni kweli kila mmoja alikuwa na hasira, lakini si kweli kabisa kwamba yuko kiongozi yeyote miongoni mwa hawa wawili aliyemrushia mwenziwe ngumi na kutoa lugha ya matusi kama ilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari," anasisitiza.

Ujumbe mahsusi kwa wagombea hawa watatu ni ule uliowahi kutolewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, katika mkutano mkuu maalumu ya UWT uliofanyika mjini Dodoma Julai 27, mwaka 2007, kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Amina Salum Ali, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa UWT, ambaye aliteuliwa kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika (AU), nchini Marekani.

Katika mkutano huo, Rais Kikwete aliwapa changamoto wajumbe na viongozi wa umoja huo aliowaita dada zake akisema; “Ujumbe wangu kwa kifupi ni kwamba ningependa kuona kwamba UWT inaendelea kuwa kimbilio, kiongozi, tumaini na ngao ya mwanamke wa Tanzania.

“Ningependa kuona UWT inashika hatamu za uongozi wa wanawake wa Tanzania bila kuyumba wala kuyumbishwa.”


Wanawake wamfitinisha Waziri Simba na Kikwete

Wanawake wamfitinisha Waziri Simba na Kikwete

Mwandishi Wetu
Januari 7, 2009

Vita yake na Janeth Kahama yazidi kupamba moto

WAKATI Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) ukitarajia kupata mwenyekiti wake mpya wiki hii, kumekuwapo na hujuma dhidi ya demokrasia itakayofanikisha mchakato wa kumpata mwenyekiti huyo, Raia Mwema imebaini.

Miongoni mwa mambo yaliyoibuka ni kutajwa kwa Rais Jakaya Kikwete kumuunga mkono mmoja wa wagombea wa naasi hiyo, Waziri wake wa Utawala Bora, Sophia Simba, madai ambayo yameshindwa kuthibitishwa na uongozi wa juu wa CCM uliopelekewa.

Pamoja na kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Sophia Simba ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, nafasi ambayo inatafsiriwa kuwa imetokana na kuwa kwake karibu na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Sophia Simba

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Sophia Simba

Mbali ya kutajwa kwa Rais Kikwete ambaye ndiye atakayefungua rasmi mkutano wa UWT leo Jumatano, tuhuma za rushwa na kuchafuana kwa wagombea ni mambo yaliyotawala kampeni za kuelekea uchaguzi wa jumuiya hiyo yenye nguvu ndani ya chama tawala.

Baadhi ya wapambe wamefikia hatua ya kusambaza ujumbe wa maneno kupitia simu za mkononi za baadhi ya wajumbe wakitumia ugonjwa wa mmoja wa wagombea kama sababu ya kutaka asichaguliwe kushika nafasi hiyo ya uongozi wa UWT. Nafasi hiyo inawaniwa pia na wabunge wa Viti Maalumu Janet Bina Kahama na Joyce Masunga.

Wagombea kupitia wapambe wao inadaiwa wanahujumu mkondo wa demokrasia ya mmojawao kuchaguliwa kumrithi mwenyekiti anayemaliza muda wake, Anna Abdallah.

Inadaiwa kuwa baadhi ya washiriki wa kampeni za wagombea hao walilazimika kusafiri na baadhi ya wajumbe kuelekea Dodoma katika kile kilichoelezwa kuwa kuwathibiti wasibadili mawazo ya kumchagua mgombea wa kundi wanalounga mkono.

Wajumbe waliojikuta wakisafiri na wapambe wa wagombea hao ni pamoja na wanaotoka katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Wajumbe wengine kutoka mikoa ya Kusini walijikuta wakizuiwa kwa muda jijini Dar es Salaam katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni “kuwekwa sawa.”

Baadhi ya wajumbe wamejikuta wakigharimiwa huduma za malazi jijini Dar es Salaam, kabla ya kuelekea mjini Dodoma kupiga kura.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wajumbe hao wamekuwa hodari katika kutoa ushirikiano ili kupewa rushwa na wapambe wa wagombea hao.

Habari kutoka mjini Dodoma zinaeleza kuwa wapambe wa baadhi ya wagombea waliwasili mjini hapo siku kadhaa, baadhi ya wagombea waliwasili mjini hapo siku kadhaa kwa ajili ya kuwapokea wajumbe wapiga kura.

Lakini wakati wapambe hao wakiwa wamewasili Dodoma kabla ya wajumbe kuwasili, washindani wao walilazimika kusafiri hadi katika mikoa wanakotoka wajumbe hao na kusafiri nao kuelekea Dodoma.

Kilele cha uchaguzi huo kinafikiwa wakati wagombea Sophia Simba na Mbunge wa Viti Maalumu, Janet Kahama wakiwa katika mvutano na mchuano mkali.

