Waziri Simbachawene awataka Watendaji Wakuu wa Polisi kuwahoji Mahabusu

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau.
Leo Mheshimiwa Waziri George Simbachawene amekutana na kufanya mazungumzo na Watendaji Wakuu Wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katika kikao hicho Waziri Simbachawene ameliagiza Jeshi la Polisi Kuhakikisha linafanya Kazi kwa weledi ili Kuondoa mlundikano wa kesi na mahabusu na pia Kuondoa tabia ya kubambikia watu kesi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amewataka Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi wawahoji watuhumiwa waliopo katika mahabusu ya vituo vya polisi nchini ili kujua makosa waliyoyafanya kama wanastahili kuwepo katika mahabusu hizo.

Waziri Simbachawene amesema lengo lake kuu la agizo hilo ni kudhibiti ubambikizwaji kesi ambao upo katika vituo mbalimbali nchini ambapo baadhi ya watuhumiwa wanapelekwa magerezani kwa makosa ambayo hawakuyafanya.

Akizungumza katika kikao chake na Watendaji hao kilichofanyika ukumbi wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam, leo, Waziri Simbachawene alisema maelekezo yake pamoja na ya Rais John Magufuli yanahusu masuala ya kesi na ubambikizaji wa kesi ambayo yapo katika baadhi ya vituo vya Polisi nchini.

Nawataka mfanye mchujo katika kesi za watuhumiwa mbalimbali waliopo mahabusu ambazo zinapelekwa mahakamani watuhumiwa hao wanafanyiwa screening hata mara mbili au tatu kwa kuwahoji makosa yao uso kwa uso ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo ndiye mwenye kesi ya mauaji, au anakesi ya kubaka, au anakesi ya wizi, na hata akipelekwa mahakamani awe ndiye anayestahili, alisema Simbachawene.

Simbachawene ameongeza kuwa, kunaweza kutokea wakati mwingine mtuhumiwa anakuwa na kesi nyingine lakini anapewa kesi ambayo hastahili na mtuhumiwa huyo anashangaa kwa kuwa sio kosa alilolitenda ambalo kakamatwa nalo.

Pia Waziri Simbachawene, aliwataka Viongozi hao wa Polisi kusimamia kwa hekima na busara suala la vijana wengi wanaoendesha bodaboda, kwa kuwa ni kundi kubwa na vijana ambao wamejiajiri kwa lengo la kupambana na ukosefu wa ajira nchini na duniani kwa ujumla.

Isitafsiriwe kwamba ukiwaona vijana waenda bodaboda ni watu wa hovyo hovyo, waendesha bodaboda wapo wenye digrii, diploma, kidato cha sita, wenye vyeti, wapo kidato cha nne, sio kundi la hovyo kama wanavyofikiri baadhi ya watu, hawa ni watu waliojiajiri na wanafanya shughuli zao kihalalikwa mujibu wa sera za nchi, kwa hivyo ni lazima tutambue mchango wao na pia tutambue changamoto zao, alisema Simbachawene.

Alisema Jeshi la Polisi linapaswa kuwa makini, na litumie busara na uadilifu na pia liwe na huruma katika kuwaangalia vijana hao waendesha bodaboda ambao wanahangaika kutafuta riziki na kuendesha maisha yao.

Aliongeza kuwa, Taifa na dunia kwa ujumla kuna ukosefu mkubwa wa ajira hivyo kunapotokea vijana wanajiari lazima eneo hilo litunzwe na lipendwe na sio kupachukulia eneo la kukomeshana kwa kuwanyanyasa na kuwafanya kama hawatakiwi katika jamii.

Aidha, Waziri Simbachawene aliwataka watendaji hao waendeleze ushirikiano walionao ili kuweza kupata njia ya mafanikio zaidi katika utendaji wa Jeshi hilo.

Hii nyimbo yenu ya maadili kwa kweli nimeependa, na ninatamani kila mwananchi ajifunze, ni mzuri na unalengo jema, hivyo wimbo huu nawataka muuishi kutokana na wimbo unavyotaka, lazima tuwe na maadili mema na tuliendeleze Jeshi letu la Polisi, alisema Simbachawene.

Kwa upande wake, Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro, alimshukuru Waziri huyo kwa kufanya kikao na viongozi wa Jeshi lake, na alimuahidi kwa kushirikiana na viongozi wenzake, watayafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa.

Tumefurahi kumpokea Mheshimiwa Waziri hapa Makao Makuu Madogo ya Polisi, ni mara ya kwanza kufika hapa, na pia amezungumzia mambo mengi, yakiwemo maadili ya kazi, na pia amezungumza masuala ya uhalifu, amesema tupambane na uhalifu mapema kwa kuzuia kabla ya kutokea, na pia amezungumza masuala ya kushirikiana ndani ya Jeshi, na pia amezungumzia masuala ya bodaboda, na tunaahidi maagizo yote aliyoagiza tutayafanyia kazi, alisema Sirro.

