Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,986
- 13,763
Waziri Silaa aliyasema hayo tarehe 24 Januari, 2025 wakati akizundua mfumo wa usafirishaji wa vifurushi, mizigo, na abiria ujulikanao kama “Swifpack” na kusisitiza kuwa, huduma hii itatoa fursa za kipato cha uhakika, na kuifanya kazi ya bodaboda kuwa sawa na kazi nyingine za usafirishaji wa vifurushi, mizigo, na abiria.
“Leo tunashuhudia hatua nyingine muhimu kwa Shirika la Posta Tanzania kupitia huduma ya Swifpack ambayo itawezesha upatikanaji wa huduma za usafirishaji wa vifurushi, mizigo na abiria kwa kasi, ufanisi na gharama nafuu”, alisema Waziri Silaa na
kuongeza kuwa Teknolojia inabadilisha jinsi tunavyofanya kazi na kuwasiliana, na huu ni mfano bora wa jinsi taasisi za umma zinavyoweza kutumia ubunifu wa teknolojia kutibu mahitaji ya soko na kuboresha huduma kwa wananchi.
“Moja ya mafanikio tuliyoyapata kupitia utekelezaji wa mkakati huu, tumefanikiwa kuunganisha huduma na biashara zetu kwenye programu tumizi inayojulikana kama “posta kiganjani’ inayopatikana playstore na Apple store ambapo kwa sasa kupitia programu hii mwananchi yeyote mwenye simu janja anaweza kufurahia huduma zetu za posta kiganjani mwake ikiwemo kufuatilia mzigo wake (tracking), kuomba na kufanya malipo ya huduma zetu mbalimbali”, alisema Bw. Mbodo.
Aidha, Waziri Silaa alieleza kuwa Serikali ina matarajio makubwa na kwamba huduma hii itachangia kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu kazi za bodaboda, ambazo mara nyingi zimekuwa zikipata sifa mbaya mitandaoni na kutajwa kwa changamoto mbalimbali za kijamii.