Waziri Simbachawene usiwe kigeugeu ndugu yangu

Kinachonishangaza ni kuona ndugu yangu huyu ambaye naamini ni msomi wa sheria leo anaamua kugeuka makusudi mbele ya umma wa watanzania bila hata kuogopa na kuzingatia maadili ya kazi yake.

Nataka niulize swali, hivi si ndio huyu huyu Simbachawene alikuwepo wakati wa kutunga katiba mpya awamu ya 4 chini ya Jaji Warioba? Alishindwa nini wakati ule kusema kuwa Wananchi hawahitaji katiba mpya? Kwenye bunge la katiba alipiga kura ya nini kupata katiba iliyopendekezwa kama mjumbe?

Hivi ninyi viongozi ni lini mtaacha kuwa vigeugeu? Hamumuogopi hata Mungu wenu?

Bora Mhe Rais alitoa msimamo wake kuwa anaimarisha uchumi kwanza lakini hakukataa katiba mpya. Hawa wasaidizi wake wakati mwingine ni wanaisumbua tu jamii na wanamwangusha kwa kujipendekeza kwake.

Waziri mzima msomi wa sheria unasimama unasema kuwa wananchi hawahitaji katiba mpya? Huu ni sawa na usaliti wa taifa, viongozi wetu wajifunze.
Hiyo ndio mwanasiasa halisi anavyutakiwa kuwa. Kigeukageuka kwa kufuata mahitaji ya siasa ya sasa hivi.
Kuwa kiongozi ndio unatakiwa uhakikishe maamuzi yako yaangalie sasa na baadae. Lawyers are always there to serve politics and never the reverse.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachonishangaza ni kuona ndugu yangu huyu ambaye naamini ni msomi wa sheria leo anaamua kugeuka makusudi mbele ya umma wa watanzania bila hata kuogopa na kuzingatia maadili ya kazi yake.

Nataka niulize swali, hivi si ndio huyu huyu Simbachawene alikuwepo wakati wa kutunga katiba mpya awamu ya 4 chini ya Jaji Warioba? Alishindwa nini wakati ule kusema kuwa Wananchi hawahitaji katiba mpya? Kwenye bunge la katiba alipiga kura ya nini kupata katiba iliyopendekezwa kama mjumbe?

Hivi ninyi viongozi ni lini mtaacha kuwa vigeugeu? Hamumuogopi hata Mungu wenu?

Bora Mhe Rais alitoa msimamo wake kuwa anaimarisha uchumi kwanza lakini hakukataa katiba mpya. Hawa wasaidizi wake wakati mwingine ni wanaisumbua tu jamii na wanamwangusha kwa kujipendekeza kwake.

Waziri mzima msomi wa sheria unasimama unasema kuwa wananchi hawahitaji katiba mpya? Huu ni sawa na usaliti wa taifa, viongozi wetu wajifunze.
VIONGOZI WETU ACHENI KUTUPOTOSHA WANANCHI
WANANCHI TULISHIRIKI KUTOA MAONI NA MAPENDEKEZO YA KATIBA KWENYE TUME YA WARIOBA KWA SABABU TUNATAKA KATIBA MPYA WAPI TULISEMA HATUTAKI?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Yaleyale mawazo ya walio wengi wa elimu za kuunga unga...mie mara ya mwisho nakumbuka Mheshimiwa alikuwa na FTC, sasa hiyo degree ya sheria itakuwa na mengineyo....
Aliisotea open university kwa miaka nane,kichwa kigumu
 
Hii naunga mkono hoja na isiwe Warioba na akina polepole warudishe posho za wanyonge ..Mana wanaikana rasimu waliyopigania..
Mie naona tuwafungulie kesi ya wizi wa kuaminiwa na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
 
Kama unafikiri wanasiasa wanajali taaluma zao, au ni watu honest wasio na vigeugeu basi una shida kubwa kichwani.
 
Kinacho mbeba ni vimiwani, suti, tie na vipodozi otherwise kichwani ni blank
 
Back
Top Bottom