Waziri Selemani Jafo ashauri kuanzishwa kwa wiki ya nyungu katika kupambana na Corona

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
3,984
4,131
Waziri wa Tamisemi amesisitiza watanzania waanze kujifukiza kama namna ya kujenga kinga katika kupambana na corona.

Ili jambo liwe na ufanisi amependekeza kuwe na wiki ya nyungu kwa maana ya wiki ya kujifukiza. Kama ambavyo mh Rais alipendekeza hivi karibuni.

Amesema tutumia,mipapai,miarobaini,miembe,mibuyu,michachai iwe chochote kile unachoamini kinafaa kujifukizia.

Hii itasaidia kuitokomeza corona.

Tusione haya kuwa ni ushirikina, Tujifukizie.

Corona ipo,zingatia taratibu za afya kadiri zinavyotolewa hata zile za WHO.

Hawa ndiyo wasomi tulio nao! Hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa kujifukizia ni tiba ya Coronavirus bali kuna ushahidi wa kisayansi kuwa kujifukizia kunaua mapafu. Taifa ambalo haliwekezi katika tafiti, sayansi na technolojia ni Taifa mfu
 
Waziri wa Tamisemi amesisitiza watanzania waanze kujifukiza kama namna ya kujenga kinga katika kupambana na corona.

Ili jambo liwe na ufanisi amependekeza kuwe na wiki ya nyungu kwa maana ya wiki ya kujifukiza. Kama ambavyo mh Rais alipendekeza hivi karibuni.

Amesema tutumia,mipapai,miarobaini,miembe,mibuyu,michachai iwe chochote kile unachoamini kinafaa kujifukizia.

Hii itasaidia kuitokomeza corona.

Tusione haya kuwa ni ushirikina, Tujifukizie.

Corona ipo,zingatia taratibu za afya kadiri zinavyotolewa hata zile za WHO.

Sent using iphone pro max
Waukae huyu naunga mkono hoja...
IMG_20200320_223458.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli kama hawa ndo viongozi wetu basi kuna kasoro kubwa katika Taifa letu,nilitegemea waziri ahimize uvaaji wa barakoa na kugawa barakoa bure

Na mtafanya Babu wa Leliondo afufuke,

Halafu Tanzania ni mwanachama wa WHO kwa nini wasipeleke hii tiba kule iwe proved kama njia mojawapo ya kuuisadia Dunia ? Ambapo WHO wangeiongeza kwenye moja ya njia za kujikinga na maambukizi ya Covid 19

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..mitaani ndio kuna uwezo mbadala wa kupiga vita korona. mitaani ndio wapo Wananchi-manesi, madaktari, waganga wa kienyeji, hao vile vile ni wazazi, ambao pia ni viongozi kuna ulazima wa kufanya juhudi hizi mitaani ambamo Mh. Jafo ndio kiongozi mkuu wa mitaa.

Mfano tu: kuna wapishi(mama ntilie) kwa kutumia miongozo au protokali za afya wachaguliwe ambao badala ya kusafiri kwenda kuuza mitaani ambako siko kwao, basi watumie hata simu za mkononi na kupokea oda za walaji, wapite kuchukua wakalie majumbani mwao.

Washonaji: wapo wa mtaani, wapewe elimu kwa namna ya kutumia vitambaa vninavyoaminika kupunguza virusi, washone, wasambaze mitaani....

TAMISEMI must act na sio kushurutiwa
 
Nawaza kujifukiza na bangi sijui kama serikali itakuwa bega kwa bega na mimi.

Kwa kweli kama hiyo bangi itakusaidia basi heko kwako, laiti umejufukuzia kabla ya bandiko lako, basi limekuongezea masihara. Masihara kama hayo ni kejeli kwa wale wanaotafuta nguvu za kundokana na tauni
 
Katika vikao vya familia akinyoosha mkono yule asiye na elimu au kipato itaonekana anataka kuleta vurugu,ila aliyenacho husikilizwa hata kama anachokiongea hakieleweki!!

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Back
Top Bottom