Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 58,998
- 103,379
Ndugu yetu Simbachawene, inaonekana majukumu yako yamekushinda, sasa hivi umerukia utoaji wa maoni ya wananchi mitandaoni.
Ungetuonyesha kwanza ukamilikaji wa vitambulisho vya taifa kwa wananchi wote wenye kustahili, kisha ndio utake kuwafurahisha hao waliokuwa cheo kwa kudhibiti maoni ya wananchi.
Ifahamike mko madarakani kisheria, lakini bila ridhaa ya umma, kwani mko madarakani kwa uchaguzi uliokuwa wa kihayawani kuliko kawaida. Hali hii inawafanya kudhibiti uhuru wowote wa maoni ambao utaanika uhuni wenu uliowaingiza madarakani.
Unaweza kudhibiti magazeti, TV, redio nk, lakini kwenye mitandao huwezi maana ni technology iliyo nje ya uwezo wenu, na hila zenu za kutawala kwa shuruti.
Hivyo acha kusaka sifa za kijinga wakati umeshindwa kutupatia vitambulisho vya taifa wote tunaostahili.
Kwa taarifa yako ww unalipwa hela ya bure wakati huna tija yoyote, sasa ili kuhalalisha malipo makubwa bila tija, ndio unajifanya unataka kudhibiti uhuru wa kujieleza.