Waziri Simbachawene usiwe kigeugeu ndugu yangu

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
309
1,000
Kinachonishangaza ni kuona ndugu yangu huyu ambaye naamini ni msomi wa sheria leo anaamua kugeuka makusudi mbele ya umma wa watanzania bila hata kuogopa na kuzingatia maadili ya kazi yake.

Nataka niulize swali, hivi si ndio huyu huyu Simbachawene alikuwepo wakati wa kutunga katiba mpya awamu ya 4 chini ya Jaji Warioba? Alishindwa nini wakati ule kusema kuwa Wananchi hawahitaji katiba mpya? Kwenye bunge la katiba alipiga kura ya nini kupata katiba iliyopendekezwa kama mjumbe?

Hivi ninyi viongozi ni lini mtaacha kuwa vigeugeu? Hamumuogopi hata Mungu wenu?

Bora Mhe Rais alitoa msimamo wake kuwa anaimarisha uchumi kwanza lakini hakukataa katiba mpya. Hawa wasaidizi wake wakati mwingine ni wanaisumbua tu jamii na wanamwangusha kwa kujipendekeza kwake.

Waziri mzima msomi wa sheria unasimama unasema kuwa wananchi hawahitaji katiba mpya? Huu ni sawa na usaliti wa taifa, viongozi wetu wajifunze.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,823
2,000
Ilikuwa ni Rasimu ya Katiba Mpya, viongozi wa CCM wote huicheza ngoma ya mwenyekiti wao, akiwa katili nao hujigeuza makatili, akiwa mpole nao hujigeuza wapole, nasubiri siku awe zezeta nione nao watakavyojigeuza mazezeta.
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
23,717
2,000
Yani anasema eti wala katiba haiwahusu...
Yani amechukulia wale jamaa ni kama ng'ombe masikini.
 
  • Love
Reactions: BAK

Rusumo one

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,830
2,000
Huyo achana nae ni mjomba na mbunge wangu lakini chenga tu katika Kata za kule jimboni kwake pamoja na kuwa mbunge kwa miaka tele lakini Jimbo lipo hoi, hakuna maendeleo yoyote kibri kingi aje apinge hapa najua yupo humu na Nick name yake naijua, so swala la katiba mpya kwanza hawezi kuwa na mchango wowote hiyo degree yake ya sheria aliyosoma haina msaada wowote kwa Taifa bora angesomea hata Nutrition apike komoni, Kamwene mbehwali yo!
 
Bunsen Burner

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
625

Yaleyale mawazo ya walio wengi wa elimu za kuunga unga...mie mara ya mwisho nakumbuka Mheshimiwa alikuwa na FTC, sasa hiyo degree ya sheria itakuwa na mengineyo....
 
Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
1,858
2,000
Huyu jamaa hata ukisia argument zake kuhusu sheria na ukafananisha na argument za watu kama wakina Lisu,Halima nk utagundua utofauti mkubwa sana
 
Moo B

Member
Feb 4, 2013
49
125
CCM na wat wao wanatumia ujinga wa watanzania kula mema ya nchi sasa mtu amekua mbunge kwa vipindi vitatu mfululizo eti bado anajivunia kuzungumzia changamoto zilezile ie maji, umeme, afya na barabara lakini hii yote shida inaanzia kwenye mfumo hakuna sehemu yoyote mwananchi/mpiga kura anaweza kumwajibisha kiongozi aliyemchagua kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake kwaiyo wabunge ni sehemu ya watu wanaofaidika na hii katiba tuliyonayo hawataki kabisa kusikia katiba mpya
Screenshot_20210811-220907.jpg
 
Moo B

Member
Feb 4, 2013
49
125
Huyu jamaa hata ukisia argument zake kuhusu sheria na ukafananisha na argument za watu kama wakina Lisu,Halima nk utagundua utofauti mkubwa sana
Alifeli ifunda hiyo degree ya sheria ina walakini maana aliipata baada ya kuwa mbunge ie watu waliosoma sheria wanajua mziki wa kupata hiyo degree lakini hawa wakina simbachawene hizi degree wao wanataka vyeti na tittles ila sio content ya walichosomea
 
Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
1,858
2,000
Alifeli ifunda hiyo degree ya sheria ina walakini maana aliipata baada ya kuwa mbunge ie watu waliosoma sheria wanajua mziki wa kupata hiyo degree lakini hawa wakina simbachawene hizi degree wao wanataka vyeti na tittles ila sio content ya walichosomea
Nadhani alikimbilia chuo huria
 
Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,596
2,000
Mawaziri na baadhi ya viongozi wamekua wajinga
Swali lao na jibu lao .
"Nimekuja hapa sijaona mtu ananiomba katiba"
Kero za wananchi ni maji ,barabara ,umeme .
Wakati wanajua kabisa katiba hii iliyopo ndo imeshindwa kuleta ustawi wa maendeleo..
Narudi kwa kauli ya Jenerali kuwa CCM ina wanachama milioni 8 lakini mawazo yao hayazidi 3.
 
