Waziri Selina Kombani (Katiba na Sheria) na Hatima ya Katiba Mpya

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Waziri Kombani adai wanaodai Katiba mpya ni watu 'wa barabarani'

Kauli ya Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, kwamba wale wanaodai katiba mpya ni watu wa barabarani wasiokuwa na uelewa juu ya masuala hayo, hakika imetusikitisha sana. Kwamba sauti zinazoendelea kupazwa kuhusu umuhimu wa kuandika katiba mpya zinatoka katika vinywa vya watu wa kawaida wanaotembea kwa miguu, kwa kweli ni kauli tete inayofaa kulaaniwa na wananchi kwa nguvu zote.

Akizungumza na gazeti dada la The Citizen mwanzoni mwa wiki, waziri huyo pia alisema hakuna umuhimu wa kuwapo katiba mpya na kwamba Serikali inaridhika na utaratibu uliopo wa kuifanyia katiba hiyo marekebisho ya mara kwa mara pindi umuhimu wa kufanya hivyo unapokuwapo. Alisema kuwa Serikali haiko tayari kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya kwa sababu wanaodai kuwapo kwa katiba hiyo hawajapeleka maombi yao serikalini kwa maandishi.

Waziri Kombani alisema maombi hayo lazima yaainishe vifungu vya katiba ambavyo wanaona vina utata na wapendekeze vifungu mbadala, lakini alionya kwamba suala hilo lina gharama na sio kipaumbele cha Serikali wala wananchi. Alisema hayo mara baada ya kuhudhuria kikao cha baraza jipya la mawaziri kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Tumelazimika kuelezea kauli ya waziri huyo kwa kirefu ili kuwatoa mashaka watu wanaoweza kudhani kuwa labda kauli yake ilikuwa mawazo yake binafsi, hivyo ilitolewa kwa nia njema tu, au kwamba kauli hiyo aliitoa kwa niaba ya Serikali, kwa maana ya kufikisha ujumbe kwa watu na asasi zinazodai katiba mpya kwamba Serikali ya Rais Kikwete haitafanya kitu kama hicho, wala hailazimiki kufanya hivyo kwa sababu suala hilo halimo katika Ilani ya chama tawala kinachounda serikali hiyo.

Ni kauli inayofifisha matumaini ya Watanzania waliodhani kwamba huu ulikuwa wakati muafaka wa kusimika katiba mpya ambayo ingebeba matakwa ya wananchi wengi badala ya katiba ya sasa ambayo ni matokeo ya mawazo na matamanio ya kundi dogo la wakereketwa wa chama tawala. Ni kauli inayolenga kuihalalisha katiba iliyopo ambayo imewekwa viraka vingi kiasi cha kutokuwa tena na nafasi ya kupachika viraka vingine. Ni kauli isiyo na ujasiri wa kutenda, bali woga wa kufanya mabadiliko kukidhi matakwa ya wananchi walio wengi na kwa wakati uliopo.

Ni kauli yenye kubeba ujumbe mzito wenye shari na jeuri. Waziri anaposema kuwa kuandika katiba mpya hakuna maslahi kwa Serikali wala taifa, hana lengo lolote zaidi ya kuwadhihaki na kuwadhalilisha wananchi wenyewe ambao kwa muda mrefu sasa, wameonyesha kiu ya kupata katiba mpya yenye kukubalika kwa wengi na kuondoa uwezekano wa kufarakana katika masuala ya msingi, ikiwamo kupata viongozi waliotokana na ridhaa ya wananchi kutokana na kuwapo tume huru ya uchaguzi itakayosimamia chaguzi zilizo huru na haki.

Tumesema tena na tena kwamba suala la katiba mpya ni la Watanzania wote na kuwa nchi yetu haina njia mbadala ya kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinakuwa vitu vya kudumu isipokuwa kusimika katiba mpya itakayokubalika kwa wengi. Ndio maana tumekuwa tukisisitiza kuwa ni vizuri Serikali ya Rais Kikwete ikajipanga sasa na kuanza mchakato wa kuhakikisha kwamba nchi yetu inapata katiba mpya ndani ya miaka mitano ijayo.

Hoja yetu daima imekuwa kwamba tusisubiri machafuko ndipo tutende, kwamba tutende wakati tukiwa bado wamoja, kwani kutenda baada ya kufarakana na kutengana au kutenda wakati nyoyo na mitima yetu ikiwa tayari imegubikwa na chuki, visirani na dhamira ya kuangamizana wenyewe kwa wenyewe, tutakuwa hatuwezi kutenda tena kwani hatutakuwa tena watu timamu bali wendawazimu.



Source: MWANANCHI 1st December 2010
 
Tufanye je sasa WATZ, Hivi hili suala si la chadema tu kama kweli watz tunahtaji changes inabidi tubadilike tuandamane nchi nzima kulaaani na kutoa tamko, FEMACT MPO NA TAMWA tusaidien jamani
 
kabla hata vidonda kupoa majeraha yake leo vyombo vya habari vimesikika vikiripoti kuwa Selina Kombani (Waziri wa katiba na sheria) akisema hakuna mpango wa kutengeneza katiba mpya.

Pili hiyo tume inayodaiwa na vyama vya siasa kuundwa ambayo itakuwa huru na haki haelewi itapaswa iweje na itaripoti kwa nani? Kwa maono yake tume lazma iwe chombo cha serikali na serikali hiyo ni ya CCM kama ilivyo sasa.

Zaidi anasema wanaotaka maboresho ya muundo wa tume wapeleke mapendekezo ili ayapitie kuona kama yanakidhi au la. Naomba kuuliza, huyu mama anapata wapi kiburi hiki? Na kwa maana hiyo taratibu za uchaguzi zitabaki hivi milele ili kukibeba chama tawala (ccm)?

Je, katiba wanayodai ni watanzania au vyama vya siasa?
 
nijuacho huyo mama yuko sahihi kabisa!
tume ya kurekebisha sheria ni ya serikali lakini katiba hutengenezwa na bunge linapokaa kama constituent assembly.

mkuu yeyote mwenye article hiyo ya katiba ya jmt 1977 atunukulie kwa faida yetu sote!
 
nijuacho huyo mama yuko sahihi kabisa!
tume ya kurekebisha sheria ni ya serikali lakini katiba hutengenezwa na bunge linapokaa kama constituent assembly.

mkuu yeyote mwenye article hiyo ya katiba ya jmt 1977 atunukulie kwa faida yetu sote!

Kama unadai unamwelewa Celina Kombani kwamba yuko sahihi basi una matatizo!
 
Namjua vema huyu mama..ni mbumbumbu kweli kweli. Kimsingi, hiyo wizara anahitajika mtu mwenye walau bachelor of laws (LLB). Sasa huyu na advanced diploma ya Mzumbe.. sijui walikosekana wengine? Maana Tanzania hii--japo haijulikani idadi yetu halisi--sasa hivi tupo zaidi ya milioni 43..
 
Waziri huyu mpya wa sheria na katiba ana uelewa kiasi gani wa issues hizi za sheria na katiba au anasema haiwezekani kwasababu ameambiwa haiwezekani tu bila kujua facts? Nina shaka sana naye!!!
 
nijuacho huyo mama yuko sahihi kabisa!
Tume ya kurekebisha sheria ni ya serikali lakini katiba hutengenezwa na bunge linapokaa kama constituent assembly.

Mkuu yeyote mwenye article hiyo ya katiba ya jmt 1977 atunukulie kwa faida yetu sote!

kama swala la katiba ni la constitutional assmbly, yeye katoka wapi leo kuongea maneno ya kuchefua kiasi hiki? Kwa kauli yakee anataka kuwaonesha watanzania kuwa yeye ana mamlaka ya kuamua kuwa katiba mpya iwepo au isiwepo?
 
Source:NIPASHE, Alhamisi, Desemba 2, 2010:
Quotation: " Mara utamsikia Tundu Lissu anazungumza....lakini Serikali haijapokea mapendekezo yao ili kujua nini wanachokitaka kifanyike ama kirekebishwe"
Niliposoma habari yote yenye kichwa Waziri anguruma madai Katiba mpya, yakiwemo pia:

  • Agusia pia Tume Huru ya Uchaguzi
  • Limo la madaraka makubwa ya Rais
Huyu Waziri kasema haya yote yanazungumzika bungeni:-

  • Katiba Mpya !!
  • Tume Huru ya Uchaguzi!!
  • Hata la Mgombea Binfsi!!
Nikadhani huyu waziri yuko Chadema!!!! Nikawaza sisiemu wana agenda gani na hoja hizi nzito kitaifa bungeni hata waseme hivi!!!!! Nikawaza labda wanahakika ya kuyatema kwa wingi wa kura bungeni; lakini nikajiuliza kama watafanya hivi ili kuhadaa watanzania, nikajiuliza hivi wana sisiemu about 5 millions katika watanzania about 40 million kweli dhana hii ikiwa ndivyo watakuwa wamepoteza mapenzi mema na nchi hii au ni sera ya sisiemu nchi hii kubakia katika kapu la nchi masikini duniani??????????!!!!!!!
Lakini ukisoma qoutation juu utaona between the lines kuwa kuwepo kwa Tundu Lissu kapu lote linakung'utwa mbele ya wote asije akaleta matatizo kwa Spika Anna na Naibu wake Ndugae mjengoni-ni mtu matata sana, mwenye maswali magumu-heri yapite haraka anavyotaka; maana Mkwere alimuona kwa mbali kuwa heri Slaa awe rais kuliko Tundu Lissu kuingia mjengoni; lakini hatimaye ameingia- iko kazi!!!!!! Haya CDM kazi kwenu!!!!!!!!!!!!
 
Mie kanikera zaidi pale Gazeti la nipashe lilipomnukuu "Mimi nasikia kwenye magazeti na kwa kuwa mimi ni mtawala, siwezi kuyafanyia kazi mambo ya mtaani, lazima hao wanaoitaka tume huru walete mapendekezo yao kwangu na mimi nitakaa na kuyachambua," alisema. Alisema wapinzani waandae na kuwasilisha mapendekezo hayo, lakini mwisho wa siku watumishi wa tume huru wanayoitaka watapaswa kuwajibika kwa serikali kwa kuwa ndio itakayowalipa na kuwagharimia kila kitu.

Sasa mtu anaesikia mpaka magezeti??? Ataweza kuwasikia binaadamu wenzie?????? Sijui masikio yake yana Macho inside 4 inside?????????
 
2nd December 2010

Agusia pia Tume Huru ya Uchaguzi
Limo la madaraka makubwa ya Rais

Serikali imewataka wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya siasa kuwasilisha mapendekezo maalum kwake kama wanataka kuwepo Tume Huru ya Uchaguzi badala ya kulalamika mitaani.

Kadhalika, Serikali imesema suala la mgombea binafsi limekabidhiwa kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba ndiye atakayeamua kuitisha mjadala miongoni mwa wabunge na kisha kulitolea uamuzi.

Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, alitoa msimamo huo wa Serikali jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na NIPASHE katika mahojiano maalum ofisini kwake.

Kombani alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku yake ya tatu akiwa ofisini baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo, alisema hajui tume huru inayoombwa na wanasiasa inatakiwa iweje na watumishi wake wagharimiwe na nani, ingawa alisisitiza kwamba ikiwa atapokea mapendekezo hayo atayafanyia kazi.

"Mimi nasikia kwenye magazeti na kwa kuwa mimi ni mtawala, siwezi kuyafanyia kazi mambo ya mtaani, lazima hao wanaoitaka tume huru walete mapendekezo yao kwangu na mimi nitakaa na kuyachambua," alisema. Alisema wapinzani waandae na kuwasilisha mapendekezo hayo, lakini mwisho wa siku watumishi wa tume huru wanayoitaka watapaswa kuwajibika kwa serikali kwa kuwa ndio itakayowalipa na kuwagharimia kila kitu.

Kuhusu kuajiri watumishi walio nje ya serikali kwa ajili ya kusimamia uchaguzi badala ya kutumia wakurugenzi wa halmashauri na maofisa watendaji wa kata, Waziri Kombani alisema suala hilo halitawezekana.

Alitoa mfano kuwa mwaka 1995 Serikali iliajiri watu kutoka nje ya Serikali kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu, lakini badala ya kufanya kazi hiyo vizuri, waliishia kukimbia na masanduku ya kura.

Alifafanua kwamba watu hao waliamua kukimbia na masanduku ya kura kwa kuwa walikuwa hawawajibiki kwa Serikali kama ilivyo kwa wakurugenzi wake inaowatumia mara zote kufanya kazi hiyo.

Alidai kuwa vyama vya upinzani ndivyo vinavyotaka Tume Huru na sio Chama Cha Mapinduzi (CCM) wala wananchi, lakini akasema suala hilo linazungumzika ikiwa upande unaolalamika utawasilisha mapendekezo rasmi.

"Mara utamsikia Tundu Lissu anazungumza kwenye vyombo vya habari, lakini Serikali haijapokea mapendekezo yao ili kujua nini wanachokitaka kifanyike ama kirekebishwe," alisema.

Alisema watu wanaotaka Tume Huru wasikate tamaa na kuangalia historia ya huko nyuma katika utawala wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, na kipindi cha kwanza cha Rais Jakaya Kikwete ambapo labda waliwahi kuwasilisha mapendekezo yao, lakini hayakufanyiwa kazi.

"Atafutaye hachoki wala hakati tamaa," alisema. Alipoulizwa kuhusu madai yanayotolewa na makundi mbalimbali ya jamii kutaka kutungwa kwa katiba mpya, Waziri Kombani alisema kuwa suala hilo linazungumzika na kwamba wanaotaka katiba mpya wapeleke hoja bungeni ijadiliwe.

Kuhusu suala la mgombea binafsi, Kombani alisema Serikali imeshajivua na kuliachia Bunge liamue, hivyo wabunge wana nafasi nzuri ya kulijadili bungeni.

Hata hivyo, suala hilo lilishawahi kuamuliwa na Mahakama Kuu mara mbili na kutaka waruhusiwe kuwepo katika chaguzi za kisiasa, lakini baadaye serikali ilikata rufaa katika Mahakama ya Rufani ambayo ilisikilizwa na jopo la majaji saba wakiongozwa na Jaji Mkuu, Augostino Ramadhani mwaka huu na waliamua suala hilo lipelekwe bungeni kwa maelezo kuwa mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi za katiba.

Akizungumzia malalamiko kwamba katiba inampa Rais madaraka makubwa na kutaka yapunguzwe, Kombani alisema suala hilo linapaswa kuwasilishwa bungeni na wabunge wanaoona kuna haja ya kufanya hivyo ili lijadiliwe na kutolewa maamuzi.

Alisema wabunge ndiyo wanaoweza kujadili suala la kumpunguzia Rais madaraka kama wanaona yamezidi, lakini akatahadharisha kuwa suala hilo linaweza kusababisha mkanganyiko na mwingiliano wa mihimili mitatu ya nchi ambayo ni Serikali, Mahakama na Bunge.

Kuhusu mikataba mibovu ambayo Serikali imekuwa ikiingia, Kombani alisema tatizo lililokuwa linachangia hali hiyo ni uelewa mdogo wa wanasheria wa Serikali katika kuandika na kuichambua mikataba.

Alisema baada ya serikali kubaini tatizo hilo, ilianzisha programu maalum ya kuwasomesha wanasheria wake ndani na nje ya nchi ili kuwawezesha kuwa na uwezo wa kumudu kufanya kazi hiyo kwa maslahi ya nchi.

Mambo mengine aliyosema atayapa kipaumbele katika uongozi wake kama Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria, alisema ni pamoja na kukomesha vitendo vya rushwa katika mahakama nchini na kupunguza mrundikano wa kesi.

Aidha, alisema ataziboresha mahakama kwa kuzipatia vitendea kazi, kutoa mafunzo kwa watumishi wa idara hiyo pamoja na kuchunguza sababu zinazochangia kuwepo kasi ndogo katika kushughulikia kesi mbalimbali. Aliahidi kukutana na watumsihi wa mahakama ili kujadiliana na kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.

Baada ya Mahakama ya Rufani kujitoa kusikiliza kesi ya mgombea binafsi, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, alisema kuwa Serikali inaweza kuaandaa na kuwasilisha muswada bungeni ili Bunge lifanye maamuzi.


CHANZO: NIPASHE
 
Hapo hakuna hoja nikuendelea kujitapa tu kwa mawaziri wapya wasiojua waanzie wapi katika kutatua matatizo yanayozikabili wizara zao

wajifunze kwa john pombe magufuli jinsi anavyojipanga katika kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Kama kombani anania ya dhati basi kwa mjibu wa wadhifa wake anao uwezo wa kumwamrisha mwanasheria wa serikali kupitia katiba na kuandika miswada mipya juu ya marekebisho ya katiba pia anao uwezo wa kuitisha kula ya maoni juu ya mabadiriko ya katiba huyo anapaka rangi tu jamani au mwasemaje?
 
Tatizo nadhani halipo ktk chuo alichosoma wala fani aliyosomea kwa kuwa uwaziri hausomewi. Tatizo mi naona ni huyu mama kukubali kuwa kipofu nakuwa tayari kutoukubali ukweli kuwa yanahitajika mabadiliko. Mbona watu wengne wasiokuwa na hata hyo diploma kama yeye lkn wanauona na kukubali umuhimu wa katiba mpya?? Yeye nani hasa? Ama kweli!!

Mwanzo huu sijui nisemeje manake kila mteule ktk hawa wapya wanajipambanua kivyake, mwingine hadi alikiri kuchakachuliwa na fataki..., na kuwaambia wanafunzi waliokuwa wakimsikiliza kuwa wawavalishe wapenzi wao kondromu na kamwe wasikubali kuchakachuliwa bila hiyo zana! Hapa kuna kitu kweli?? Hakuna kitu! Nothing! Ni wale wale tu. Mashairi mapya mdundo uleule.

Haya bwana.
 
nijuacho huyo mama yuko sahihi kabisa!
tume ya kurekebisha sheria ni ya serikali lakini katiba hutengenezwa na bunge linapokaa kama constituent assembly.

mkuu yeyote mwenye article hiyo ya katiba ya jmt 1977 atunukulie kwa faida yetu sote!

unawezakuona usivyokuwa makini. Tume inayojadiliwa ni ya uchaguzi na siyo ya kurekebisha sheria. Wewe ndo yeye tu. Na siamini kama huna matatizo tena makubwa.
 
celine kombana ni bonge la dikiteta tumefanya nae kazi pale tamisemi kamama haka kanajipendekeza kweli kanafuata pinda na kikwete wamesema nini kwahiyo kwa hiyo wizara bila maandamano haukuna kitu, haya ndio matunda ya uchakachuaji-tutapata shida kweli
 
kabla hata vidonda kupoa majeraha yake leo vyombo vya habari vimesikika vikiripoti kuwa Selina Kombani (Waziri wa katiba na sheria) akisema hakuna mpango wa kutengeneza katiba mpya. pili hiyo tume inayodaiwa na vyama vya siasa kuundwa ambayo itakuwa huru na haki haelewi itapaswa iweje na itaripoti kwa nani? Kwa maono yake tume lazma iwe chombo cha serikali na serikali hiyo ni ya ccm kama ilivyo sasa. Zaidi anasema wanaotaka maboresho ya muundo wa tume wapeleke mapendekezo ili ayapitie kuona kama yanakidhi au la. Naomba kuuliza, huyu mama anapata wapi kiburi hiki? Na kwa maana hiyo taratibu za uchaguzi zitabaki hivi milele ili kukibeba chama tawala (ccm)? Je katiba wanaodai ni watanzania au vyama vya siasa?

THE GOVERNMENT ON ONE SIDE AND CCM AS A PARTY ON ANOTHER SIDE ARE MERELY 'INVITEES' AND NOT 'MONOPOLIST' OF A CONSTITUTIONAL RE-WRITING EXERCISE:

Mama Celina Kombani need to tread CAREFULLY while issuing any statement to the public in the name of that 'government'. Many of us felt badly irked and saddened by her reckless assertions that at best suggested her just arriving from another planet if not being familiar with what had just transpired of our elections courtesy of a Constitution primarily designed to guide actions and decisions in a MONO-POLITICAL SYSTEM environment being forced to do the same in guiding Democratic Processes in a totally contrasting MULTI-POLITICAL SYSTEM setting today.

Instead of Kombani addressing the MALE CHALLENGES on the ground that her new docket must quickly add up to, she miserably choose the CCM self-agradisement path as she sought to make us believe that CONSTITUTION and CONSTITUTIONALISM is a preserve for the people in office to dictate terms - so sick and crazier a fallacy indeed!!! It sounds utterly irresponsible for a rather-thought-of motherly mind in Mama Kombani to call the CRITICAL MASS of Tanzanians calling for a most urgent starting of Constitutional re-writing a 'Pedestrian (useless / meaningless)' yelling in the streets and rural areas. The days of 'NDIO MZEE' are long gone as a new dawn of openness, accountability and wider stakeholder involvement with a possible 'SIO MZEE' becoming an order of the day. Think deeper over your recent and future statements when it comes to A PEOPLE CONSTITUTION!!

Tanzanians are no mad people. Our insistence for this project to be done long before 2015 General Elections is indeed informed by the way this year's elections were failed to achieve it primary intended participatory democratic wishes and aspirations on a free volution basis. Thus, it all make the call for a complete constitutional overhaul in Tanzania top in citizen's list as all else can painfully be asked to wait.

Likewise, it is a matter in public knowledge that Presidential Elections 2010 in Tanzania were by large a bugled exercise, a win snatched in broad daylight by installing a lame-duck into office. It is equally attested to by some most authoritative international representation in our elections (EU Election Monitoring Team) that this year's election exercise had more to do with MONKEY-BUSINESS that far way fail to meeting international standards of what a Democratic Election ought to be. This way, it means that something has to be done to permanently seal-off porous points that CCM had unilaterally exploiting to own advantage but to the deep misery of the common-people in the streets and rural areas.

As such, the MERE FACT that Dr Slaa most skillfully, wisely and painstakingly PREVENTED the nation from turning into MASS-VIOLENCE to go for what is RIGHTLY ours MUST never be interpreted by the International Community that 'Things are Under Control' the least!!! When you see a usually peace-loving citizenry of Tanzania thinking of going for someone's BLOOD only to be 'Urged Down Intelligently' by the BERIEVED Party (CHADEMA), you should be able to imagine what could very well be GOING ON DEEP DOWN UNDER THE RIVER WHOSE WATERS WERE JUST A WHILE AGO SO VIOLENTLY DISTURBED only to SADDENLY TURN quiet at the surface.

What I am saying here, it is Squarely a Business of the International Community to MOST URGENTLY ENSURE that a TOTAL CHANGE take place today by way of ALLIGNING ALL THEIR FUTURE RELATIONS AND FINANCIAL FUNDING of projects, yet to be undertaken by a President elected by NEC on behalf of Tanzanian voters, to a quicker OVERHAUL of the country's STALE CONSTITUTION for a Comprehensive Review by Ordinary Tanzanians before 2015 Elections. Should the International Donor Community seek to abdicate this central role in good time then any future SWIMMING IN A POOL OF BLOOD in my beloved country Tanzania shall all be blamed on you as the people who colluded into it preparing such an unadmirable scence.

Let all friends of Tanzania, within the country or outside, let all friends of DEMOCRACY, let all friends of Anti-Corruption fights, let all friends of MEANINGFUL poverty alleviation, let all friends of Basic Human Rights turn their ears to a MASS-CRY by ordinary Tanzanians that we get most urgently get your much needed help to enable us Comprehensively Overhaul this Opressive Independence constitution as replace it with our current WISHES and ASPIRATIONS in the modern times.

Do something Now as a sure step to help avert likelihood of free-flow blood-bath in some elections to come under the same frameworks!!! And that is our MOST IMPORTANT PRAYER to the international Community NOT TO SEEK TO FUND AND OR SPONSOR any future oppression in our ever-peaciful country. However, your sit-back on this most pressing issue of top national priority would only act as a recipe for uncontainable development by us the most oppressed Youths.
 
KATIBA MPYA ni ndoto - at least for now.

Uchaguzi wa huyu mama kuwa waziri plus mizengwe iliyopelekea uchaguzi wa Anne Makinda kuwa Speaker ni indicator tosha kabisa
 
Wana JF huyu mama, aliye mbumbumbu wa sheria ndiye anafaa kwa zoezi hili la kupata TUME HURU YA KUCHUNGUZA WIZI WA KURA; TUME HURU YA UCHAGUZI; KATIBA MPYA!! maana yeye kila kitu atafuatisha Tundu Lissu anasema nini pale mjengoni; ili na spika Anna na Naibu Ngugai wapumue!!!!!!!!!!!! Huyu jamaa Tundu Lissu kama sisiemu wataweka waziri wa sheria kama AC au EL au RA mjengoni patawaka moto!!!!!!!!!!!! Sasa si heri kuepusha shari kwa huyu mama wa Ifakara Mahenge??????
 
nijuacho huyo mama yuko sahihi kabisa!
tume ya kurekebisha sheria ni ya serikali lakini katiba hutengenezwa na bunge linapokaa kama constituent assembly.

mkuu yeyote mwenye article hiyo ya katiba ya jmt 1977 atunukulie kwa faida yetu sote!

SI CELINA KOMBANI, SI CCM WALA SI BUNGE AMBALO LINA UWEZO WA KUTUZUIA SISI UMMA WA TANZANIA KUJIANDIKIA UPYA KATIBA: SHERIA WATATUNGA WAO ILA KATIBA NI MALI YETU SISI HAPA

Celina Kombani au mtu mwingine yeyote yule HANA UBAVU wa KUZUIA juhudi za pamoja za Wananchi Tanzania kuamua kuandika upya mkataba wa utawala kati yetu na watawala wa leo na wa miaka ijayo!!! Sana sana, wana uwezo wa kuchelewesha MABADILIKO YA KWELI kutokea (Japo kwa gharama kubwa mmno) lakini si kuyazuia kamwe.

Pia, tungeomba ieleweke ya kwamba hata kule bungeni, mbunge yeyote atakayependa kuchaguliwa kwake 2015 kuwe ni kwepesi zaidi na bila kutumia gharama kubwa kwenye uchaguzi ni sharti aunge mkono kwa dhati kabisa (bila unafiki wala itikadi za pembezoni kama vile za chama, uzanzibari, ubara, ukristo, uislamu, jinsia wala nini) KUANDIKWA UPYA kwa Katiba Mpya, Kuundwa Tume huru Kuchunguza Uchakachuaji Uchaguzi 2010, na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi kuwazuia MAFISADI kujinunulia nafasi za kujiita viongozi wetu tupende tusipende bila hata ya ridhaa yetu.

Hata hivyo, endapo mtu yeyote au taasisi yoyote nchini itaonekana kuwa na mwenendo wa kuzuia mambo ambayo ni ya msingi kwetu kama KATIBA basi wategemee kukutana na sisi VIJANA uso kwa uso ndio tupate kujua kwamba Tanzania ya siku zijazo inamhusu zaidi KIONGOZI MZEE wa miaka nenda rudi serikalini au ni SISI VIJANA??? Na hata kama itakua ni kijana mwenzetu sawa yake Ndg Ndugai ndiye atakayeonekana kutukwaza sisi vijana KUWAFUNGIA MAFISADI KENGELE ya kudumu basi atatufahamu vema bila ya shida yoyote. Chezeeni mambo mengine ila kwenye haya mambo ya msingi kwetu sisi Vijana tusije tukaonana wabaya tena!!
 
Back
Top Bottom