TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Nimepata habari muda huu huu kwamba ajali mbaya imetokea Wilani Njombe , na katika ajali hiyo Mh.Salome Mbatia amefariki. Mtoa taarifa hakuweza kunieleza zaidi maana alikuwa na wasi wasi ila kasema miongoni mwa walio fariki ni waziri Salome Mbatia .

Mengine nitayasema kwa kadiri nitakavyo weza kuyapata.
---

1713093622024.png
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bibi Salome Mbatia, amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana saa 10: 45 eneo la Kibena Factory wilayani Njombe mkoani Iringa.

Akithibitisha kutokea kifo hicho kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. David Mathayo, alisema marehemu Mbatia alikumbwa na mkasa huo akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Njombe, akiwa katika gari lake binafsi, Nissan Patrol namba T 724 AGZ.

“Tupo hapa tunajaribu kukata bati tuwatoe, ni kweli wamekufa alikuwa kwenye gari lake binafsi, Nissan Patrol yeye na dereva wake, “alisema Dkt. Mathayo.

Alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya Mitsubishi Fusso lenye namba T 299 AFJ lililokuwa likitoka Njombe kwenda Makambako kuhama njia yakena kugongana uso kwa uso na gari la waziri huyo.

“Nimepata taarifa kuna watu walikuwa wanamsubiri (Naibu Waziri) huko Njombe, naamini alikuwa safarini kwenda huko lakini sielewi ilikuwa safari ya kikazi au binafsi,” alisema Dkt. Mathayo.

Dkt. Mathayo alikumbana na tukio hilo wakati akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Tunduma kikazi kufuatilia manunuzi ya korosho. Alisema mtu mmoja ambaye hakutambulika mara moja aliyekuwa kwenye lori hilo, naye alikufa papo hapo.

Francis Godwin kutoka Iringa anaripoti kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Bw. Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo nakueleza nakuwataja waliofariki kuwa ni watu watatu, akiwemo Waziri Mbatia. Alisema polisi mkoani hapa wanaendelea na uchunguzi ajali hiyo , watatoa taarifa kamili baada ya kukamilika uchunguzi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Njombe, Dkt. John Luanda alithibitisha kupokea majeruhi wa ajali hiyo na kwamba baadhi ya madaktari walikwenda eneo la tukio kusaidia kutoa miili iliyong’ang’ania kwenye mabaki ya magari hayo.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio, zilisema mbali ya Dkt. Mathayo, watu wengine walikuwa kwenye eneo la tukio na kutoa msaada mkubwa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe ambaye alikuwa safarini kwenda mkoani Ruvuma.

Bw. Kabwe alimweleza mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kuwa alishuhudia magari hayo yakigonganga uso kwa uso na kulazimika kukatiza safari yake kusadia kuwahisha majeruhi hospitali.

Moja ya matukio ya kukumbukwa kwa naibu waziri huyo ni kwamba Machi 8 mwaka huu wakati wa kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, alitembelea chumba cha habari cha gazeti la Majira kama mgeni rasmi na kujionea jinsi waandishi na wafanyakazi wanawake, walivyokuwa wakiandaa gazeti siku hiyo.

Akiwa kwenye chumba hicho cha habari, marehemu Mbatia aliwaasa wanawake wa Kampuni ya Business Times inayomiliki magazeti ya Business Times , Majira, Dar Leo, Spoti Starehe na Maisha kuwa wachapakazi na kueleza jinsi alivyofurahishwa kuona jitihada zao Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge, marehemu Mbatia, alizaliwa Juni 17, 1952 na kupata elimu yake ya msingi katika shule za St. Ann (1959-1962), St. Theresa (1963-1964) na Shule ya Msingi Msimbazi (1965-1966).

Aliendelea na elimu ya sekondari kwenye shule ya St. Joseph (1967-1970) na kuhitimu elimu ya juu ya sekondari kwenye Shule ya Wasichana ya Korogwe mwaka 1972.

Marehemu pia alikuwa mmoja wa wanawake wasomi kwa kupata elimu ya juu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi akiwa mtaalamu aliyebobea katika masuala ya utawala na uchumi.

Wasifu wake unaonesha kuwa alipata shahada ya kwanza ya sanaa [BA (Hons)] kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1976 kabla ya mwaka 1982 kujiunga na Chuo cha ADL nchini Marekani ambako alipata shahada ya uzamili katika utawala (MSc. Management).

Pia alikwenda nchini Uholanzi mwaka 1987 ambako alipata Diploma ya Uzamivu katika Utawala (Post-Graduate Diploma in Administration & Management) kutoka chuo cha RVB Delft.

Kabla ya kuingia katika siasa, marehemu alifanya kazi mbalimbali za fani alizosomea ambapo mwaka 1977 aliajiriwa na Bodi ya Biashara ya Nje akiwa mfanyakazi-mwanafunzi kabla ya kupanda vyeo hadi kuwa Meneja Masoko na kisha Meneja wa Mauzo wa Kanda.

Mwaka 1979 alijiunga na kampuni ya Biashara Consumer Services Co. Ltd ambako alipanda vyeo hadi kufikia wadhifa wa Meneja Mkuu mwaka 1990.

Mwaka 1998 alikuwa Katibu Mkuu wa Taifa wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT) wadhifa alioutumikia hadi mwaka 2005.

Aliingia kwenye siasa mwaka 2000 ambapo amekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kutoka mkoa wa Kilimanjaro na kuwa pia mjumbe wa Mkutano Mkuu. Amekuwa pia kwa miaka kadhaa sasa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Uwekezaji la Taifa (NICO).

Kati ya mwaka 2002 na 2005 alikuwa Mweka Hazina wa chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na kuonesha umahiri katika siasa hasa wakati wa kampeni ambapo alikuwa mmoja wa makada waliokuwa wakiaminika sana katika kuipigia kampeni CCM hasa kwenye majimbo yaliyokuwa yakionekana kuwa na upinzani mkali.

Januari mosi mwaka jana, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Uchumi, Mipango na Uwezeshaji kabla ya Oktoba 17 mwaka huo huo kuhamishiwa kuwa Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nafasi aliyokuwa nayo hadi mauti yalipomfika jana.

Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kukumbana na matukio ya kupigwa riasasi
- DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

- Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)

- Kifo chenye utata cha Waziri Nicas Mahinda

- John Mwankenja auawa kwa risasi

- Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

- Maandamano ya CHADEMA: Aqulina Akwilini Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika
 
Habari nilizozipata sekunde kadhaa zilizopita ni kuwa Ajali nyingibe Mbaya imetokea huko Iringa, iliyomhusisha Salome Mbatia.

Habari zinasema kwamba amefariki dunia!
Bado tunaendelea kufuatilia jinsi ilivyotokea!
 
tusubiri tusikie zaidi manake tusije kutoa pole na pengine yupo hai.

invisible......hebu twambie khabari hii.

mkuu umeanza kuelewa sasa ?

hapa jamvini tumepunguza sana credability, kwa kuleta habari ambazo baadae zinakuja bainika kuwa si za kweli.

wacha tusubiri kwana, hatuwezi kusema si kweli wala ni kweli hadi tuzithibitishe kwa vyanzo vingi au kwa wale ambaowanaaminika kuwahawajawahi kutudanganyana
 
Mtu wa Pwani test yako ni nzito sana "mtu anayeaminika au ambaye hajawahi kutudanganya" Mkuu hiyo ni kali.
 
Hapa hadhi bado iko juu ila unaweza wewe pekee ndiye umejipunguzia credibility ama hutaki kuelewa . Habari hizi nimezipata kwa mtu muhimu sana aliyekuwa katika mmojawapo wa misafara akielekea Songea na yuko katika eneo la tukio hilo. Katika watu walio kufa kathibitisha kwamba Ndugu Salome kafariki na mengine atanipa kadiri muda unavyo enda .
 
mkuu umeanza kuelewa sasa ?

hapa jamvini tumepunguza sana credability, kwa kuleta habari ambazo baadae zinakuja bainika kuwa si za kweli.

wacha tusubiri kwana, hatuwezi kusema si kweli wala ni kweli hadi tuzithibitishe kwa vyanzo vingi au kwa wale ambaowanaaminika kuwahawajawahi kutudanganyana

mtu wa pwani......

mie napenda sana jinsi invisible anavyojibu hoja ndio maana nikasema hii habari afuatilie kwa makini.

so far nimewasiliana na washikaji bongo naona hawana taarifa hizo but bado mapema na wao wanajaribu kuulizia zaidi.wanasubiri taarifa ya habari CHANNEL 10 ya saa 1900.
 
Waziri Salome Mbatia amefariki katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Kibena Factory (kati ya Makambako na Njombe)saa 11 kasorobo jioni ya leo. Pamoja naye wamefariki watu wengine wawili. Waziri alikuwa katika gari dogo aina ya Nissan ambalo liligongana na Lori la Fuso lilikuwa limeshehena mbao. Lori hilo liliangukia gari hilo dogo na kuwaua watu hao papo hapo. Ninavyoandika hivi, bado wanajaribu kuitoa miili ya marehemu...
 
Du! Mambo yamekuwa siyo mambo.

Hali inaelekea kubaya sana, inabidi kujiuliza kulikoni?
Mungu awape nguvu za Kustahimili!
 
sasa habari iaminini na nnatanguliza samahani sana kwako lunyungu maana wewe hasa habari zako zina walakin

inna lillahi wa innna ilayhi rajiiun

mola ndie alietupa na mola ndie aliechukua.
mola ape subira wanafamilia yake, ndugu na jamaa zake, rais wa jamhuri ya muungano, viongozi wote wa vyama na serikali. hasa mawaziri wenziwe na wabunge wenziwe
 
Ni kweli Mwanakijiji maana kuna ndugu mmoja yuko hapo hapo anasema hali ni mbaya sana .
 
viongozi ni binadamu wa kawaida tu, kama mtashangaa viongozi kufa kwa ajali sidhani kama itakuwa vizuri kutoshangaa wananchi wanaokwisha kila siku kwa ajali ya gari !
 
nitawaletea taarifa toka eneo la tukio as they become available.. kwa vile bado wako kwenye shughuli ya kunasua miili viongozi wa Polisi hawapatikani na hawajaweza kuzungumzia lolote kwa kirefu. Nilichoweza kupata ni hiyo confirmation ya habari ya Lunyungu na niomba Mods mchukue hayo niliyoongezea na kuyaingiza kwenye original threat ya Lunyungu ...

KLH News.. inamtandao wa kutosha kuthibitisha habari mahali popote Tanzania, tukifanya makosa ya hapa na pale ni udhaifu wetu, lakini hii haina shaka hata kidogo.
 
mwaka huu ni mzito, maana sijui nisemeje, wengine wataanza kushangiria sasa hivi, ila nnawaomba kwa hili tuache na tuhuzunike ni msiba wetu sote na ajali haina bwana wala bibi na wala haina chama. kwa hili tuungane kuonesha huzuni zetu.

pia tukae kujiuliza kwa nn tanzania sasa kuna ajali nyingi na zaidi viongozi? kuna nini? somo gani tunalipata hapa?
 
Back
Top Bottom