Waziri Sitta apingana na Waziri wa Sitta: Aasa serikali kujibu kwa hoja siyo dola! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Sitta apingana na Waziri wa Sitta: Aasa serikali kujibu kwa hoja siyo dola!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Mar 9, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ameishauri Serikali kutotumia vyombo vya dola kuzima moto wa vyama vya upinzani kutokana na kauli zao kuhusiana na utendaji wa Serikali.

  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wiki iliyopita kilihitimisha ziara yake ya maandamano na mikutano ya hadhara katika mikoa na wilaya za Kanda ya Ziwa kikiishinikiza Serikali kutoilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Sh. bilioni 94.
  Mbali na hilo, pia Chadema kiliendesha maandamano hayo kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kushusha bei ya umeme, kupinga kupanda kwa gharama za maisha na kupinga uchaguzi wa Meya wa Arusha, ambao unadaiwa kujaa mizengwe.

  Baada ya ziara hiyo, Serikali ilikishutumu chama hicho kuwa maandamano yake ni ya kuwachochea wananchi waichukie na kukitishia kuwa itafika mahali serikali itakosa uvumilivu.

  Kauli hizo zilitolewa kwa nyakati tofauti na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita kwa taifa, ambaye alisema kauli za viongozi wa Chadema ni hatari kwa amani ya nchi na kwamba zinalenga kuifanya nchi isitawalike.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, alidai kauli za uchochezi katika maandamano ya Chadema yatailazimisha serikali kukosa uvumilivu.

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alirudia kauli ya Wasira akiwa ziarani mkoani Kagera kuwa itafika mahali serikali itakosa uvumilivu.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Mwanza, Sitta aliitaka Serikali kuwa nyepesi kwa kujirekebisha na kuwachukulia hatua viongozi wake ambao ni kero kwa wananchi.

  Alisema viongozi hao ni wale wanaojinufaisha wenyewe pamoja na familia zao badala ya kuwatumikia wananchi.
  Sitta ambaye alikuwa anahudhuria mkutano wa Afrika Mashariki, alisema Serikali inatakiwa kutambua kuwa vyama vya upinzani vipo na vimejiimarisha kwa kutaka kuiondoa madarakani.

  Hata hivyo, alisema ndani ya Serikali iliyopo madarakani, kuna viongozi wazuri wanaokubalika kwa wananchi.
  "Serikali hata siku moja isitegemee wapinzani wataongea lugha nyepesi, wapinzani sio rafiki zetu na kamwe hawawezi kutuonea huruma ila kinachotakiwa ni kujirekebisha haraka na kuwa wepesi wa kukubaliana na mambo," alisema Sitta na kuongeza:
  "Mfumo wa vyama vingi hauendelezi ukiritimba wa chama kimoja japo ilizoeleka kuwepo kwa chama kimoja, sasa wanatakiwa kushindana kwa hoja."

  Alisema Serikali iwe na kawaida ya kuchukua hatua za haraka pale jambo linapotokea badala ya kukaa muda mrefu bila ya kutoa maamuzi na kuwafanya wananchi kuwa na wasiwasi.

  Aidha, Waziri Sitta alisema viongozi waliopo madarakani wanatakiwa kuachana na tabia ya kutumia vyeo vyao kuendeleza biashara zao, jambo ambalo alisema hata Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alilikemea kwa lengo la kuhakikisha watu wote kuwa sawa.

  Alisema anashangaa kiongozi ambaye ni Mbunge na ni mfanyabiashara mwenye biashara kubwa anapata wapi muda wa kufanyabiashara hiyo kama sio kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuendeleza biashara zake. Alisema kuwa anaamini kuwa wakati umefika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake, Rais Kikwete, kuchukua hatua.

  Alisema Rais Kikwete hawezi kuyaacha mazuri ya CCM yakayeyuka bila sababu. Alisema anaamini kuwa viongozi wa kitaifa watahakikisha imani kwa CCM inaendelea kuwepo kwa kuwa bado kina mashabiki wengi wanaokipenda ila wanakwazika wanapowaona viongozi wao wanachelewa kuchukua hatua.

  Akizungumzia vuguvugu la kisiasa lililopo nchini, Sitta alisema sio busara kwa wapinzani kuhubiri habari za kumwaga damu na kuwataka wananchi kulinganisha wapinzani na serikali iliyopo madarakani kwa kuhoji kama itaweza kuwa serikali mbadala badala ya ile iliyopo madarakani ya CCM. Alisema ana matumaini makubwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, CCM itaendelea kuwa madarakani kwani chama hicho bado kina hazina kubwa na watapatikana viongozi wazuri watakaoweza kuongoza.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  propagandaa mix...
   
 3. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sita lazima atoe kauli hiyo kwani anambua dhairi wananchi na nchi yetu tunakoelekea: mambo ya kutishana katika karne hayana nafasi, anayeleta mchezo anawekwa pembeni. Na hili ndilo linalo enda kufanyika 2015 TMRG
   
 4. Lugovoy

  Lugovoy JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Du, leo six ameuma na kupulizia,kaazi kweli kweli!!
   