GAUTAMA

JF-Expert Member
Aug 5, 2014
1,114
2,000
Huyo achana nae ni mjomba na mbunge wangu lakini chenga tu katika Kata za kule jimboni kwake pamoja na kuwa mbunge kwa miaka tele lakini Jimbo lipo hoi, hakuna maendeleo yoyote kibri kingi aje apinge hapa najua yupo humu na Nick name yake naijua, so swala la katiba mpya kwanza hawezi kuwa na mchango wowote hiyo degree yake ya sheria aliyosoma haina msaada wowote kwa Taifa bora angesomea hata Nutrition apike komoni, Kamwene mbehwali yo!

bee unoge
 
Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,596
2,000
Kinachonishangaza ni kuona ndugu yangu huyu ambaye naamini ni msomi wa sheria leo anaamua kugeuka makusudi mbele ya umma wa watanzania bila hata kuogopa na kuzingatia maadili ya kazi yake.

Nataka niulize swali, hivi si ndio huyu huyu Simbachawene alikuwepo wakati wa kutunga katiba mpya awamu ya 4 chini ya Jaji Warioba? Alishindwa nini wakati ule kusema kuwa Wananchi hawahitaji katiba mpya? Kwenye bunge la katiba alipiga kura ya nini kupata katiba iliyopendekezwa kama mjumbe?

Hivi ninyi viongozi ni lini mtaacha kuwa vigeugeu? Hamumuogopi hata Mungu wenu?

Bora Mhe Rais alitoa msimamo wake kuwa anaimarisha uchumi kwanza lakini hakukataa katiba mpya. Hawa wasaidizi wake wakati mwingine ni wanaisumbua tu jamii na wanamwangusha kwa kujipendekeza kwake.

Waziri mzima msomi wa sheria unasimama unasema kuwa wananchi hawahitaji katiba mpya? Huu ni sawa na usaliti wa taifa, viongozi wetu wajifunze.
Alitakiwa abaki kuwa kondakta tu
Simbachawene sio msomi kihivo ndugu yake alokua Mnikulu pale Magogoni ndo alikua anambeba.
Nadhani Baraza lijalo atafyekelewa mbali .
Uwezo wake ni mdogo alikua Madini akafeli .
Akaletwaa mambo ya ndani akafeli bila uchawi na ndumba na connection yule angerud 7 7 auze mitumba.
 
G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
843
1,000
Alifeli ifunda hiyo degree ya sheria ina walakini maana aliipata baada ya kuwa mbunge ie watu waliosoma sheria wanajua mziki wa kupata hiyo degree lakini hawa wakina simbachawene hizi degree wao wanataka vyeti na tittles ila sio content ya walichosomea
Alikuwa konda wa daladala huyu.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
9,038
2,000
Kinachonishangaza ni kuona ndugu yangu huyu ambaye naamini ni msomi wa sheria leo anaamua kugeuka makusudi mbele ya umma wa watanzania bila hata kuogopa na kuzingatia maadili ya kazi yake.

Nataka niulize swali, hivi si ndio huyu huyu Simbachawene alikuwepo wakati wa kutunga katiba mpya awamu ya 4 chini ya Jaji Warioba? Alishindwa nini wakati ule kusema kuwa Wananchi hawahitaji katiba mpya? Kwenye bunge la katiba alipiga kura ya nini kupata katiba iliyopendekezwa kama mjumbe?

Hivi ninyi viongozi ni lini mtaacha kuwa vigeugeu? Hamumuogopi hata Mungu wenu?

Bora Mhe Rais alitoa msimamo wake kuwa anaimarisha uchumi kwanza lakini hakukataa katiba mpya. Hawa wasaidizi wake wakati mwingine ni wanaisumbua tu jamii na wanamwangusha kwa kujipendekeza kwake.

Waziri mzima msomi wa sheria unasimama unasema kuwa wananchi hawahitaji katiba mpya? Huu ni sawa na usaliti wa taifa, viongozi wetu wajifunze.
Mpuuzieni huyu mbavuchawene!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom