Waziri Simbachawene ukiapa tunaomba lugha ya kiswahili itumike ktk kutoa haki

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,120
7,701
Waziri Mteule wa Katiba na Sheria Mhe. Simbachawene awali ya yote tunakupongeza kwa kuendelea kuaminiwa na Mhe. Rais.

Sisi wananchi wa Tanzania kwa masikitiko makubwa tunashangaa hadi leo bado Mahakama zinatoa Haki kwa Lugha ya kizungu pamoja na Sheria kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge.

Bado tunatafsiriwa kutoka kwenye kizungu kwenda kiswahili tena kwa maneno machache!!

Kwa nini Haki zetu zinatolewa kwa lugha ya kiingereza?! hivi huu Muhimili wa Mahakama unawahudumia watanzania au wazungu?!

kama kweli nia ni kuwahudumia wananchi kwa nini kuna ucheleweshwaji wa kutafasiri baadhi ya sheria muhimu kwa lugha ya kiswahili?!

Sisi wananchi tunakuomba Waziri Mteule ulifanyie kazi suala hili kwa maslahi ya wananchi, inaonekana kuna baadhi ya viongozi hawapo tayari kuona kiswahili kinatumika ktk kutoa haki za wananchi.

Tunaomba kiswahili kitumike kikamilifu hatutaki tafsiria kwa maneno kidogo kutoka kwenye kilicho andikwa kwa kizungu.

Wananchi tunashangaa kwa nini Mahakama zetu bado zinakumbatia lugha ya Kiingereza wakati tunao enda kutafuta haki ni waswahili watanzania?!

Kama SADC wamebadilisha sheria zao zote kwenye Lugha ya kiswahili iweje sisi Tanzania tunasuasua?! tunafanya hivyo kwa masilahi ya nani haswa?

Tunaamini Rais wetu ni Msikivu, pia tunaamini Waziri Simbachaweni ni mtetezi na msimamizi wa Haki za wananchi.....ni mategemeo yetu kuwa hii sintofahamu ya matumizi ya Lugha ya kiswahili ktk vyombo vyetu vya utoaji Haki itatatuliwa mara moja.

Mungu akubariki waziri.
 
Back
Top Bottom