seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,654
Mheshimiwa Waziri Simbachawene ameyasema hayo Leo wakati akijibu maswali yanayohusiana na malalamiko ya tozo akiwa sambamba na Waziri wa Fedha Mheshimiwa Mwigulu Nchemba
Simbachawene amesema watu lazima watambue maisha yana badilika kila wakati na kwa sasa binadamu anamahitaji mengi sana kama simu na TV ambazo hazikuwepo wakati huo hivyo Leo watu wengi wanaishi maisha mazuri zaidi ukilinganisha na zile zama ambazo TV tulijazana kwa majirani kundi la watu kutazama
Simbachawene amesisitiza kwa sasa watanzania wana mahitaji mengi hivyo wananunua data au bundle, wanalipia ving'amuzi vya TV, Kuna luxiary nyingi sana kwa sasa ndio maana watu wanaona maisha màgumu lakini Kiuhalisia wakati huo zamani ndio maisha yalikuwa magumu zaidi hakukuwa na huduma bora kama za sasa
Simbachawene amesisitiza kuwa watu wasifikiri wao viongozi wanaishi tofauti au maisha mengine kwani Maini ya nyama ya ng'ombe anayenunua Yeye au Mawaziri ni yale yale ya buchani kama watu wengine wanayokula
Waziri Simbachawene amesisitiza lazima kwa dhama hizi kelele zikijitokeza mtandaoni mfano tozo zijibiwe kwa wakati kwani watu wakiacha kupotosha mambo ya uchumi wananchi watafikiri jambo hilo ni kweli, Amesisitiza mambo ya uchumi na Sera mtu sahihi wa kuliongelea ni Waziri wa Fedha na sio mtu mwingine
Simbachawene amesisitiza kuwa wakati huo watu walikuwa na maisha màgumu sana mfano Yeye alienda shule Mazengo Sekondari akiwa ana suruali moja tu lakini Leo vijiji vingi vya Tanzania watu angalau wanaweza hata kuvaa chacha au sandles za wazi shule
Waziri amehitimisha kuwa tozo zinazokusanywa ni kwa maslahi mapana ya Taifa na hivyo watu wanapoongelea maisha Leo magumu hawafanyi ulinganifu makini kwani kwa sasa maisha sio magumu bali mahitaji yameongezeka mfano watu wanataka kula milo mitatu na kupanda boda boda kwa kilomita moja, Miaka hiyo watu walitembea kwa miguu hivyo maisha yalikuwa magumu sana
Akichangia hoja hiyo kwa basha basha Waziri wa Fedha bwana Mwigulu Nchemba amesema hata Yeye anashangaa Leo hii watu wanakula robo kuku, au Nusu kuku lakini miaka ile mfano Yeye walikuwa watu 11 kwenye Familia moja hivyo kuku akipikwa wakigawa hata neno paja utalisikia tu kwani paja linaweza kugawanywa hata mara tano ili watu wale chakula
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa hata Yeye ni maskini na anafahamu maisha kwani ndio amekuwa nayo kijijini hata Yeye hapendi kutoza watu kodi na pia hata Mheshimiwa Rais hapendi hilo lakini wananchi wana mahitaji muhimu wanayotaka yatekelezwe na jukumu hilo lote wameachiwa serikali mfano elimu bure, Afya kwa wananchi na Miundombinu ya kisasa