Waziri Sophia Simba amedanganya bunge kumlinda Salma Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Sophia Simba amedanganya bunge kumlinda Salma Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Apr 20, 2012.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kwenye mtandao wa gazeti la serikali la Habari Leo kuwa Waziri Sophia Simba amesema kuwa Salma Kikwete hakuitumia WAMA kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010. Nikatafuta Salma Kikwete+WAMA+Kampeni na nikakuta ushahidi kuwa Waziri huyu amedanganya bunge.

  Ushahidi mmojawapo ni huu:Mama Salma Kikwete afanya kampeni kwa mgongo wa WAMA.

  Asha
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  N a yeye ajiuzuru mapema!
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Asha Abdala bana!!
   
 4. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ha ha ha! Duh Kupenda Siasa tabu sana!
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  nani salma au simba?
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wote wameshazoea kulidanganya bunge. Unamkumbuma Waziri mkuu alivyolipuliwa na Lema wakanywea mpaka leo?
   
 7. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Wote ni galegale
   
 8. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145


  Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya WAMA ambaye pia ni mke wa Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Mama SALMA KIKWETE ameweka bayana ahadi hiyo wakati akizungumza na wanawake katika wilaya Kibaha na Bagamoyo Mkoani Pwani.


  Amesema taasisi hiyo imekwishatekeleza mambo mengi katika awamu ya Nne ambayo aliahidi katika kampeni za mwaka 2005 hasa kwa wanawake,watoto yatima,waishio katika mazingira magumu,watoto wakike na sekta ya afya.  Mama SALMA amebainisha kuwa aliahidi CCM ikichaguliwa taasisi ya WAMA itachukua watoto WATANO kila Mkoa kwa lengo la kuwasaidia katika suala zima la elimu na imetekeleza na kati ya watoto hao mmoja wao atafanya mtihani wa kidato cha Nne mwaka huu.  Mbali ya kusaidia watoto hao chini ya taasisi hiyo pia haikuwa nyuma kupeleka vifaa mbalimbali vya akina mama wajawazito katika zahanati na hospitali hapa nchini,kusaidia vikundi vya akina mama kuvipatia fedha za kuendesha vikundi vyao na kusomesha watoto yatima.  Aidha Mama SALMA amesema CCM imetekeleza mengi katika sekta ya afya,miundombinu,elimu,kilimo chini ya ilani yake,katika kipindi cha awamu ya NNe hivyo amewaomba wanawake na wananchi Kiujumla mkoani pwani kuchagua Rais,wabunge na madiwani kutoka CCM itakapofika Tr 31 Octoba ili kumalizia machache yaliyobaki.  Nae Mwenyekiti wa UWT wilayani Kibaha Mji ,Bibi NURU MSUMI amemshukuru Mama SALMA kwa kuipatia Saccos ya wanawake wilayani humo Tsh milioni Moja na Laki Tano.  Mama SALMA KIKWETE anaendelea na ziara yake yakuomba ridhaa kwa wananchi kuendelea kukipigia kura Chama cha Mapinduzi,ambapo ameshafanya ziara hiyo wilayani kibaha Mji , Kibaha vijijini , Bagamoyo, Chalinze na leo anaendelea kisarawe na Mkuranga kesho atakuwa Rufiji.

   
 9. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Wakati waziri Sophia Simba akilijibu suala Hilo kwa majibu mepesi toka ktk hoja nzito,Kama kawaida ya wabunge Wa ccm walimpigia makofi na kugonga meza kwa nguvu kweli.Wananchi wasipoichukua nchi Yao mapema basi tutarajie mambo haya kuendelea kutokea
   
 10. J

  John W. Mlacha Verified User

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  wezi wote hawa
   
 11. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,250
  Trophy Points: 280
  Tatizo mibunge ya CCM imekaa kudanganywa danganywa na inaridhika haraka ikiambiwa uongo. Wacha wadanganywe wazembe hawa.
   
 12. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  .....naomba mwongozoo wa SPIKA TAFADHALI!! mbunge akilidanganya bunge na wabunge kukubali kudanyika...KAMUMI ZINASEMAJE HAPO?
   
 13. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Waziri katika serikali ya CCM ana kinga ya kutokuchukuliwa hatu pale anapodanganya bunge.Ndiyo maana viongozi wa serikali wanapoiba wanaitwa wabadhirifu na wakikamatwa huambiwa warudishe wakati wezi wengine hasa wa kuku hufungwa jela. Hiyo tofauti hamwuijui wanajamvi?
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi wameanza kujidanganya wenyewe at an alarming rate. Uongo hauwezi kusimamisha salama mihili na uwepo wa Taifa letu.
   
 15. n

  nasikitikaa Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani Sophia Simba bado ni waziri?si tayari alishatoka au nimekosea jamani
  siku hizi hasikiki na zile mbwembwe zake za I DONT CARE WHO ARE YOU?
  IM THE KIBOKO YAOOOOOOOOOOOO!aa mambo yuleeeeeee!mhhhhh!
   
 16. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  Salma Kikwete anapiga kampeni kama nani na kwa pesa ipi?
  [​IMG]

  Nkwazi Mhango​
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  JUZI niliona habari kuwa mke wa rais Jakaya Kikwete aliyetambulishwa kama mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete, akimnadi mgombea wa ubunge CCM, jimbo la Mafia, Abdulkarim Shah.
  Swali la kwanza lililonijia ni: kama WAMA ni asasi isiyo ya kiserikali ya kutetea wanawake wote wa Tanzania wakiwemo na wa vyama vya upinzani, inakuwaje mwenyekiti wake amnadi mgombea wa CCM?
  Je, kweli WAMA iko kwa ajili ya maendeleo ya wanawake wote kama jina lake au kutumika kama chombo cha kukusanyia pesa kwa ajili ya familia ya Kikwete na chama chake? Je kwa kujiingiza kwenye siasa, bado WAMA inaaminika? Je WAMA si taasisi ya nyuma ya pazia ya ulaji ya CCM kwa mgongo wa ikulu?
  Nikiri. Nimekuwa na picha mbaya ya WAMA si kwa sababu nina ugomvi nayo bali hali halisi. Nikikumbuka yaliyotokea kwa EOTF ya Anna Mkapa iliyoishia kuwa kichaka cha ufisadi kwa kutumia ikulu, sina imani na amani na WAMA.
  Kuondoa utata basi WAMA iitwe WAMACCM yaani Wanawake na Maendeleo wa Chama Cha Mapinduzi. Hili likifanyika sitakuwa na ugomvi na WAMA ingawa kama mchezo wa kutumia mali za umma na serikali kufanya shughuli za kisiasa kama ilivyo utaendelea, vitanilazimisha kuwashukia tena. Huu ni wizi hata kama unafanywa na wakubwa. Wizi ni wizi na si mzuri.
  Niliwahi kuuliza ingawa sikujibiwa. Kwanini kila shughuli ya WAMA inaonekana kuwa ya kidikteta kwa maana ya kusimamiwa na mtu mmoja-Salma kiasi cha WAMA kuwa Salma na Salma kuwa WAMA?
  Kwa nini iote baada ya bwana mkubwa kuingia madarakani kama lengo si ulaji kwa kutumia mgongo wa ikulu kama EOTF?
  Hata ukiangalia mpangilio wa watendaji wake unagundua kuchanganya mambo kiasi cha kuumbuka au kuufichua ukweli ulioko nyuma ya pazia. Kwa mfano kwenye watendaji wa WAMA kuna mtu aitwaye Anande Munuo ambaye ametajwa kama secretary to the first lady siyo to the chairperson. Hii ni nini kama siyo kufanyiana usanii?
  Habari tajwa inaendelea kusema kuwa Salma alikuwa kwenye ziara ya siku moja kisiwani Mafia kuwahamasisha wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kuwachagua wagombea wa CCM! Je hapa kuna swali tena? Je huu si ushahidi wa kimazingira kuwa asasi hii ni hatari kwa demokrasia kwa sababu kuu mbili:
  Mosi kutumika kisiasa kwa manufaa ya Kikwete na CCM. Na pili kuanzisha katika wakati na mazingira yanayotia shaka ukiachia mbali shughuli zake kutia shaka vile vile. Mbona hatuoni taarifa ya ukaguzi wa hesabu za WAMA kila mwaka? Nani ataikagua iwapo hata mume wake amegoma kutaja mali zao na WAMA ikiwemo?
  Hapa hujagusia mapokezi mazito anayopewa kama mke wa mkubwa kila anapokwenda m ikoani hata nje ya nchi anapokusanya pesa kwa mgongo wa ikulu. Bado hapa hujadodosa misafara mirefu ya magari anayoandamana nayo. Kama nani chini ya katiba yetu viraka? Je huku si kutumia vibaya madaraka kwa mumewe? Leo utasoma habari za Salma akifanya kazi ya CCM kesho mwanae wa kufikia, Ridhiwan akimnadi baba yake kabla ya baba mwenyewe. Je hapa si kutengeneza ufalme wa familia ya Kikwete jamani?
  Najua Salma ni mwalimu. Wengi wangedhani, kama kweli angekuwa ana uchungu na watanzania, basi angewekeza kwenye elimu badala ya siasa za nyuma ya pazia. Asingepata muda wa kuwania nafasi chamani bali kutumia muda wake kama first lady kuhamasisha elimu iliyosahauliwa na utawala wa mumewe. Hata hayo maendeleo yasiyoonekana anayohamasishwa yanakwamishwa na serikali ya mumewe iliyokumbatia ufisadi na kujuana.
  Tusiseme bila ushahidi. Wako wapi kina Kagoda ambao wanazidi kutesa huku wanaowapinga wakiteseka? Wako wapi kina Richmond wanaotukoga kila uchao kuwa urafiki wao na Kikwete si wa barabarani na hauwezi kuvunjwa na vyombo vya habari? Leo fisadi ananyea ofisi mchana anatimuliwa lakini anaitwa mstaafu! Tangu lini mharifu aliyekiri kwa kujiwabisha akawa mstaafu? Au ni kwa vile wastaafu wa kweli kama vile waliokuwa wafanyakazi wa Jumuia ya Afrika Mashariki tumewadhulumu na kubadilisha maana ya mstaafu? Kama Salma na WAMA yake wanapigania maendeleo kweli, kwanini asimwambie mumewe kuwa maendeleo hayawezi kupatikana katikati ya ufisadi na ubabaishaji?
  Wakati Salma akiwatumia wanawake na ikulu kumpigia debe mumewe, mumewe naye anatumia magari ya umma kujipigia kampeni! Hivi nchi hii imerogwa na nani na itapona lini?
  Je, kwa tabia hii na ufichi huu Salma anajitofautisha vipi na ma-first ladies mafisadi kama Grace Mugabe bingwa wa kufuja pesa ya umma, mareheme Stella Obasanjo aliyewahi hata kutoa amri ya kufungia gazeti, Lucy Kibaki aliyewahi kuwachapa waandishi wa habari bila kusahau, Nana Kanadu Rawlings aliyewahi kutajwa na mumewe kuwa ni binadamu pekee ambaye angeweza kumdhibiti Jerry Rawlings rais wa zamani wa Ghana?
  Je, kitendo cha mke wa rais kutumia taasisi isiyo ya kiserikali kuwahadaa na kuwahonga kina mama hakitoshi kuwa ufisadi? Kwanini wapinzani wasichukue hoja hizi na kuwabwagia watanzania wajue nchi yao inavyoliwa kwa mgongo wa rais? Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka yanayokinzana na utawala bora na wa sheria anaojisifia kutekeleza rais Kikwete. Wapinzani wakiuonyesha umma madudu yake, licha ya kufichua ubovu wake, watakomesha tambo na uongo wa Kikwete ambaye kwa miaka mitano hajafanya lolote la maana zaidi ya kulinda ufisadi na matumizi mabaya ya raslimali na fedha za umma.
  Pia kwa kufichua hujuma ya WAMA angalau wananchi watajua siri ya kampuni hii kuundwa pindipo rais Kikwete alipoingia madarakani na si kabla. Kwa kuiandama hata kuifutilia mbali WAMA tutaepusha wake za marais wajao kuendelea kutuibia kwa kisingizio cha NGO na visingizio vingine ambavyo kimsingi vinaonyesha hizi NGO zinaanzishwa kwa minajili ya kujitajirisha na kuzitumia kupitisha rushwa kwa wapiga kura kama inavyofanya WAMA.
  Ningeshauri WAMA iitwe MAWA au Maulaji ya Wake (za Wakubwa). Ukitaka kujua ninachomaanisha nenda uangalie wadhamini wa WAMA. Ni mke wa makamu wa rais na mgombea wa urais wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Zakhia Meghji waziri wa fedha wa zamani, Balozi Mwanaidi Majaar, Sophia Simba waziri wa Kikwete, Blandina Nyoni katibu wizara Regina Lowassa mke wa waziri mkuu aliyetimuliwa na wengine wakubwa tu. Hapa WAMA haijawa mradi wa ulaji wa wake za vigogo na vigogo? Je hawa hawajateuliwa kutokana na kujuana na bi mkubwa aliyempa ushauri mumewe awateue mashoga na washirika wake katika kusaka ngawira?
  Hakika WAMA imeficha mambo mengi ambayo umma unapaswa kuyajua hata kuhoji.
  Wapinzani na watanzania ibomoeni WAMA. Kwani inatumika kutuhujumu kwa mgongo wa ikulu na ni alama ya matumizi mabaya ya madaraka, ulafi, ufisadi na udhalilishaji wa taasisi ya urais.
  Je, Salma anapiga kampeni kama nani na kwa pesa ipi?
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Salma Kikwete anapiga kampeni kama nani na kwa pesa ipi?
   
 17. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wake wenza
   
Loading...