Waziri Simbachawene afanya mazungumzo na balozi wa Marekani, Umoja wa Ulaya, asema nchi ipo salama, uchaguzi utakuwa huru na haki

KITAULO

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
1,926
2,777
PIX-5-660x400.jpg


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani, Umoja wa Ulaya (EU), Angola na Kuwait nchini, na kuwahakikishia kuwa Tanzania ipo salama, na pia katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu utakuwa wa huru na haki.

Akizungumza na mabalozi hao waliofika kwa wakati tofauti ofisi ndogo ya Wizara, jijini DSM, leo, Simbachawene amesema vyombo vyake vinaendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao nchini.

“Tunatarajia kufanya uchaguzi mwaka huu, na swali lako hali ya usalama nchini, tunawahakikishia nchi ipo salama, ulinzi utaimarishwa na uchaguzi utakua wa huru na haki,” Simbachawene.

Pia Waziri Simbachawene aliwahakikishia shirikiano zaidi kati ya Wizara yake na mabalozi hao katika masuala mbalimbali ya utendaji kazi.

“Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yangu imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio hapa nchini,” Simbachawene

Simbachawene aliwashuru mabalozi hao kwa kumtembelea, na aliwataka wawe huru muda wowote wanapohitaji kumuona wanakaribishwa ofisini kwake.

“Najisikia furaha kwa ujio wenu na karibuni sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” Simbachawene.
 
jamani serikali inaziakikishia jumuiya za kimataisfa kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki...sasa ni jambo jema kuuinga mkono serikali na juhudi zake kwa wengi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la TEC
 
WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MAREKANI, UMOJA WA ULAYA, ASEMA NCHI IPO SALAMA, UCHAGUZI UTAKUWA WA HURU NA HAKI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani, Umoja wa Ulaya (EU), Angola na Kuwait nchini, na kuwahakikishia kuwa Tanzania ipo salama, na pia katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu utakuwa wa huru na haki.

Akizungumza na mabalozi hao waliofika kwa wakati tofauti ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo, Simbachawene amesema vyombo vyake vinaendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao nchini.

Tunatarajia kufanya uchaguzi mwaka huu, na swali lako hali ya usalama nchini, tunawahakikishia nchi ipo salama, ulinzi utaimarishwa na uchaguzi utakua wa huru na haki, alisema Simbachawene.

Pia Waziri Simbachawene aliwahakikishia shirikiano zaidi kati ya Wizara yake na mabalozi hao katika masuala mbalimbali ya utendaji kazi.

“Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yangu imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio hapa nchini, alisema Simbachawene
Simbachawene aliwashuru mabalozi hao kwa kumtembelea, na aliwataka wawe huru muda wowote wanapohitaji kumuona wanakaribishwa ofisini kwake.

Najisikia furaha kwa ujio wenu na karibuni sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali, alisema Simbachawene.

MWISHO/-
PIX%201.JPG
PIX%202.JPG
PIX%207.JPG
PIX%204.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upinzani nanyi nenda mkaseme kwa ushahidi kuwa katika mazingira ya sasa hakuwezi kuwa na uchaguzi wa huru na haki. Siyo mnakaa kutoa matamko! Hawa wana uwezo wa kuwabana serikali wakatenda haki

Naunga mkono hoja, inatakiwa wapinzani watoke hadharani na kusema wazi kuwa bila tume huru ya uchaguzi hawatashiriki, na waweke ushahidi wa wazi jinsi tume isivyo huru. Hizi chaguzi za marudio na uchaguzi wa serikali za mitaa unatosha kabisa kuwa ushahidi tosha.

Wapinzani wafuatilie vizuri kuwa hata idadi ya wanaojiandikisha kupiga kura ni ndogo, na wasiojitokeza ni wapiga kura wa upinzani maana wamechoka kura zao kuchezewa. Pia nashangaa sana kwanini wapinzani hawajapeleka hoja binafsi bungeni kutaka tume huru ya uchaguzi. Inabidi bunge hili la bajeti wapeleke hoja binafsi ili wapate pakuanzia.
 
Mbona hata uchaguzi wa juzi wa Serikali za mitaa ulikuwa hulu na wa haki.hawa watu kila siku wanawaza uchaguzi tu,mnaogopa nini wakati kwenye uchaguzi wa mwezi wa kumi mtapita bila kupigwa
 
Kuna uwezekano kila upande una maana yake tofauti ya 'uchaguzi huru na haki'. Nionavyo mimi 'huru na haki' ni mambo yote yahusuyo uchaguzi ikiwemo kuhesabu kura na kutangaza matokeo.
 
Upinzani nanyi nenda mkaseme kwa ushahidi kuwa katika mazingira ya sasa hakuwezi kuwa na uchaguzi wa huru na haki. Siyo mnakaa kutoa matamko! Hawa wana uwezo wa kuwabana serikali wakatenda haki
Yes, hiyo inaitwa bandika bandua. Kabla jambo halijapoa viongozi wa upinzani walipaswa kutinga balozi hizo hizo na kuelezea kwa uwazi mahitaji ya support yao hata kwa kauli Kali dhidi ya ukandamizaji na mahitaji ya Tume huru kabla ya uchaguzi.
Wanapaswa wawaeleze kuwa bila hiyo tume uchaguzi hautafanyika kwa hiari au lazima na hata watu wao na uwekezaji wao utakuwa mashakani kama amani itatoweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom