Waziri Simbachawene amwagiza IGP kuwapangia kazi nyingine matrafiki wenye vitambi. Je, ni kosa askari kuwa na kitambi?

Hiyo vita tayari na uchonganishi kwa siro na askari wake
Siro siyo Mwanasiasa ni Mtu muelewa sana nina uhakika atajua namna ya kulifikisha suala lile kwa wasaidizi wake.

Ninachokiona hapa ni Simbachawene kupata aibu. Amri inaweza kutoka juu kupangua hoja yake. Huu nimwaka wa uchaguzi hatutaki kuwaudhi Wabeba Mbeleko Yetu.

Askari hupimwa kwa utendaji wao wa kazi na siyo kwa maumbile yao. Kwani maumbile yale yako kwa Polisi tu?? Hata kwenye nyanja zingine za Watumishi wa Umma wamejaa tele. Hata kwa kwa Madaktari ambao ni Wataalam wa afya wapo huko pia.

Tusibaguane/ tusinyanyapaane bali Tuchape Kazi Kweli kweli. Tutangurize masrai ya Taifa retu mbere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namshauri Simbachawene askari wote wenye vitambi sio traffic peke yao wapelekwe FFU walau mwaka mmoja.
 
Kitambi hakihusiani na kazi ya utraffic hata kidogo hujawahi kumuona mtu mwenye kitambi lakini ni mwepesi kwenye vitendo kuliko hata huyo asiyenacho. Tatizo letu viongozi wetu wanataka sifa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
ha haaa dunia yote hakuna kibonge mwepesi au mwenyekitambi mwepes under ceteris paribus
 
Polisi na wanajeshi wanakuwa na masaa ya mazoezi ya viungo kila wiki, haya yanahesabiwa katika masaa yao ya kazi. Kitambi ni ushahidi kuwa mmiliki alipokea pesa bila kufanya mazoezi ya viungo kwa mujibu wa mkataba.
niliwahia andika kuwa kitambi ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza, so mazoezi si dawa ya kitambi.
Na ndo maana unakuta daktari na muuguzi wanavitambi ila wanamwambia mgonjwa punguza uzito/mwili, kiufupi ni aibu binadamu yoyote kuwa na kitambi au mwili mkubwa kuliko uwezo wake ni swala la kilamtu kujichunguza kujua chanzo cha tatizo lake then kuchukua hatua si mpaka daktari akwambie punguza wanga na sukari ndo ufanye hivyo.
 
kwakuhitimisha hili mtizamo wangu ni kuwa kitambi ni ugonjwa wa lishe na ni ugonjwa wa ukosefu wa elimu nzuri ya lishe.
ufahamu wa nini chakula na nini si chakula ndio kitu cha msingi sana, ila mwarubaini wa hili swala si kuwatoa tu, ni kuwatoa na kuwasaidia kupata afya nzuri ikiwa ni elimu nzuri ya namna ya kula na mazoezi kwa afya zao maana mazoezi si dawa ya kitambi
 
Ho wameshindwa korona sasa wanataka viwango vya ulevi?

Waziri ana ya kujibu.

Kwa hiyo mtu ukiota kitambi kazini uondolewe? Lugha zingine bana
 
Nakumbuka kaka yangu RIP alipokua anasomea udaktari waliulizwa swali "Obesity is malnutrition, discuss'
Kwa kweli trafiki wengi ukiwakagua utakuta ndani mle sio nyama ila ni kinyesi kilichochacha, kama umeshakua karibu na choo ambacho trafiki yuko ndani anashusha mzigo utanielewa ba utajua barakoa si mpaka korona
✓Khahh hahahaha hahahaha hahahaha hahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Simbachawene amemwagiza IGP kuwaondoa trafiki wote wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine.

Najiuliza, ipo sheria inayokataza trafiki kuwa na kitambi? Shughuli ya utrafiki Ni ngumu kuliko majukumu ya OCD, OCS na RPC?

Natamani awamulike pia hao, ila pia tofauti na utrafiki kazi zilizobaki polisi zote ngumu na nzito hivyo sidhan Kama Kuna kitengo kinachofaa zaidi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Geogre Simbachawene, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, kuwaondoa askari wa Usalama Barabarani wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine kwani wamekosa sifa. Ametoa kauli hiyo wakati wa Kongamano la Usalama Barabarani lililofanyika jijini Dodoma lililoandaliwa na TAMWA kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia zinazochochea mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973.

"Wapo trafiki wanastahili kuondolewa kwa kukosa sifa ya kuwa trafiki! Kwa mfano wa trafiki wa Gairo wana vitambi! Askari anakuwaje na kitambi? Namuagiza IGP kuwaondoa askari wote wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine, amesema Waziri Simbachawene.

Waziri Simbachawene ameongeza kwa kusema kuwa wapo askari wasio waadilifu wanaotumia sare na kofia zao kula rushwa. "Wapo askari wa usalama barabarani ambao wamegeuza 'crown', sare nyeupe na kofia kudai rushwa kutoka kwa bodaboda, malori na kirikuu!! Naelekeza trafiki kufanya kazi kwa weledi! tuache kusimamia sheria kwa mazoea!”, amesisitiza

Amesema kuwa ajali zimekuwa zikigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya uokozi na kupoteza nguvu kazi ya taifa. "Ajali hizi zimekuwa zikiigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya maokozi na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Vilevile, Waziri Simbachawene amesema kuwa wapo madereva wanaendesha magari wakiwa wamelewa; wapo watembea kwa miguu wanavuka barabara wakiwa wamelewa; wapo madereva wanaendesha mwendokasi hatarishi katika maeneo ya makazi ya watu au yasiyoruhusiwa na alama za barabarani.

Katika kongamano hilo Waziri Simbachawene aliahidi kwamba mapendekezo hayo ya maboresho ya Sheria yaliyotolewa na wadau yatapelekwa Bungeni baada ya mchakato ndani ya Serikali kukamilika. "Serikali kupitia wizara yangu ipo katika mchakato wa kurekebisha Sheria ya Usalama Barabarani 1973, ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa", amesema Simbachawene

"Kongamano la usalama barabarani ni siku muhimu sana ya kukumbushana kuhusu masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Masuala hayo ni pamoja na kuwakumbusha madereva juu ya kuwa waangalifu na kuzingatia sheria", amehitimisha Waziri Simbachawene.

Ripoti ya usalama barabarani ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) iliyotolewa mwaka 2018, inabainisha kuwa Sheria za Tanzania zina upungufu katika kudhibiti usalama barabarani, ikiwemo kuruhusu kiwango kikubwa cha ulevi kwa madereva bila kujali uzoefu wa dereva katika kazi husika.

Tanzania imeweka ukomo wa kilevi kuwa ni 0.08g/dl lakini WHO inaeleza kuwa dereva mwenye kiwango hiki cha ulevi anakua hatarini kupata ajali mara nne zaidi ya yule ambaye hajatumia pombe kabisa. WHO pia wanashauri kuwa ni vizuri ukomo wa ulevi ukawa ni 0.05g/dl kwa madereva wazoefu na 0.02g/dl kwa madereva wapya wasio na uzoefu.
Atakuwa kawaonea traffic,vitambi vinatisha huko Police
 
Kwa observational research ndogo tu niliyoifanya trafic wengi wala rushwa ni wenye vitambi na matumbo makubwa asubuhi tu yale matumbo yanahitaji supu ya kuku au nyama na maji makubwa hiyo budget inatoka wapi na kwa mshahara gani wanaolipwa ? So kwa hawa kuomba rushwa kwao ndo suluhisho la kumanatain hivyo vitambi maan akitambu kina gharama sana
 
Hao wenye vitambi ndo wanatumia hivyo vitambi kuhifadhi vipesa vya kubrashia viatu na kununulia barakoa.....
 
Back
Top Bottom