Kumekuwapo na malalamiko kutoka katika kila upande kuhusiana na kuchezeana ‘rafu’ na zaidi ni kambi mbili za Janet Kahama na ile ya Waziri Simba.

Mbunge wa Viti Maalumu, Janet Kahama

Mbunge wa Viti Maalumu, Janet Kahama

Janet Kahama kama ilivyo kwa Joyce Masunga ni wabunge wa Viti-Maalumu na ukweli ni kwamba mchakato wa kupata wabunge wa aina hiyo huhusisha ushindani ikiwa ni pamoja na kupigiwa kura na wajumbe maalumu katika mikoa wanakogombea.

Hata hivyo, madai kwamba Waziri Simba ametumwa na mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kugombea nafasi hiyo yamekwishakanushwa.

Madai hayo si mara ya kwanza kutajwa, yamewahi kujitokeza katika kinyang’anyiro cha viongozi wa juu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) pia.

Mara kadhaa, Rais Kikwete mwenyewe amesikika akikanusha madai hayo. Lakini wakati Waziri Simba akiwa katika mazingira hayo, mgombea Janet Kahama naye anadaiwa kuungwa mkono na mwenyekiti anayemaliza muda wake, Anna Abdallah.

Haijafahamika ni kwa nini Anna Abdallah amuunge mkono mgombea huyo, lakini inawezekana ni imani yake kuwa mama huyo aliyepishana naye miaka mitatu kiumri (Anna akiwa mkubwa zaidi) ataweza kuongoza umoja huo kwa tija zaidi.

Lakini licha ya kuwapo kwa madai hayo, Anna Abdallah hakuwahi kusikika hadharani akiyapinga, lakini pia hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa anamuunga mkono Janet Kahama.

Wakati wagombea hao wakiwa na mazingira hayo, mgombea mwingine Joyce Masunga naye anatajwa kuwa na kigogo anayemuunga mkono.

Baadhi ya wajumbe wa UWT wanadai kuwa anaungwa mkono na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

Tofauti na wenzake hao wawili, Masunga amekuwa akiendesha kampeni za kimya kimya, na kwa wanasiasa wengine waliozoea mikikimiki ya kampeni wanadai kuwa mwenendo wa kampeni za mgombea huyo zinaweza kumwangusha.

Anna Abdallah anaondoka madarakani baada ya kuongoza UWT kwa miaka 14. Aliingia madarakani mwaka 1994, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Sophia Kawawa, aliyefariki dunia.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa, endapo mmojawapo kati ya Sophia au Kahama atashinda kiti hicho, uongozi wake huenda ukakabiliwa na changamoto nyingine ndani ya umoja huo.

Kuna uwezekano mkubwa changamoto hizo zikawa zinaibuliwa na kundi la mshindani atakayeshindwa ili hatimaye kuthibitisha kuwa ilikuwa ni makosa kwa mhusika kuchaguliwa kutokana na uwezo duni kiutendaji.

Hali hiyo inatabiriwa kwa kuwa wito wa kuvunja makundi ndani ya CCM umekuwa ukipuuzwa licha ya wito huo kutolewa na viongozi wa juu, akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Rais Kikwete.

Nafasi ya Uenyekiti wa UWT kama ilivyo kwa jumuiya nyingine za chama hicho, ina umuhimu wa pekee kutokana na anayeshika nafasi hiyo kuingia moja kwa moja katika vikao vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.

Kuwa mjumbe wa Kamati Kuu CCM mwaka mmoja kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kuna umuhimu mkubwa kisiasa, si tu kwa mjumbe husika bali pia kwa wanasiasa wengine wakiwamo wagombea wa nafasi za kisiasa katika dola ikiwamo Urais na Ubunge.

Ni kwa ajili hii wanasiasa wengi makini wametupa karata zao katika uchaguzi wa UWT kama walivyofanya katika uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) uliokuwa na makeke mengi na ule wa Jumuiya ya Wazazi, ambao umeshindwa kufanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo makundi ndani ya chama hicho tawala.

Uchaguzi huo umetanguliwa na mkutano wa Baraza Kuu la UWT lililoketi Jumanne, wiki hii.

Miongoni mwa mambo yaliyopitiwa katika mkutano huo wa Baraza Kuu ni pamoja na kupitia ripoti ya utendaji ya umoja huo katika kipindi kilichopita.
 
Hebu mwenye habari kamili za mshindi wa UWT atupatie ili tujue ukweli wa nani mshindi.
 
Mh. Gembe, umetoa hoja nzoto ambayo tunapaswa kuingia kwa undai zaidi. Ni kweli kabisa mwenendo wa familia ya mkulu unatia mashaka iwapo itajiingiza kwenye kila maamuzi, ushiriki wa riz kwenye ushindi wa beno na huu wa mama kwa Sofia uko wazi mno. Hii ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu, kwamba familia ya magogoni iwe na jukumu la uweka viongozi kila sehemu.

Sasa nashawishika kuamini uvumi ulioenea jijini Mbeya kwamba mkulu alikuwa na mkono kwenye ushindi wa mgombea wa ccm katika uchaguzi mdogo ujao kwenye jimbo la Mbeya Vijijini, Mch. Mwanjali.

Wakaazi wa mji mdogo wa Mbalizi wanaamini kabisa kwamba mgombea huyo ametangulizwa tu na bosi wake wa kanisa lao Mch. Mrcus Lena, ambaye inadaiwa yuko aribu na mkulu! Hiyo familia inatajwa kila sehemu za chaguzi, hii ni hatari.
 
Taarifa nilizopata sasa hivi toka kwa mtu aliyeko kwenye mkutano huo pale Dodoma zinasema Sofia ameshinda kwa asilimia chini ya sitini, matokeo rasmi bado kutangazwa nao ndo wanasubiri.
 
- At this time nina-confirm kwa 100% kwamba Sophia Simba ndiye mshindi wa huu uchaguzi wa jana, wa uwt, ingawa bado hazitangazwa rasmi.

- Sijapata details zote za yaliyojiri lakini dataz chache nilizonazo ni kwamba Sophia amesaidiwa sana na mawaziri wenzake wawili, yaani waziri wa Utumishi, waziri wa mali ya asili, pia kuna waziri mwingine wa tatu bado sijamthibitisha.

- Dau la Sophia kwa wajumbe wapiga kura lilikuwa shillingi laki moja kwa kila mpiga kura, mama Janet ametoa zaidi lakini hakuwafikia wapiga kura woten na hasa wasimamizi wa kuhesabu kura, maana technically amechezewa game kwenye kuhesabu. This is another win kwa kwa mafisadi kwa so far tuko nao 2-2.

Bado tunafuatilia dataz kwa karibu na kama kawa tukizipata tutazimwaga hapa uwanja wa damu JF.

Wazee wa sauti ya umeme!
 
kafuata nyayo za kikwete, kwani mkulu aliweza kushinda uchaguzi kwa gharama ya shs 133bn za epa, deep green nk, sasa tunashangaa nini? utawala huu umefikia mwisho wake, mwenyezi Mungu haweza kushuhudia kuwepo na madola batili kama haya milele, dola la kinafiki la kikwete na ccm linakaribia gharika kuu
 
Mkuu wa medani na wengineo, nawapongeza kwa taarifa nzito zisizo mashaka.

Natumia fursa hii kumpongeza mwanasheria bi sophia mnyambi simba kwa kuwa ndiye m/kiti wa tatu wa uwt-ccm.

Hongera mama, kaza mwendo ..................
 
Mkuu wa medani na wengineo, nawapongeza kwa taarifa nzito zisizo mashaka.

Natumia fursa hii kumpongeza mwanasheria bi sophia mnyambi simba kwa kuwa ndiye m/kiti wa tatu wa uwt-ccm.

Hongera mama, kaza mwendo ..................
 
Once you are the chairperson of UWT, you are automatically Mbunge. 2010 huna expense`yeyote ya kutafuta kura. Uko assured kuwa "employed " mpaka 2015.

Real? Did not know that!!! No wonder all these FUSS!!!!! So to speak $2mil is worthy it..teh teh thithithi
 
Wadau,

Hivi Sophia Simba atapata wapi muda wa kufanya kazi zote kama Mbunge, waziri na mwenyekiti wa UWT?

Wakati mamilioni ya watu hawana kazi, hawa wengine wanahodhi vyeo na kushindwa ku deliver.

Kwani Anna Abdalla wakati wa Mkapa alipata wapi muda wa kuwa mbunge, waziri wa afya na M/kiti UWT?. Only in TZ is possible wenzetu wenye wito wa huduma huamua kujiuzulu nafasi nyingine na kubakia na moja ili awe effective, ila kwa bongo nafasi hizi ni ulaji na si huduma hata hamsini mtu anazimudi si ni kuhudhuria vikao tu nani atashindwa?.
 
Last edited:
Kiongozi anayenunua uongozi kwa gharama yeyote ile huyu si kiongozi lazima ujiulize anataka nini au ana agenda gani katika harakati zake za kuwania uongozi?, Uongozi ni wito mtu anajitolea kuwatumikia watu na watu wanahaki kumpima na kumchagua kutokana na upeo wake kama mwombaji anatumia kutanguliza kitu kidogo kuwarubuni wapiga kura huyu hafai inabidi kumwogopa kama ukoma au kama ukimwi kabisa.
 
Back
Top Bottom