figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Habari njema kwa wana Ilala na wapenda haki.
Waziri wa Tamisemi Mh George Simbachawene ameagiza wabunge wote ambao michakato ya wao kupatikana haikuanzia Ilala wasiruhisiwe kushiriki uchaguzi wa Meya na Naibu Meya.
Pia ameagiza uchaguzi huo ufanyike kabla ya tarehe 16 January 2016 ili shughuli za maendeleo kwa manispaa ya Ilala ziendelee.
Kwa sababu hiyo wabunge wote wa Zanzibar na hata wa bara ambao si wakazi wa Ilala hawaruhusiwi kushiriki mchakato wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya Manispaa ya Ilala.
From: Mwita Waitara (Mb) Ukonga
Waziri wa Tamisemi Mh George Simbachawene ameagiza wabunge wote ambao michakato ya wao kupatikana haikuanzia Ilala wasiruhisiwe kushiriki uchaguzi wa Meya na Naibu Meya.
Pia ameagiza uchaguzi huo ufanyike kabla ya tarehe 16 January 2016 ili shughuli za maendeleo kwa manispaa ya Ilala ziendelee.
Kwa sababu hiyo wabunge wote wa Zanzibar na hata wa bara ambao si wakazi wa Ilala hawaruhusiwi kushiriki mchakato wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya Manispaa ya Ilala.
From: Mwita Waitara (Mb) Ukonga
Sakata la Uchaguzi wa Meya wa manispaa ya Ilala umechukua sura mpya baada ya Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh George Simbachawene kuagiza wabunge wote ambao michakato ya wao kupatikana haikuanzia katika Manispaa ya Ilala wasiruhusiwe kushiriki uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala.
Pia ameagiza uchaguzi huo ufanyike kabla ya tarehe 16.01.2016 ili shughuli za maendeleo kwa Manispaa ya Ilala ziendelee kama ilivyo kwa maeneo mengine. Kwa sababu hiyo wabunge wote wa Zanzibar na hata wa bara ambao hawakutokana na Manispaa ya Ilala wamekosa sifa ya kushiriki kwenye uchaguzi wa Meya na Naibu meya wa Manispaa ya Ilala.
Mpango wa kukwamisha uchaguzi wa Ilala ulikuwa unafanywa na viongozi wa CCM Wilaya na Mkoa ili kuonyesha kwamba rais Magufuli hafuati utaratibu wa sheria na kanuni mbali mbali.
Majina ya Wabunge na sehemu wanazotoka waliosajiliwa katika manispaa ya Ilala na vyama vyao ni kama ifuatavyo.
Wabunge wa Chadema Manispaa ya Ilala
1. Grace Tendega-Ilala
2. Lucy Mlowe-Ilala
3. Anatropia Theonest-Segerea
4. Sware Semesi
5. Risala Kabongo
Wabunge wa CCM Manispaa ya Iala
1. Sofia Simba-Ilala
2. Angelina Malembeka-ZNZ
3. Amina Saleh Molel-ZNZ
4. Asha Abdala Juma-ZNZ
5. Martha Mlata-Singida
6. Mwantumu Dau Haji-ZNZ
7. Mariam Nassoro Kisangi-Pwani
8. Prof Joyce Ndalichako--Hajaapishwa
9. Prof Makame Mbarawa--Hajaapishwa
10. Dr Philip Mpango--Hajaapishwa
Idadi ya awali ya Wajumbe wa Baraza la madiwani Manispaa ya Ilala waliokuwepo 10.12.2015 ilikuwa na kama ifuatavyo.
UKAWA (CHADEMA + CUF) Madiwani=35
CCM(+Wabunge wa ZNZ)=31
Idadi Wajumbe wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala kwenye kikao cha Uchaguzi wa Meya jana tarehe 09.01.2015 ni Kama ifuatavyo.
UKAWA (CHADEMA + CUF) Madiwani=37
CCM (+Wabunge wa ZNZ)=34
Baada ya maelekezo ya Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, kuagiza Wabunge ambao uteuzi wao ulianzia Manispaa ya Ilala ndiyo watakaohusika na Uchaguzi wengine wasiohusika kama Wabunge wa Zanzibar na Wale wengine wa Tanzania Bara wanatakiwa waondilewe kwa kukosa sifa.
Kwa maana hiyo idadi ya Wajumbe wa CCM inaporomoka vibaya sana kama ifuatavyo.
UKAWA (CHADEMA + CUF) Madiwani=35
CCM (+Wabunge wa ZNZ)=25 (Ukiondoa na Mawaziri watatu ambao hawajaapishwa kuwa Wabunge)
Kwa maelekezo ya Mh George Simbachawene, ni dhahiri kuwa Meya na Naibu Meya wa Manispa ya Ilala atatoka UKAWA.
Mbunge wa Ukonga amempongeza Waziri wa TAMISEMI Mh. George Simbachawene kwa kutumia taaluma yake ya sheria kuonyesha nia ya dhati kulitatua jambo hili na kuingilia kati mgogoro huu wa Umeya na kutoa maelekezo stahiki kwa Vyama vya siasa. Kwa hatu hii ya Waziri wa TAMISEMI, Mh Waitara amemwahidi kuwa UKAWA watampa ushirikiano anaouhitaji ili kuwahudumia na kuwaletea maendeleo wananchi wa manispaa ya Ilala.
Last edited by a moderator: