VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Nianze kumpa pole Ndugu Lijualikali, Mbunge wa Kilombero kwa kashkash aliyoipata jana kwenye mkutano wa Madiwani kule Ifakara. Hakika, Lijualikali ameonja ladha aliyoionja Mbunge Joseph Mbilinyi Bungeni Dodoma. Nampa pole Mbunge Lijualikali na kumpa moyo wa kusonga mbele kuwatumikia wananchi wake.
Imesemwa kuwa kuna maelekezo toka kwa Waziri wa TAMISEMI iliyoelekeza kumzuia Mbunge Lijualikali kuhudhuria mkutano huo wa Madiwani kwa kile kinachosemwa kuwa Lijualikali si mjumbe wa mkutano huo. Najua kuwa Waziri wa TAMISEMI ni Ndugu George Simbachawene.
Ni wewe Simbachawene ndiye uliyeandika barua hiyo kama inavyosemwa? Hujui kuwa Wajumbe wa mkutano wa Madiwani ni pamoja na Wabunge wa majimbo yaliyo kwenye Halmashauri husika? Hujui kuwa Lijualikali ni Mbunge mmojawapo wa Halmashauri hiyo kama alivyo Mbunge wa Mlimba?
Hujui kuwa Waziri hana mamlaka yoyote juu ya Madiwani isipokuwa mamlaka juu ya Mkurugenzi ambaye hata yeye hana mamlaka juu ya Madiwani na vikao vyao? Imeshindikana vipi kujulikana kuwa Waziri hawezi kuzuia jambo linaloratibiwa na sheria?
Jambo hili lifanyiwe kazi haraka na liwekwe sawa. Litasababisha yasiyotakiwa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Unguja, Zanzibar)