Waziri Simbachawene azitaka Halmashauri kutoa elimu ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi

rose mzalendo

Member
Mar 5, 2019
71
114
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amefungua Mkutano wa mwaka wa wadau wa kilimo kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na utayari wa nchi katika kukabiliana na changamoto hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF) jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa halmashauri zote kuwa na mipango kabambe inayotekelezeka kwa ajili ya kuhakikisha elimu ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi inawafikia wakulima katika maeneo yao.

Pia amezitaka kuwajengea uwezo maafisa ugani kutekeleza jukumu hili muhimu pamoja na kuboresha mawasiliano na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na kuboresha ufikishaji wa taarifa hizi kwa wakulima na maelekezo ya nini wafanye kulingana na hali ya wakati husika.
 
Back
Top Bottom