Waziri Simbachawene tangu ateuliwa na Rais Magufuli kuiongoza Wizara hiyo, baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, kangi Lugola, kuondolewa katika nafasi hiyo, ameanza ziara ya kutembelea taasisi za wizara yake ambazo ni Jeshi la Polisi, tayari amezungumza nao, na anatarajia kufanya kikao na Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.

Mwisho

------
FB_IMG_15821315574043306.jpg
FB_IMG_15821315474934882.jpg
FB_IMG_15821315403275247.jpg
FB_IMG_15821315329470756.jpg

_11A3091.JPG
_11A3070.JPG
IMG_4d8icr.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa ni kitu cha ajabu
Hivi Polisi kubambikiza watu kesi hawajui kwamba ni kosa hadi waziri awakumbushe?

Halafu ati wao wenyewe wakahoji mahabusi.

Huyo ndie waziri mwenye taaluma ya sheria.. This is funny.

Ana tegemea kupata mrejesho gani toka kwao zaidi ya kudanganywa?
 
Asiwasahau na wabambika kesi sugu - polisi wa usalama barabarani. Hao nao ni shida.
 
Binafsi cjamuelewa labda kama uelewa wangu ni mdogo! Hivi sheria inamtaka police akae na mahabusu kwa mda gani?

Mi nadhani police wana sero kumbe nao wana mahabusu?

Nilidhani mahabusu ambao hawajaperekwa mahakamani kwa kigezo cha upererezi wa police ndo wangehojiwa huko mahabusu ya magereza .

Wadau ufafanuzi tafadhari.
 
Waziri angewaagiza police iwe nimarufuku kumweka raia polisi zaidi ya muda ulowekwa kisheria natena angekazia Kama upelelezi Bado mtu apewe zamana, mtu anasota lumande miaka eti upelelezi hii Sheria ya kuwaweka watu lumande Bila dhamana kwa kosa ambalo halijathibitishwa niuonevu mkubwa"harafu baada ya mtu kusota miezi mingi Kisha anaachiwa eti Hana hatia ,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
This is a good move
P
katika watu wanaoonewa nchi hii na trafiki police namba moja ni daladala na boda boda sijui waliwakosea nini traffic

kundi la pili ni wamiliki wa private cars yaani kwa traffic kuwa na private car ni kama uhujumu uchumi.Hata uwe na kila kitu mikoa ya dar es salaam na Arusha utapigwa mkono kila kona ya mji

safari ndogo tu unapigwa mkono na traffic zaidi hata ya mara saba.

kuna siku nilitoka posta mpya kwenda tua mbagala mission kumfuata mgonjwa sio mbali

nilipigwa mkono wa kwanza pale sanamu ya askari monument,mkono wa pili ukanikuta pale round about ya kuelekea pale Bp daraja ra reli,nkono wa tatu nikapigwa pale bandari,mkono wa nne nikapigwa pale Salvation army mbele ya JKT mgulani,mkono wa tano nikapigwa pale mtoni kwa Azizi Ali ,Mkono wa sita nikapigwa pale mtongani mkono wa saba nikapigwa nyuma kidogo ya mbagala mission pale penye mwembe mbele ya kituo kinachojengwa cha mwendo kasi

kote huko sikuwa na kosa lolote kila kitu kilikuwa sawa wanacheki wanakuambia nenda.
yaani Traffic dar es salaam.nadhani kuna over employment wengine waondolewe wapelekwe mikoani au warudishwe kuwa polisi wa kawaida
 
katika watu wanaoonewa nchi hii na trafiki police namba moja ni daladala na boda boda sijui waliwakosea nini traffic

kundi la pili ni wamiliki wa private cars yaani kwa traffic kuwa na private car ni kama uhujumu uchumi.Hata uwe na kila kitu mikoa ya dar es salaam na Arusha utapigwa mkono kila kona ya mji

safari ndogo tu ndani ya wilaya ti unapigwa mkono na traffic zaidi hata ya mara saba.

kuna siku nilitoka posta mpya kwenda tua mbagala mission kumfuata mgonjwa

nilipigwa mkono wa kwanza pale sanamu ya askari monument,mkono wa pili ukanikuta pale round about ya kuelekea pale Bp daraja ra reli,nkono wa tatu nikapigwa pale bandari,mkono wa nne nikapigwa pale Salvation army mbele ya JKT mgulani,mkono wa tano nikapigwa pale mtoni kwa Azizi Ali ,Mkono wa sita nikapigwa pale mtongani mkono wa saba nikapigwa nyuma kidogo ya mbagala mission pale penye mwembe mbele ya kituo kinachojengwa cha mwendo kasi

kote huko sikuwa na kosa lolote kila kitu kilikuwa sawa wanacheki wanakuambia nenda.
yaani Traffic dar es salaam.nadhani kuna over employment wengine waondolewe wapelekwe mikoani au warudishwe kuwa polisi wa kawaida

Hawa maaskari kwa jinsi walivyo wengi wangekutasaidia sana kusimamia safari za usiku. Kuna umuhimu mkubwa sana kiuchumi kwa nchi kuwa na 24/7 reliable transport/access..
Tatizo hawa maaskari wetu hawaaminiki tena... Hawajiamini tena!
Sipati picha usiku itakuwaje!?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom