Waziri Simbachawene nimekusikia kwenye redio ila la sijui hizo hatua utazigawaje

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,269
2,000
Waziri mhe. Simbachawene nimekusikia ukielezea hatua mbalimbali zitakazo chukuliwa dhidi ya watu wanaowakejeli, watukana na kuwakashifu Rais na viongozi pamoja na hata waliofariki!

Mimi ninachojiuliza ni wewe ni waziri wa serikali ya Tanzania kwa watanzania au ni kwa wanaccm tu?

Sijui utawezaje kuwalazimisha polisi wamkamate mwanaccm aliyemtendea kosa mwanachadema?

Ni ukweli usiopingika kuna wanachadema wengi waliojeruhiwa, kufariki na kukashifiwa bila jeshi la polisi kichukua hatua zozote!

Japo polisi hiyohiyo ni nyepesi kuwakamata wanachadema kwa mambo ambayo hayana makosa kisheria.

Mhe. Waziri unajitwisha mzigo mzito uliojengwa wa ubaguzi wa kiitikadi ambao utajikuta unakandamiza kundi moja huku jingine ukilikumbatia.
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,269
2,000
Kwa ambao hawakumsikia, kauli yake imelenga sana kwenye mitandao ya kijamii na ameonya msishangae mkikamatwa.
 

Patra31

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
4,083
2,000
Tatizo siasa za kibongo bongo kupinga, kuuliza na kukosoa vyote vitaitwa kukejeli.

Watu wanajua mbinu za kujilinda sana
 

tyc

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
963
1,000
Ujumbe wako mzuri, ila usisahau mwanaCCM ex-DC Sabaya anasota mahakamani huku kashikilia kifungo cha hukumu ya kwanza

Majuzi nako Polisi walimpeleka kuzimu mwanaCCM bw Hamza kwa kumchakaza na risasi

Unapokengeuka sheria za nchi utachukuliwa hatua tu bila kujali wadhifa wako, Chama chako, kabila wala dini

Hvyo tupunguze kulialia na kutokusahau mambo
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,269
2,000
Ujumbe wako mzuri, ila usisahau mwanaCCM ex-DC Sabaya anasota mahakamani huku kashikilia kifungo cha hukumu ya kwanza

Majuzi nako Polisi walimpeleka kuzimu mwanaCCM bw Hamza kwa kumchakaza na risasi

Unapokengeuka sheria za nchi utachukuliwa hatua tu bila kujali wadhifa wako, Chama chako, kabila wala dini

Hvyo tupunguze kulialia na kutokusahau mambo
Vizuri ungeeleza hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliowaua, jeruhi, kuwatesa, kuwatukana na mengine mengi wanachadema, pia usisahau tofali la akina Rage wakimtupia mwanachadema Dodoma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom