reyzzap
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 6,661
- 20,995
Kuna namna nyingi mkuu..Kuingiliaje utenda kazi mkuu au kuleta uzembe na usingizi kazini?
1. Wewe Unaongea na bosi wako hujampa hata mkono, tayari kishamsukuma..
2. Barabarani, unasimamisha gari kusoma vibali, leseni, bima n.k unamsogelea dereva chini tayari ushamsaidia kufuta bonnet,
3. Ofisini umekaa kwenye kiti, chenyewe kinatakaa kikae kwenye meza,
4. Mda mwingine hata Afande anaweza akuulize..
Mbona hujachomekea?....
Kumbe mkanda umefunikwa na tumbo..
5. Unaenda uwani fasta, lakini kuitafuta bakozi ufungue mkanda mpaka uiname ukipush juu kwanza, la sivyo unajikojolea...
6. Unaendesha gari, tumbo tayari linasukuma usukani, alieoko pembeni yako naye tayari lipo kwenye dashboard,
7. Unapiga Salute, mguu haufiki juu inavyotakiwa maana chenyewe kinausukuma chini,
8. Unaenda kula mgahawani, unatoka tayari kilishanawa kwenye sink, kimepangusa meza, kishaonja mchuzi.
9. Kila baada ya mda inatakiwa uchungulie kama shati halijachomoka au au hakija fungua kifungo cha shati, Ndio maana Maana wenye vitambi kila saa unaona ana seti mkanda na kushika shika tumbo.
10. Unaitwa, unatakiwa ukimbie, chenyewe kinacheza dance,
Yaani kwa ufupi kinaweza kikukosanishe na mtu.
Wakuu ni nyingi sanaa, hapo nimezungumzia mazingira ya kazi, kwa ufupi tuepuke hii kitu...