Waziri Sofia Simba atimuliwa bungeni kwa kuvaa sare za CCM

Eee Mungu wanguWee; Leo mwaka wa 2013 Bunge letu linazungumziya "mavazi" !! Looh sijui nchi itajengwa na mavazi au UBONGO wa viongozi ? hayo ni matusi na kejeli kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. aiibu tupu!!
 
Itapendeza kama kombati ( chadema), kijani ( CCM) na rangi za vyama vingine zikapigwa marufuku ili kulifanya bunge la kitaifa zaidi kuliko kivyama.

Ingawa kombati ni vazi la kawaida lakini linapotumiwa na chama fulani na kuvaliwa na wafuasi wake hakuondoi dhana kwamba ni alama ya chama chao.

TANZANIA MBELE VYAMA BAADAYE.

Hivi zile za CHADEMA ni Kombati au Kadeti?
 
Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Alidhani anaingia kwenye Onyesho la Isha Mashauzi EQUATOR GRILL !
 
Hivi Tanzania Daima hawana habari? si walifanye gazeti lao liwe jarida la mambo ya kimahaba ili lilete tija! maana huu upuuzi walio uandika una maana gani?
 
Huyu Sophia Simba naona mabalaa yanazidi kumkumba juzi kidogo watwangane na mbunge mwenzake wa CCM Anne kilango Malecela.
 
si nasikia ana makid kibao kila mtu na babiye??makada wanajibondea tu na kuibuka na kid...mwenye detailz zaidi atumwagie tafadhali.

shughuli ipo akianza kupata misiba, mara leo namsindikiza mwanangu wa pili kafiwa na babu yake mtwara, mara juzi sikuwepo mwanangu wa nne alifiwa na baba yake mdogo tabora, mara kesho naenda shinyanga mtoto wangu wa kwanza kafiwa na shangazi yake. Kila wakati occupied na safari za kuzika na kuhani
 
Hivi vyama vitatuongezea umaskini tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu wakati wa chama kimoja tulikuwa matajiri? Mbona tulikuwa tunapanga foleni kununua unga, sukari, sabuni, chumvi, nk?
 
Wanaiga makamanda wa CHADEMA wakati sio saizi yao,ahamie CHADEMA kama anawaonea wivu makamanda na mavazi yao.
Kuelekea 2015 tutashuhudia mengi
 
• NI KUTOKANA NA MAVAZI ALIYOVAA

na Edson Kamukara, Dodoma

WAZIRI wa Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, jana alizuiwa na walinzi wa Bunge kuingia ukumbini kutokana na kuvalia mavazi yanayokiuka kanuni zinazoliendesha Bunge.

Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), alifika bungeni hapo jana akiwa amevalia sketi na shati la mikono mirefu lenye rangi ya kijani na alama za CCM.

Tanzania Daima ilimshuhudia Waziri Simba alizuiliwa kuingia bungeni kutokana na vazi lake hilo lenye alama za chama.

Katika kuonesha kuwa Waziri Simba alivalia sare hiyo kwa makusudi, wakati akiingia alijifunika kwa mtandio ili shati hilo lisionekane, lakini walinzi walimshtukia kupitia upande wa mgongoni ambako mtandio huo haukufunika vizuri.

Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Waziri Simba alijibu kwa kifupi kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (sms) akisema; “achana na mimi”.

Hatua hiyo inakuja wiki chache tangu Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kudai kuwa aliandikiwa ujumbe na baadhi ya wabunge wakihoji kama mavazi ya kombati yanayovaliwa na wabunge wa CHADEMA hayakiuki kanuni.

Ndugai katika kauli yake hiyo alisema ziko kombati za rangi mbili, nyeusi na kaki zinazovaliwa bungeni, kwamba na wengine wanataka kuja na kombati za rangi ya kijani.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika walipinga kauli ya Ndugai wakidai anafanya porojo za kisiasa bungeni.

Walisema kuwa kombati ni mavazi yanayoruhusiwa na kanuni za Bunge na kufafanua kuwa kwa mujibu wa kanuni, vazi la wanaume linaloruhusiwa ni pamoja na suti za safari zinazovaliwa na CHADEMA.

Kwa mujibu wa kanuni ya 149 (3) (a) kwa wanawake na (b) kwa wanaume kuna aina za mavazi yanayopaswa kuvaliwa bungeni.

Kanuni hiyo inasomeka kuwa kutakuwa na vazi rasmi kwa wabunge (a) kwa wanawake;- (i) Vazi lolote la heshima yaani ambalo si la kubana mwili, lisiloonesha maungo ambayo kwa mila na desturi za Kitanzania hayapaswi kuoneshwa na ni refu kuvuka magoti, (ii) gauni la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi ya rangi yoyote (iii) kilemba cha kadiri au mtandio (iv) suti ya kike; au (v) vazi linalovaliwa wakati wa eda.

b) Kwa wabunge wanaume;-

(i) suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baraghashia;

(ii) Vazi la kimwambao yaani kanzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na makubazi au viatu;

(iii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi kadiri isiyomeremeta;

(iv) koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote ya heshima; au

(v) tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.

Utoro bungeni

Katika kile kinachoweza kutafsiriwa wabunge kutotilia maanani umuhimu wa kuhudhuria vikao, mijadala mbalimbali ya hotuba za bajeti imekuwa ikiendelea huku idadi ndogo ikionekana ndani ya ukumbi.

Uchunguzi wa gazeti hili kwa wiki kadhaa, umebaini kuwa wabunge wengi wanahudhuria kipindi cha maswali na majibu asubuhi na baada ya hapo wanatoka nje kuendelea na shughuli zao binafsi au vyama vyao.

Wengine wanakaa katika mgahawa wa Bunge na kufuatilia mjadala unaoendelea kupitia televisheni, halafu jioni wanaingia dakika za mwisho wakati Bunge likikaribia kukaa kama kamati ili kupitia kifungu kwa kifungu.

Baadhi ya wananchi mkoani hapa wanaofuatilia Bunge kupitia televisheni, wamekuwa wakihoji umakini wa wabunge katika kupitia mafungu na kisha kuipitisha bajeti wakati hawakai ukumbini kuwasikiliza mawaziri wanaposoma bajeti zao ama kujibu hoja.

Jumamosi iliyopita wakati wa kujadili na kuzipitisha bajeti za wizara mbili; ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi pamoja na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kulikuwa na idadi ndogo.

Wakati kikao kinaanza saa 3.00 asubuhi, ukumbini walikuwemo wabunge 21, mawaziri na Naibu Spika. Na hadi Naibu Waziri wa Mifugo, Benedict ole Nang’oro anahitimisha kujibu hoja za wabunge saa 3.20 walikumo wabunge wasiozidi 30.

Ilipokaribia saa 5.00 muda wa Bunge kukaa kama kamati ili kuipitisha bajeti hiyo, idadi ya wabunge iliongezeka ghafla na kutimiza akidi kisha bajeti ikapitisha bila wengi wao kujua hoja zao zilijibiwaje.

Utoro huo uliendelea jana wakati mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ukiendelea kwani kuanzia muda wa saa tano hivi hadi kufikia saa 7.00 wakati wa mapumziko ya mchana ukimbini walikuwamo mawaziri watano, manaibu wanne na wabunge wasiozidi 60 kati ya 357.

Akizungumzia utoro huo, Naibu Spika, Ndugai alisema kanuni haziwapi madaraka ya kuwadhibiti, isipokuwa akikosa kuwepo mikutano mitatu mfululizo yaani robo tatu ya mwaka mzima.

Bado kidogo watkuja na skini taiti, kama ile katuni ya Kenya.
 
shughuli ipo akianza kupata misiba, mara leo namsindikiza mwanangu wa pili kafiwa na babu yake mtwara, mara juzi sikuwepo mwanangu wa nne alifiwa na baba yake mdogo tabora, mara kesho naenda shinyanga mtoto wangu wa kwanza kafiwa na shangazi yake. Kila wakati occupied na safari za kuzika na kuhani
Hahahaaaa balaa hili kisa ndumba na ----- wa masisiem wanamfanya punching bag..
 
Back
Top Bottom