Waziri Sofia Simba atimuliwa bungeni kwa kuvaa sare za CCM

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
WAZIRI wa Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, jana alizuiwa na walinzi wa Bunge kuingia ukumbini kutokana na kuvalia mavazi yanayokiuka kanuni zinazoliendesha Bunge.
Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), alifika bungeni hapo jana akiwa amevalia sketi na shati la mikono mirefu lenye rangi ya kijani na alama za CCM.

Tanzania Daima ilimshuhudia Waziri Simba alizuiliwa kuingia bungeni kutokana na vazi lake hilo lenye alama za chama.

Katika kuonesha kuwa Waziri Simba alivalia sare hiyo kwa makusudi, wakati akiingia alijifunika kwa mtandio ili shati hilo lisionekane, lakini walinzi walimshtukia kupitia upande wa mgongoni ambako mtandio huo haukufunika vizuri.
Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Waziri Simba alijibu kwa kifupi kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (sms) akisema; “achana na mimi”.
Hatua hiyo inakuja wiki chache tangu Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kudai kuwa aliandikiwa ujumbe na baadhi ya wabunge wakihoji kama mavazi ya kombati yanayovaliwa na wabunge wa CHADEMA hayakiuki kanuni.
Ndugai katika kauli yake hiyo alisema ziko kombati za rangi mbili, nyeusi na kaki zinazovaliwa bungeni, kwamba na wengine wanataka kuja na kombati za rangi ya kijani.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika walipinga kauli ya Ndugai wakidai anafanya porojo za kisiasa bungeni.

Walisema kuwa kombati ni mavazi yanayoruhusiwa na kanuni za Bunge na kufafanua kuwa kwa mujibu wa kanuni, vazi la wanaume linaloruhusiwa ni pamoja na suti za safari zinazovaliwa na CHADEMA.

Kwa mujibu wa kanuni ya 149 (3) (a) kwa wanawake na (b) kwa wanaume kuna aina za mavazi yanayopaswa kuvaliwa bungeni.

Kanuni hiyo inasomeka kuwa kutakuwa na vazi rasmi kwa wabunge (a) kwa wanawake;- (i) Vazi lolote la heshima yaani ambalo si la kubana mwili, lisiloonesha maungo ambayo kwa mila na desturi za Kitanzania hayapaswi kuoneshwa na ni refu kuvuka magoti, (ii) gauni la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi ya rangi yoyote (iii) kilemba cha kadiri au mtandio (iv) suti ya kike; au (v) vazi linalovaliwa wakati wa eda.
b) Kwa wabunge wanaume;- (i) suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baraghashia;
(ii) Vazi la kimwambao yaani kanzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na makubazi au viatu; (iii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi kadiri isiyomeremeta; (iv) koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote ya heshima; au (v) tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.
 
Itapendeza kama kombati (CHADEMA), kijani ( CCM) na rangi za vyama vingine zikapigwa marufuku ili kulifanya bunge la kitaifa zaidi kuliko kivyama.

Ingawa kombati ni vazi la kawaida lakini linapotumiwa na chama fulani na kuvaliwa na wafuasi wake hakuondoi dhana kwamba ni alama ya chama chao.

TANZANIA MBELE VYAMA BAADAYE.
 
huyu yupo kambi gani kwenye yale mambo yetu ya 2015? maana mama ni jembe kiboko ya Mh Anna Kilango..
 
Itapendeza kama kombati ( chadema), kijani ( CCM) na rangi za vyama vingine zikapigwa marufuku ili kulifanya bunge la kitaifa zaidi kuliko kivyama.

Ingawa kombati ni vazi la kawaida lakini linapotumiwa na chama fulani na kuvaliwa na wafuasi wake hakuondoi dhana kwamba ni alama ya chama chao.

TANZANIA MBELE VYAMA BAADAYE.

Sasa unatapatapa...maana viti maalumu vinaelekea kufutwa.
 
Hivi rangi za bendera ya chadema hazifahamiki hadi wahusishe na kombati.?

Aliewazuia ccm kuvaa kombati nani./
 
"Achana na mimi"....huyu Mama bana,ni wale wamama wa mjini sana
 
WAZIRI wa Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, jana alizuiwa na walinzi wa Bunge kuingia ukumbini kutokana na kuvalia mavazi yanayokiuka kanuni zinazoliendesha Bunge.
Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), alifika bungeni hapo jana akiwa amevalia sketi na shati la mikono mirefu lenye rangi ya kijani na alama za CCM.

Tanzania Daima ilimshuhudia Waziri Simba alizuiliwa kuingia bungeni kutokana na vazi lake hilo lenye alama za chama.

Katika kuonesha kuwa Waziri Simba alivalia sare hiyo kwa makusudi, wakati akiingia alijifunika kwa mtandio ili shati hilo lisionekane, lakini walinzi walimshtukia kupitia upande wa mgongoni ambako mtandio huo haukufunika vizuri.
Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Waziri Simba alijibu kwa kifupi kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (sms) akisema; “achana na mimi”.
Hatua hiyo inakuja wiki chache tangu Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kudai kuwa aliandikiwa ujumbe na baadhi ya wabunge wakihoji kama mavazi ya kombati yanayovaliwa na wabunge wa CHADEMA hayakiuki kanuni.
Ndugai katika kauli yake hiyo alisema ziko kombati za rangi mbili, nyeusi na kaki zinazovaliwa bungeni, kwamba na wengine wanataka kuja na kombati za rangi ya kijani.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika walipinga kauli ya Ndugai wakidai anafanya porojo za kisiasa bungeni.

Walisema kuwa kombati ni mavazi yanayoruhusiwa na kanuni za Bunge na kufafanua kuwa kwa mujibu wa kanuni, vazi la wanaume linaloruhusiwa ni pamoja na suti za safari zinazovaliwa na CHADEMA.

Kwa mujibu wa kanuni ya 149 (3) (a) kwa wanawake na (b) kwa wanaume kuna aina za mavazi yanayopaswa kuvaliwa bungeni.

Kanuni hiyo inasomeka kuwa kutakuwa na vazi rasmi kwa wabunge (a) kwa wanawake;- (i) Vazi lolote la heshima yaani ambalo si la kubana mwili, lisiloonesha maungo ambayo kwa mila na desturi za Kitanzania hayapaswi kuoneshwa na ni refu kuvuka magoti, (ii) gauni la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi ya rangi yoyote (iii) kilemba cha kadiri au mtandio (iv) suti ya kike; au (v) vazi linalovaliwa wakati wa eda.
b) Kwa wabunge wanaume;- (i) suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baraghashia;
(ii) Vazi la kimwambao yaani kanzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na makubazi au viatu; (iii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi kadiri isiyomeremeta; (iv) koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote ya heshima; au (v) tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.

Nimependa ufafanuzi
 
Hivi vyama vitatuongezea umaskini tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Upuuzi mtupu. Watashindana lakini hawatashinda, kombati za Chadema hazina rangi ya alama za chama na ni za rangi tofauti tofauti. Je, mtu akivaa kadeti suruari na shati atahesabika amevaa kombati za Chadema? Safari suit zinavaliwa na mtu yeyote, na isitoshe kombati ni za kipekee.
 
Eti wabunge wa aina hii (Viti maalumu) ndiyo Judge Warioba anawapigia chapuo kwenye rasimu ya katiba mpya wawe 1/2 bin 1/2 na wanaume!Judger Warioba hii katiba mpya ni zaidi ya akina Sophia Simba! TUHURUMIE SISI WATANZANIA tutakaoituimia hii katiba kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
 
Itapendeza kama kombati ( chadema), kijani ( CCM) na rangi za vyama vingine zikapigwa marufuku ili kulifanya bunge la kitaifa zaidi kuliko kivyama.

Ingawa kombati ni vazi la kawaida lakini linapotumiwa na chama fulani na kuvaliwa na wafuasi wake hakuondoi dhana kwamba ni alama ya chama chao.

TANZANIA MBELE VYAMA BAADAYE.

Sawa........................ lakini kumbuka kwamba waziri simba hakuzuiliwa kwa sababu ya rangi ya nguo zake zinazoashiria uccm, bali alizuiliwa kwakuwa alikuwa amevalia nguo zenye nembo ya chama yaani Jembe na Nyundo, halafu imeandikwa ccm.
Hata kama chadema nao wameingia na kombat zimeandikwa M4C halafu wakakoleza na neno chadema nao wazuiwe!
Kiti cha spika lazima kipewe heshima yake japo inapwaya kiukweli!
 
Back
Top Bottom