 5. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  SIX KANG'ATA NA KUPULIZA SIOO...KAMA PANYA...HATA MIMI NIMESHTUKIA BEST...Hhahaahaaha....Ila anatazamisha pamoja na kwamba anaogopa hapo alipo ndipo palipo na unga wake wa leo lazima apalinde kwa kufunika kidogo,au alishawahi kugombezwa labda kutokana na kauli zake za Dowans...!!!Ila amewatazamisha SISIEMU kuwa sio kila moto unazimwa na moto,moto mwingine unazimwa na maji...!!
   
 6. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi Mheshimiwa anaimbia serikali ipi? yeye si mmojawapo?
   
 7. n

  nchasi JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Hana lolote. Anataka kuwarudisha moyo Watz ili 2015 achukue fomu ya uraisi kupitia CCM. Someni majira ya nyakati, watu tumeshaichoka ccm hata kama viongozi wake ni wazuri vipi.
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mambo ya nimo simo hayo! hekima ya huyu baba nayo sijui ikoje?
   
 9. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Amesema kweli sita. Hujawahi kuona mchezaji mpira akijifunga bao pekee la ushindi kwa wapinzani wao? Uzembe lazima usemwe, sio wote walioko ccm wanakubaliana na uozo unaolindwa na kuendekezwa katika chama hicho. Serikalini pia sio wote wanakubaliana na legelege ya serikali ya awamu hii, kwa sababu mambo yanakwenda jumla jumla kwa jina la uwajibikaji wa pamoja, lakini ndio maana mpunga huchambuliwa kwenye mchele. Kama JK alifikiri anawaficha watu serikalini ili kulinda maovu yao ndio imekula kwake, Taifa mbele na ubinafsi nyuma baadaye. Na bado.
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CCMwanalitambua hilo ila ni kiburi, majivuno, na tambo zisizo na msingi. Sitta ni miongoni mwa wana ccm wachache sana wanaojitokeza wazi kuikosoa serikali. Wapo wana ccm wengi sana ambao kimsingi hawakubaliani na mwenendo wa utendaji wa serikali lakini unafiki umewajaa.
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  interlectual at work, hongera 6
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kimsingi 6 ni Pipooooooooz.....!
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni mtu wetu humo ndani mwao -- tusimharibie jamani!
   
 14. a

  atieno Senior Member

  #14
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijui ni siasa, au ni kitu gani? nafikiri anasoma alama za nyakati.
   
 15. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni muyendelezo wa unafiki mambo hayo akawaambie wenzake kwenye vikao vya baraza la mawaziri na kamati kuu ya chama chao.
  "Sita acha unafiki ile ofisi ya spika uliokuwa unajenga jimboni kwako sasa nani ataitumia"
  "SIONI TOFAUTI KATI YA MAFISADI NA HAWA WANAFIKI WANAOIPONDA CCM HUKU WAMENG'ANG'ANIA NDANI"
   
 16. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  naamini ulitaka kusema intellectual au siyo mkuu?
   
 17. s

  smz JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Cha msingi wajue kwamba Wa Tz wameichoka ccm. hata kama wewe ni mzuri vipi so long as umo ccm, 2015 hupati kitu. Sisi nitofauti na Libya: Wao wamemchoka Gaddafi {Raisi), sisi tumeichoka CCM (Chama). Kwa hiyo mzee wa Urambo Six fanya maamuzi bado nafasi zipo.
   
 18. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  • Kwa kifupi Mh. Sitta anajua vyombo vya dola vikitumiwa vitasababisha amani
  • Hatimaye viongozi wa serikali ya CCM wataishia The Hague
  video Clip hii chini ya selo ya The Hague iwakumbushe viongozi wa serikali ya CCM kama wakitumia vyombo vya dola badala ya hoja basi selo yao ipo hivi:

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. o

  omuhabhe Member

  #19
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa mheshimia sitta umeongea point na vilevile ume-loose points kwa upande mwingine.
  kwenye point ni pale unapowambia ccm hasa wale viongozi ambao mh.waziri mkuu mstaafu amewaita viongozi maslahi,
  ambao wengi wao ni ktk ile sombasomba ya makamba ambao ukiwasikiliza kauli zao ni kimakambamakamba
  ambazo hazina directives na tija kwa taifa.
  kwenye ku-loose points ni pale anapodhani ushindi utakuwepo tena kwa ccm 2015.
  mimi si mwanachama wa chama chochote lakini si siri kila dalili sasa hivi kwa mtanzania yeyote yule ameishaona
  ishara toka kwa Mungu wetu kuwa tuliletewa kiongozi sahihi wa kuchaghua ila kwa mbinu mbalimbali baadhi yetu
  hatuweza kung'amua hilo na tukafanya kinyume na matokeo tunayaona sasa.
  mpangilio wa wananchi kupata majibu ya utatuzi wa matatizo yao unaokana kuanzia pale bungeni,bunge lina wawakilishi wa wananchi waliowachaghua wanaenda pale kufanya mchezo kama akina JOTI.
  bunge limemalizika tumeona wote jinsi tulivyofanya makosa,sasa Bw. Sita hiyo picha ya hazina ya viongozi toka ccm
  inapatikana ktk ibara ipi ya KATIBA kwa hapo 2015??????????????????????????????.
  naomba kuwasilisha.
  NA HUYO MTZ AMBAYE BAADO ATAKUWA BAADO NA TONGOTONGO.
   
 20. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha uongo wewe, hakuna ofisi ya spika urambo. kuna ofisi ya mbunge urambo-usip[otoshe watu
   
Loading...