Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawene ametoa kali ya mwaka kwa kudai kuwa tabia ya kujipendekeza kwa wakubwa ni dalili mojawapo ya kuwabaini watu walioghushi vyeti vya kielimu na taaluma.
Simbachawene alifichua njia hiyo nyepesi ya kuwabaini wenye vyeti feki wakati akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya siku tano ya awamu ya kwanza kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri yanayotolewa na Taasisi ya uongozi mjini Dodoma, juzi.
Alisema katika kazi ya uhakiki wa vyeti, watumishi wengi walionaswa na vyeti feki ni wale waliokuwa wakipenda kujipendekeza na kufanya ushawishi (lobbying ) kwa viongozi wao. Alisema watumishi wa aina hiyo, wengine walipandishwa vyeo vya juu wakati hata uwezo wa kazi hawana, lakini mtaji wao ulikuwa ni kujipendekeza kwa wakubwa wao.
"Na hawa ndio wanaopewa vyeo sana kuweni makini. Katika zoezi la vyeti feki wengi walioshawishi sana (lobbying) na kupanda vyeo hivyo walionekana na vyeti feki", alisema Simbachawene.
Aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanawagundua watu wanaojituma bila ya kujipendekeza kwa kuwa hao ndiyo wanaofanya kazi vizuri.
Mtu ambaye siyo mfanyakazi anapenda kukaa karibu na kujikomba kwa wakubwa kwa vizawadi mbalimbali. Lakini basi fanyeni hiyo haki ya kuwagundua na hao wengine walio chini huko kwa kuwatambua ndiyo wafanyakazi... kufanya hivyo mtajenga mshikamano na kupunguza uzembe kazini ", alisema.
Alisema kuna kundi la watumishi ambao ni wajanja wanaumiza wenzao kwenye maeneo ya chini wanayotoka lakini wanajenga urafiki wa karibu na wakubwa huku wakiwapelekea wakubwa madebe ya asali, mchele na magunia ya Karanga, lakini mwishowe ndiyo hao hupandishwa vyeo.
"Kinachotokea mtu anayejituma anakata tamaa na haoni sababu ya kujiumiza na matokeo yake shule ina wanafunzi wachache na walimu wengi lakini inafelisha", alisema Simbachawene, na kuwataka wakuu hao kuwachunguza watumishi wanaopenda Kujipendekeza na kuwashtaki wenzao kwa nia ya kuwachongea ili wao wapande vyeo.
"Kama mimi ningekuwa nakubali kushawishika wanavyokuja kushtaki juu ya wakurugenzi na wakuu wa Wilaya basi hapa wengi msingekuwapo. Hakikisheni wazembe wanachukuliwa hatua", alisisitiza Waziri huyo.
Aliwataka pia kukagua miradi na kuangalia fedha za Serikali kama zimetumika ipasavyo.
Chanzo: Nipashe