Waziri Sitta, Zitto wapimana ubavu Kirumba jijini Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Sitta, Zitto wapimana ubavu Kirumba jijini Mwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rene, Mar 16, 2012.

 1. R

  Rene Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri Sitta, Zitto wapimana ubavu Kirumba jijini Mwanza

  .Ni ‘vita’ ya udiwani, CCM yapambana kurejesha heshima

  .Chadema yaomba ridhaa kuendelea kula mbivu za kisiasa

  Na Deus Bugaywa, Mwanza

  UPINZANI wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza umeugeuza uchaguzi mdogo wa kata ya Kirumba kuwa ni zaidi ya uchaguzi wa kumpata diwani.

  Kwa sasa, uchaguzi huo unatafsiriwa kama kiashirio cha ama Chadema kuendelea kujiimarisha kisiasa Mwanza au CCM kurejesha heshima katika moja ya zilizokuwa ngome zake kuu nchini.

  Baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, CCM ambacho kilikuwa kikijivunia Mwanza kama ngome yake muhimu katika kanda ya Ziwa, kilijikuta kikipoteza majimbo yanayounda Halmashauri ya Jiji la Mwanza ya Nyamagana na Ilemela na Jimbo la Ukerewe ambayo yote yalitwaliwa na Chadema. Kama hiyo haitoshi, Halmashauri ya Jiji la Mwanza nayo ikachukuliwa na chama hicho cha upinzani.

  Kupoteza majimbo hayo kuliwafanya wanachama wa CCM katika Jiji la Mwanza kunyong’onyea, hali hiyo ilirekebishwa kidogo na maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika kitaifa mkoani hapa katika Uwanja wa CCM Kirumba, ambapo kwa mara ya kwanza tangu Uchaguzi Mkuu, wanaCCM walipata fursa ya kujidhihirisha hadharani kwamba wapo.

  Ni kutokana na mazingira hayo CCM kinautazama uchaguzi wa kata hiyo kama mwanzo wa kuzaliwa upya katika Jiji la Mwanza ambako wamekuwa ni kama wapinzani.

  Kama kitaibuka mshindi katika kinyang’anyiro hiki, ushindi wa mgombea wa chama hicho, Mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Jackson Robert maarufu kama ‘Jack Masamaki’ utakipatia chama hicho nguvu mpya kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao 2015.

  Lakini kwa upande wa Chadema, uchaguzi huu pia ni kipimo cha namna wanavyoaminika na wananchi na hivyo wamejipanga kutetea kiti hicho kilichoachwa wazi na aliyekuwa diwani wa kata hiyo kupitia chama hicho, marehemu Novatus Manoko, aliyefariki dunia, Agosti mwaka jana. Kwa sasa Chadema kinatetea kiti hicho kupitia mgombea, Dani Kahungu.

  Kampeni za Chadema zilizozinduliwa mwishoni mwa wiki jana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto, zilianzia katika makaburi ya Kitangiri ili kutoa heshima kwa marehemu diwani wao na kumwombea mapumziko mema peponi.

  Vyama na mtaji wa vigogo wao
  Kila chama kilihakikisha kinatumia vigogo wazito wa chama husika ili kushawishi wapiga kura wa kata hiyo. Kwa upande wa CCM, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alizindua kampeni za chama hicho katika viwanja vya Magomeni akiwataka wana Kirumba wachague diwani wa kiwango anayetokana na chama chake.

  “Kama mnavyonifahamu, nilipokuwa Spika wa Bunge nilisimamia viwango, na maadam mimi niko hapa, huu ni mkutano wa viwango, mchangueni kijana Jack awatumikie, mimi nimemlea toka anasoma shule, atakuja kuwa mmoja wa viongozi mashuhuri wa Mwanza hapo baadaye, ana sifa zote zilizomo kwenye katiba yetu” alisema Sitta akimnadi mgombea huyo.

  Akizungumzia changamoto za kata hiyo, Sitta alisema barabara ni moja ya changamoto kubwa akawaahidi kuwa kama wakimchagua mgombea wa CCM atasimamia baadhi ya madiwani wa Jiji la Mwanza waende Mexico wakaone jinsi barabara za milimani zinavyotengenezwa kwa njia nyepesi ili waje watumie ujuzi huo hapa.

  Alisisitiza kuwa CCM imedhamiria kwa dhati kurejesha heshima yake katika Jiji la Mwanza na kwamba wamejipanga kikamilifu kutekeleza ahadi zao kwa vitendo na si maneno matamu tu.

  “Ndugu zangu hatuwezi kukomboa kata hizi kwa maneno matamu tu, tumejipanga kushughulika kero zenu, tatizo la maji Ibanda linashughulikiwa, mimi nitakuwa balozi wenu, mkishakuwa na balozi wa kuwasimamia king’ang’anizi kama mimi, mhesabu nusu ya tatizo limekamilika, kesho nikirudi Dar, naanza kazi hiyo,” alisema katika kampeni zilizozinduliwa Jumamosi wiki iliyopita.

  Katika kampeni za Chadema zilizozinduliwa Jumapili iliyopita, Zitto alianza kwa kuwapa pole wakazi wa kata hiyo kwa kuondokewa na diwani wao na kuwaeleza kuwa haiwezekani kukatia rufaa uamuzi wa Mungu, lakini uchaguzi huo ni fursa ya kuwaambia Watanzania kuwa Mwanza haiwezi kurudi kuwa chini ya CCM.

  Zitto aliwaambia wakazi wa kata hiyo kuwa umuhimu wa uchaguzi huu ni zaidi ya mipaka ya kata hiyo, hiyo ni nafasi ya kuwaeleza watawala namna ambavyo hawaridhishwi na jinsi mambo yanavyoendeshwa.

  “Gharama za maisha zinapanda kila siku, maisha magumu, mfumuko wa bei karibu asilimia 20, uchumi hauzalishi ajira, hatuoni hatua muafaka za kisheria zinazochukuliwa kwa mafisadi, yote haya yako nchi nzima, kumchagua diwani wa CCM ni kuonyesha kuwa mnakubaliana na yote haya,” alisema.

  Aliwataka wakazi wa kata hiyo kumchagua diwani kutoka Chadema, Dani Kahungu, kwa kuwa pamoja na kwamba ndiye mtu sahihi katika kukabili changamoto za kata hiyo, lakini pia watakuwa wanapeleka salamu kwa watawala kwamba wamechoka na ugumu wa maisha na ufisadi.

  “Angalieni hata uchache wetu bungeni, lakini tuna sauti kubwa inayotetea wanyonge wote nchi hii, wao kazi yao kuzomea tu, mkiwapa diwani mtawapa zawadi ya kuendelea kutuzomea, lakini mkitupa diwani sisi mtatupa moyo wa kuendelea kupambana, hata kama wakizomea tutajua mko wananchi mnatuunga mkono” alisisitiza.

  Aliwakumbusha kuwa chama hicho kimejipanga kutawala nchi hii kutokea Mwanza, kwa hiyo wananchi wa kata ya Kirumba wasiwaangushe wana Mwanza wenzao, kwa kuwa bila Mwanza itakuwa vigumu kwao kushinda Uchaguzi Mkuu 2015.

  Mikakati ya wagombea

  Mgombea wa CCM, Masamaki anasema moja ya kero kubwa kwa wapiga kura wake ni maji katika maeneo ya Ibanda ambapo anasema atahakikisha ‘tanki’ la maji linafanyiwa marekebisho ili kuwapatia wananchi maji ya uhakika.

  “Tatizo la maji Ibanda nitalipa kipaumbele kikubwa kwa kufanya marekebisho ya tanki lililopo na kuhakikisha kuwa wananchi wa eneo hilo wanaishi kama wakazi wa Jiji, ni lazima kuondoa kero hiyo ya maji,” aliahidi.

  Kwa upande wa umeme ana mpango wa kuhakikisha maeneo ambayo hayana umeme katika kata yake yanafikiwa haraka inavyowezekana na hata kero ya barabara kwa kusaidiana na akina Mzee Sitta.

  “Ninaomba kitu kimoja kwenu, wekeni imani kwangu, mimi ni mzaliwa wa hapa, nazijua taabu na matatizo yote ya Kirumba juhudi zangu nikichanganya na busara na uzoefu wa wazee hawa (Samuel Sitta) ngoma inogile,” alisema.

  Kwa upande wa mgombea wa Chadema, Kahungu, anasema anajivunia kufanya kazi na marehemu diwani aliyekuwepo kama katibu wake, kwa kuwa alikuwa ndiye mratibu na msimamizi wa mipango yote ya maendeleo ya kata hiyo.

  “Marehemu amekuwa diwani kwa miezi minane tu, lakini katika muda huo yako mambo mengi ambayo aliyawekea misingi imara ya utekelezaji, kwa hiyo nikipewa heshima hii nitaendeleza pale alipoishia kwa kuwa ninajua kila kitu tulivyokuwa tunapanga,” alisema.

  Anasema kuwa katika kipindi cha miezi minane ya udiwani wa mtangulizi wake, amefanya mambo ambayo wengine yamewashinda katika kipindi cha miaka 48, akitoa mfano kuwa akiwa mratibu wa diwani ndani ya miezi 6 walipeleka maji eneo la Kigoto na kufanya bei ya ndoo ya maji kuwa shilingi 15 badala ya shilingi 100.

  “Katika kipindi hicho hicho barabara ya Kigoto ikaingizwa kwenye mipango, tarehe 29 Agosti, 2011, ikaanza kutengenezwa, bahati mbaya siku iliyofuata tarehe 30, Agosti diwani akafariki, mradi ukasimama, na kulikuwa na barabara zingine nne, haya yote nitayafuatilia shughuli iendelee,” alijinasibu.

  Aliahidi kuhamasisha madiwani wenzake wahakikishe sheria ndogo namba 136 ya Halmashauri ya Jiji ambayo inafanya Mwalo wa Kirumba kutozwa ushuru mara mbili, tofauti na mialo mingine sita ya Jiji la Mwanza, inafutwa na ataanzisha mfuko wa elimu wa kata hiyo ili kusadia elimu kwa watoto wa wazazi wasiojiweza

  Viongozi wa chama watambiana

  Wakati Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Wilson Mshumbushi, anasema CCM hawawatishi kwa kuwa wananchi wa Mwanza wanawaamini na kwamba walishaamua kuukataa ufisadi kwa hiyo hata wamlete nani hawawezi kuambuua kitu, Katibu wa CCM mkoani hapa, Joyce Masunga ana matumaini makubwa ya kushinda kata hiyo.

  “Tunafanya kampeni za hoja, Mwanza walishaamua siku nyingi kutodanganyika, wenzetu CCM wamechoka hawawezi kusimamia mambo ya msingi ya wananchi sisi hilo ndio jukumu la kila kiongozi wetu katika ngazi zote kutetea maslahi ya wananchi, CCM wasahau kushinda chochote Mwanza,” alijinasibu Mshumbushi.

  Kwa upande wake, Masunga anasema ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika uchaguzi huu na kwa kwamba huu ni uchaguzi muhimu sana kwao.

  “Tukishinda utaturejeshea matumaini na utakuwa ni ushindi siyo wa wana Kirumba tu huu utakuwa ni ushindi kwa wanaCCM wote, ndiyo maana kwetu huu ni uchaguzi muhimu sana kushinda, watu wameshaona tofauti tunaamini wataamua kwa busara na hilo litatupa ushindi” alisema.

  Viashiria vya kukosekana amani

  Katika hali ambayo inaashiria kampeni hizi zinaweza kutibua amani, Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Shahibu Akwilombe, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za chama chake aliwataka vijana wa chama hicho kutolitegemea jeshi la polisi badala yake wajilinde wenyewe.

  “Tunawaambia watakaotuletea fujo, tutajilinda kwa gharama zozote, hatutaenda polisi wala mahakamani tutawashughulikia wenyewe,” alisema.

  Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Buchosa, Dk. Charles Tizeba, ambaye naye alipopewa nafasi ya kutoa salamu kwa wananchi alisema; “Kama alivyosema katibu hapo awali, kwa habari ya fujo, hatutaenda kwa OCS tutashughulika nayo wenyewe.”

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema Mkoa wa Mwanza, Richard Sabini, aliwahadharisha vijana wa CCM na ushauri waliopewa na viongozi wao kuwa, wasithubutu kuleta vurugu katika kampeni hizo.

  “Vijana wetu watatii sheria, naomba nitoe onyo kwa Green Guard wakae mbali na Bavicha muziki wa Chadema mnaujua siyo wa pole pole, na ninataka nitoe onyo kwa polisi kukiwa na dalili za upendeleo tutajisimamia,” alisema.

  Akizungumzia hilo, Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, alisema; “Ninawashukuru polisi kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakinipa, ninaheshimu kazi yao, nawasihi tu wasije wakatumika kisiasa, hii ngoma mtuachie wenyewe, ni kama Zambia na Ivory Coast, kaeni kati mwanzo mwisho”

  Uchaguzi huo mdogo umepangwa kufanyika Aprili mosi, mwaka huu, kama ilivyo kwa chaguzi nyingine ndogo za udiwani na hata ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.
   
 2. commited

  commited JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  mtu mwenye akili timamu, elimu ya kueleweka na upana wa mawazo.. Hawezi tena kuishabikia ccm, hiki chama kilishakufa siku nyingi.. Ni chama cha wezi tu ambao kwao furaha yao ni kuona tanzania inazidi kuwa maskini.... R.i p ccm, wana mwanza msifanye makosa hao wote six na wassira ni wezi wakubwa na wazandiki wasio faa katika taifa hili. Miaka 50 wameua viwanda vyote, wameuza madini yetu kama vocha. Tupa kuleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee wezi hao. Razima tuwanyonge tu siku moja
   
 3. J

  Juma Hamis Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh.Sitta lazima aendelee kudhilisha uaminifu wake kwa Watanzania kwani ni mwanasiasa anayaaminika na makundi yote nchini ,yeye anakazi ya kulisafisha taifa na chama tawala kwa ajiri ya uongozi wenye tija kwa taifa.
   
 4. V

  Vonix JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Sitta si samaki ashindwe kuzungumza kwa kuzuiwa na maji,anajua madudu mengi kwenye serikali inayoongozwa na chama chake hawataki kusema wala kukihama chama mfu cha majambazi.ni kweli maiti tu ndiye atakichagua chama hiki.
   
 5. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  na pia wamemuua baba wa taifa
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,108
  Trophy Points: 280  ..CCM sasa kimekuwa chama cha matapeli tu.

  ..Sitta anatoa ahadi kushughulikia matatizo ya Mwanza, wakati ya Urambo yamemshinda.

  ..hizi kampeni zao na uwongo wanaowajaza wananchi mpaka inatia huruma.

  ..nawahurumia sana wananchi wanaodanganyika na kuipigia kura CCM
   
 7. mwitaz

  mwitaz JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nipo hapa Mwanza, na jinsi nijuavyo hili jiji; nina uhakika asilimia 100% kuwa Chadema itashinda katika huu uchaguzi
   
 8. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Naye 'fisadi' tu, kaangalie jumba lile analojenga Dar kama si wizi kapata wapi pesa yote hiyo miaka 10 tu baada ya kifo cha baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Watanzania hatudanyiki tena.
   
Loading...