Waziri Simbachawene awataka matrafiki kuchapa kazi

Bandamwagaz

Member
Feb 19, 2020
18
36
(PICHANI): Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akisalimiana na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, SSP Mhandisi Joseph Shilinde, Mjini Kibaha, leo, wakati alipokua safarini akitoka Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma.

Waziri huyo amemaliza ziara yake jijini Dar es Salaam ambapo alitembelea Magereza ya Mkoa huo na aliwataka Magereza waendelee kujitegemea na waongeze kasi ya uzalishaji. Pia alilitaka Jeshi la Magereza Mkoa huo, kuanzisha kilimo cha Mboga za Majani na Matunda ili kuendelea na kasi ya uzalishaji katika Magereza Nchini.

Akiwa njiani kuelekea Jijini Dodoma, leo, alipofika Maili Moja Kibaha, Mkoani Pwani alisalimiana na Mkuu wa Usalama Barabarani na kuwapongeza askari wa Usalama Barabarani kwa kazi nzuri na kuwataka waendelee kuchapa kazi kwa weledi.
IMG_p5hs2y.jpg
 
Ila hii wizara ni ya ajabu sana. Unaweza kuwa waziri ukawa unapigiwa salute na maafisa police ila kesho yake unaamka unakuta umetumbuliwa na saluti hupigiwi tenaaaa.
 
Back
Top Bottom