Waziri Selina Kombani (Katiba na Sheria) na Hatima ya Katiba Mpya

kweli tunapoelekea ni kubaya na ni dalili mbaya za kupatikana kwa katiba mpya,huyu mama anaanza vibaya wakati wenzake kina Magufuli wanaleta mabadiliko chanya
 
Chikawe alikuwa pale na digrii yake ya Sheria + digrii ya ushushushu alitusaidia nini?

Mimi nmemjibu mtoa hoja tu........

quote_icon.png
Originally Posted by Mfwatiliaji
Namjua vema huyu mama..ni mbumbumbu kweli kweli. Kimsingi, hiyo wizara anahitajika mtu mwenye walau bachelor of laws (LLB). Sasa huyu na advanced diploma ya Mzumbe.. sijui walikosekana wengine? Maana Tanzania hii--japo haijulikani idadi yetu halisi--sasa hivi tupo zaidi ya milioni 43..
 
Hili swala la katiba ni wananchi wenyewe waamke na kudai katiba mpya,wananchi wakiamua si waziri wala nani mwenye uwezo wa kuizuia,hizi kauli zinatolewa na waziri kutokana na usingizi tulio nao sisi wananchi na wewe unayesoma posts hii,tuamke wananchi tusiwaachie chadema tu,

Mkuu nimekuelewa na nishaamka, lakin sijui pakuanzia.
 
unawezakuona usivyokuwa makini. Tume inayojadiliwa ni ya uchaguzi na siyo ya kurekebisha sheria. Wewe ndo yeye tu. Na siamini kama huna matatizo tena makubwa.


maelezo ya awali yalikuwa ni tume ya kurekebisha sheria lakini mkuu ame-edit. no more comment.
 
Uyu mama nae yuko shallow ivi yeye alishiriki kuitunga iyo katiba ya 1977?unaweza kuta alikuwa shule sasa hapendi kuwa sehemu ya watu watakohusika na utungajiwa wa katiba mpya?
 
Nadhani ule wasi wasi wetu juu ya umahiri wa mama huyu katika uongozi haukuwa bure. Lakini Mkuu JK alijua weakness yake na anataka kuitumia kuwaumiza Watanzania. Katiba Mpya is not a choice ni LAZIMA
 
mnaomlaumu huyu mama mnakosea kwa maana huyu mama hafanyi maamuzi kwa akili yake au kwa kufuata principals fulani. huyu mama anatumiwa na waliompa kazi hii, kesho huyo aliyempa hii kazi akimwambia anakubaliana na mabadiliko ya katiba utamuona atakavyogeuka na kuimba umuhimu wa katiba mpya. kwa bahati mbaya viongozi wengi TZN hawana principals wanazoziamini wanafuata wanachoambiwa na bosi hata kama moyoni hawakiamini na viongozi kama hawa akina celina kombaini ndio wanaorudisha nchi yetu nyuma kwa maana ya kuendelea kusimamia maamuzi ambayo moyoni wanajuwa ni mabovu lakini kwa kuwa mkubwa kasema basi ni wajibu kufuata. Suala la katiba limegeuzwa kuwa ni
la serikali yaani hiyari suala la katiba ni haki ya Watanzania na siyo hiyari ya mtu fulani kutu
kubalia au vipi ?. celina kombani ni kama kasuku ataendelea kuimba wimbo wowote bosi wake atakao muamlisha kuimba. she has no principal.
 
Waziri Celina Kombani kwa hili umechemka.

kombani.jpg
Celina Kombani

Na Dismas Lyassa
KWA muda mrefu sasa Watanzania wamekuwa wakitaka katiba mpya, kutokana na ukweli kuwa iliyopo imekuwapo tangu enzi za chama kimoja na hiyo kwa sababu tuko katika mfumo wa vyama vingi inapaswa kurekebishwa ili kwenda na wakati.Katika hali ya kawaida, hakuna haja ya kubishana juu ya ama tufanyie mabadiliko au la, kama nilivyosema kwa asili yake imetengenezwa katika mfumo wa chama kimoja, tuko kwenye mfumo wa vyama vingi, pia kuna mambo mengi ambayo yamebadilika.
Inatia aibu kusikia kuna Mtanzania au Watanzania ambao hawaoni haja, hasa kwa sababu wao wananufaika na ubaya wa katiba iliyopo. Wanaamini kwamba siku zote wataendelea kubaki kwenye upande wa kunufaika kwa namna ambavyo katiba ilivyo, kitu ambacho si kweli.

Nani alijua watu kama mzee John Malecela ambaye amewahi hata kuwa waziri mkuu wa Tanzania, kwamba siku moja angeondolewa kwenye ugombea ubunge? Yapo mengi ambayo wanaofikiri wamefika CCM ni lazima wayaangalie kwa umakini mkubwa na kutenda haki.
Katiba kwa namna inavyoonekana haitenda haki, kwa mfano ni makosa kulazimisha watu kugombea madaraka mbalimbali kupitia vyama. Inavyotakiwa ni kila mtu kuwa huru kugombea anavyotaka, yeyote ambaye anapinga hili, anavunja haki na kujiona kana kwamba yeye ni Mungu mtu.

Watanzania ni lazima tufahamu kuwa duniani tunapita, hata kama mko kwenye vyama mnaona kama ndio mmefika, huko ni kujidanganya. Ni vizuri katika kufanya kazi, katika kufanya siasa, penda kufanya haki. Usifikiri labda kwa kuwa CCM kwa sababu ni chama tawala kwa muda mrefu, ndio umefika, huko ni kujidanganya mwenyewe.
Nani alijua chama kikongwe cha siasa Kenya, KANU kingepoteza umaarufu? Hakuna, wala hakuna ambaye anapenda kufa, ila wakati mwingine ni kwa sababu ya mambo ambayo unayafanya, ingawa pia inaweza kuwa ni bahati mbaya.

Kuna wengi walikuwa maarufu ndani ya CCM, nafikiri katika kuishi kwao hawakutegemea siku moja wangeondoka na kuwa kama walivyo leo…yuko wapi aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CCM, Philip Mangula na wengine wengi ambao walikuwa tegemeo kwa CCM?
Kuna watu wengi maarufu ndani ya CCM na ambaye amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya kadhaa ikiwemo ya Mbarali, Mbeya Bibi Hawa Ngulume ambaye yuko India anatibiwa, alipelekwa huko baada ya kuomba msaada kupitia magazeti.
Kwanini nayaandika yote haya? Ni kuwaasa Watanzania walio madarakani kutojiona wamefika kiasi cha kuzungumza vitu ambavyo vinatia hasira katika jamii. Suala la kubadilishwa kwa katiba ni la lazima, sio hiari tena, anayepinga hili, anapaswa kuundiwa mpango wa kuondolewa madarakani.
Inasikitisha sana kwamba Waziri wa Sheria na Katiba, ambaye ni Mbunge aliyepita bila kupingwa ni Celina Kombani wa jimbo la Ulanga, mkoani Morogoro, anasimama na kusema serikali haina fedha kwa ajili ya kutengeneza upya katiba.
Ombi langu ni kwa wapenda mabadiliko kuanza kutengeneza vijana kwa ajili ya ikiwezekana kumuondoa madarakani kwenye uchaguzi ujao, kutokana na ukweli kwamba serikali haiwezi kukosa fedha kwa jambo zito la muhimu kama hili. Bali kinachoonekana wazi ni kwamba Kombani na serikali yake kwa sababu inanufaika na kuendelea kuwa na katiba hii inayoonekana wazi kutokuwa na haki, haioni umuhimu wa kuibadilisha.
Shukrani kwa wasomi, wanasheria, wanasiasa, wanaharakati na wananchi ambao mmeonyesha wazi misimamo yenu kwa kupingana waziwazi na kauli ya Kombani ambaye amenukuliwa hivi karibuni na vyombo vya habari akisema hakuna haja ya kuwa na katiba mpya kutokana na serikali kutokuwa na uwezo wa kifedha.

Kombani, ambaye ndio kwanza alianza rasmi kazi wiki hii akiiongoza wizara nyeti inayoshughulika na sheria na katiba, alikaririwa mapema wiki hii akisema kuwa suala la kuunda katiba mpya haliwezekani kwa kuwa serikali haina fedha na kwamba itaendelea na utaratibu uliozoeleka wa kufanya marekebisho ya katiba pale inapohitajika.
Kauli ya Kombani inapaswa kulaaniwa na wapenda amani nchini kwa kuwa imetolewa kwa lengo la kuikandamiza demokrasia ya nchi.

Kauli hiyo haina lengo jema kwa mustakabali wa taifa kwa kuwa kama serikali itang’ang’ania msimamo huo wa Kombani, basi ifahamu kuwa ni vizuri wananchi wakaidai kwa staili wanazojua, kama nilivyosema suala la katiba mpya, sio lenye kuhitaji mjadala, bali ni la lazima.
Katiba mpya ni lazima, sio kuweka viraka kama ambavyo Kombani. Ni muhimu kwa serikali katika kutimiza miaka 50 ya uhuru ikaandika katiba mpya badala ya kuendelea kung’ang’ania katiba ambayo tayari imefanyiwa marekebisho mara 15.
Katiba ikiwa mbovu, uchumi haukui; taifa haliendelei; wananchi hawamiliki mali; haki haziheshimiwi. Kama sehemu ya kuelekea miaka 50 ya kujitawala, ni muafaka kuangalia tulivyojitawala, katiba mpya ni sehemu ya kujiangalia huko.
Miongoni mwa malalamiko ya katiba ni Tume ya Uchaguzi ambayo wajumbe wake huteuliwa na rais ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala na mgombea urais, matokeo yake inashindwa kufanya kazi kulingana na matakwa ya nchi.
Kombani suala la gharama kubwa linamuhusu nini ikiwa ni wananchi walipa kodi ndio wanaoihitaji. Kimsingi suala la gharama halina maana kwa sababu katiba bora husaidia ustawi wa jamii.
Dismas Lyassa ni mwandishi wa makala gazeti la mwananchi http://dismaslyassa.com
 
selina naye anataka asikike tu, hata kama hana haki ya kutoa majibu kwa kila hoja inayotolewa na wapenda maendeleo na amani ya nchi yetu
 
A. WASIFU:
Jina: Celina Ompeshi Kombani
Nafasi: Waziri wa Katiba na Sheria
Jimbo la Ubunge: Ulanga Mashariki (2005-2010) na ametetea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Tarehe ya Kuzaliwa: 19 Juni 1959

Nafasi nyingine alizowahi kushika
Waziri: Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) (2008 – 2010).
Naibu Waziri: Ofisi ya Waziri Mkuu – Tamisemi (2006 – 2008)

Elimu:
Stashahada , Chuo cha Uongozi wa Maendeleo Mzumbe (IDM) (1985)
Shahada ya Uzamili ya Uongozi (IDM) (1992-1994)

Historia ya Ajira
Afisa Tawala Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Meneja wa Kiwanda cha Maturubai Morogoro (Morogoro Canvas Mill)( 1994-1995)

maringo-profiles: CELINA KOMBANI: MBUNGE WA MOROGORO MASHARIKI; WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA (BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LA KIKWETE 2010)
http://www.afdevinfo.com/htmlreports/peo/peo_1225.html


Dada yangu asante sana kwa CV ya mama Kombani. Sasa jibu liko wazi kwa nini alitoa jibu la kiutawala zaidi katika suala la kisheria hivi. Hii haina tofauti sana na mtu aliyeamua kujivalia gauni lake safi la HARUSI katika safari ya kushiriki mazishi.

Japo vazi itabakia kuwa ni vazi tu kwa kuwa imesaidia kushitiri mwili lakini wenye busara zao hawatoweza kuuliza maswali zaidi hadi hapa ukiweka kauliza mama huyu kwenye mizania na uzito wa jambo lililokwepo mezani toka kwa Waajiri wake - sisi wananchi walipa kodi.

Hata hivyo, mpaka kalazimika kujitokeza kiaina kada mwingine wa CCM, Wasira Stefano Tyson, kukubali matakwa ya umma ndio kusema ya kwamba kwa lugha ya mwili serikali imekiri kwamba Kombani is A NOVICE or what??

Na kama hilo ndilo jibu lao sahihi, je huenda tunao NOVICE wangapi hapo serikalini ambao tunalazimika kuwalipa mishahara kwa kodi zetu lakini PERFORMANCE ni sufuri??
 
Wandugu,
Kama kuna waziri wa jk aliyeanza kazi kwa kauli nzito basi ni waziri wa sheria na katiba mhe. Celina kombani. Inakuwaje waziri tena msomi aibuke na kusema madai yanayotolewa na baadhi ya wananchi ya kutaka katiba mpya eti yanatolewa mitaani tu kwa maana kwamba siyo rasmi. Eti wanaotaka katiba wamwandikie. Eti suala la katiba halipo kwenye ilani ya uchaguzi ya ccm. Ninachopenda kujua ni je, alichoongoea waziri ni msimamo wake binafsi au ndiyo msimamo wa serikali? Kama ni msimamo wake binafsi, jeuri hiyo ya kuwaita wanazuoni, wanaharakati na wananchi kwa ujumla kwamba wao ni watu wa mitaani, anaitoa wapi?????
 
Kaka soma alama za nyakati mapema huyu ni mtumwa tuu wa kuchokoza nyuki au pima maji ujue kina chake.
 
Mama huyu ni msomi wa aina gani au kasoma nini hasa? Kuna watu walisomea degree za uhamasishaji kule eastern europe wakajiita wasomi. Kina Prof Kapuya, Prof. Msola ambao wametupwa nje ya ulingo wa baraza la mawaziri nao wasomi. Huyu ni msomi gani sasa?
 
huyu mother uwezo wake ni mdogo sana. tamisemi alikotoka hakueleweki. kumekuwa kichaka. kila mmoja anafanya lake. kazi yake ilikuwa ni kula dili na waweka hazina wa halmasahuri za wilaya. kuwapa vyeo mafisadi wanaokula fedha za halmashauri ili mradi wampe mshiko. ofisi yake ilikuwa kituo cha majungu hasa katika kupata habari za uongo na chuki toka kwa wanasiasa wenzake kuhusu wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na majiji. uonevu chuki, umbea na upendeleo vilitawala ofisi yake. hana adabu. hiyo Wizara itamshinda. kashindwa TAMISEMI itakuwa hiyo ya wasomi. wengine walifanya sherehe alipohamishwa. I dont know where the president find this woman. she is hopeles!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Jamani si msubiri mwezi wa pili atakapokuwa anabikiriwa bungeni na Chadema? Anaweza kuwashangaza mkagundua kwamba ndiye waziri bora wa sheria tz imewahi kuwa naye. Kwani yeye hataki kuandika historia kwa wajukuu wake kwamba ndiye aliyesimia uhuru wa kweli wa watz kwa kuwapa katiba mpya?
 
hivi karibuni Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, kitendo kilichopingwa na watu wengi. Waziri Kombani alisema Katiba iliyopo itaendelea kutumika kwa vile serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha Katiba hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT), David Mwasota, alisema suala hilo hivi sasa halina mjadala hasa kwa jamii yenye akili timamu.
Alisema Katiba iliyopo haikuweka ili idumu milele, bali ilitungwa kipindi ambacho hakukuwa na uanzishwaji wa vyama vingi. “Hao wanaokataa mabadiliko ya Katiba, wana maslahi yao binafsi, lakini kwa watu walio na maono ya mbali ni lazima ibadilike maana hii iliyopo inakipa nguvu chama kimoja, wakati tuko ndani ya mfumo wa vyama vingi,” alisema Mwasota.


Naye Mtume Prosper Ntepa, alisema Katiba si mama wa chama tawala pekee, bali ni kwa ajili ya kusaidia jamii nzima hivyo ni muhimu serikali ikasikiliza kilio hicho ili kuhakikisha kinakidhi mahitaji. “Serikali isipuuze kilio cha wananchi maana ni kilio halali na kimekuja kipindi husika; ni lazima Katiba ibadilishwe bila kuhofu hasa kwa wale wote wanaoitakia mema nchi na wapenda demokrasia,” alisisitiza Ntepa.

Hivi karibuni viongozi mbalimbali walijitokeza kueleza msimamo wao kuhusu kubadilishwa kwa Katiba, akiwemo Mwanazuoni na mwanaharakati mashuhuri nchini, Profesa Issa Shivji, Jaji Mkuu mstaafu Mark Bomani na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk. Steven Munga, alisema umefika sasa wa serikali kuona mabadiliko ya Katiba ni sehemu ya maisha ya wananchi.
“Jamii imebadilika, mfumo wa maisha umebadilika… sasa ni wazi kwamba Katiba iliyopo nayo lazima ibadilike, serikali ifikie hatua ikubali jambo,” alisema Askofu Munga.


Naye Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Bukoba, Methodius Kilaini, aliwataka wanasiasa kuorodhesha mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye mabadiliko hayo, kisha wayapeleke kwao ili nao waongeze nguvu ya mabadiliko. “Sisi tunawategemea sana wanasiasa watwambie maeneo ambayo yana upungufu, waorodheshe walete kwetu, tutawasaidia kuchochea hili kwani haliepukiki hata kidogo,” alisema Askofu Kilaini.


Naye Askofu wa Kanisa la GRC la Ubungo Kibangu, Antony Anthony Lusekelo, alisema Katiba mpya lazima ipatikane kwa serikali kuhakikisha inafuata utaratibu wa kushirikisha wananchi kutoa mapendekezo yao.
Alisema kipindi hiki ni muhimu kuwa na Katiba itakayokuwa na mawazo ya kila mdau, kama ilivyokuwa kipindi cha kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, ambapo hakuna madhara yaliyojitokeza kwani kila mwananchi alishirikishwa.
“Lazima tuone mbali na serikali ione hilo… ni muhimu katika hili kuhakikisha kunakuwa na mjadala mpana utakaoshirikisha watu wote kama ilivyotokea kipindi cha vyama vingi ambapo kila mwananchi alishirikishwa,” alisema Askofu Lusekelo. Alisema kama Katiba ikipatikana kwa amani, hakutakuwa na madhara, lakini iwapo serikali itapuuza matakwa ya wengi kuna uwezekano wa Katiba kuleta maafa jambo ambalo halipendezi hata kidogo.

BALOZI Hashim Mbita ambaye alikuwa Katibu wa Kamati ya Ukombozi ya uliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) amewashangaa wanasiasa wanaoogopa kuifanyia mabadiliko katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
huyu mama hayawani, amekariri kua serikali ndiyo kila kitu. akasahau kua serikali ni watu, na hao watu ndo wanadai katiba mpya. lets ignore her, go on fighting for the katiba am sure very soon tutaipata.
 
Back
Top Bottom