Coping Strategy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2014
- 439
- 384
Na ile project ya pale ukonga magereza nyumba za maaskari. Miez minne wanafyatua tu tofali.
TBA not TPAJisomeeni hapa.. Sisi tunasema TPA hakuna kitu lbda wangewapa SUMA JKT
Profesa Ndalichako awawashia moto TBA
Waziri wa Elimu, Joyce Ndlichako ametembelea mradi wa ujenzi wa madarasa, Hostel na ofisi kwa ajili ya chuo kikuu cha Muhimbili Kampasi ya Mloganzila ambapo baada ya kutembelea mradi huo hakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo ambao unasimamiwa na wakala wa majengo Tanzania 'TBA'.
Kutokana na kutoridhishwa huko ametoa wiki moja vifaa vya ujenzi viwe vimefika na mafundi wa kutosha waongezwe vinginevyo amemuagiza katibu Mkuu wa wizara hiyo kuangalia namna ya kuvunja huo mkataba
mmhSekta binafsi wengi hawa wazawa nao walijenga vitu visivyo imara. Kuna chuo flani cha umma miaka ya 2004 hadi 2008 walijenga Theatre Halls za ajabu. Miezi michache tangu kuzinduliwa zilitokea nyufa.
Tuna tatizo na wahandisi wengi wazawa kuwa na uwezo mdogo kwenye ufanyaji kazi kwa vitendo. Kuanzia usimamizi hadi utendaji kazi wenyewe.
Pamoja na kuongezewa majukumu wamenyimwa kibali cha kuajiri, kwahiyo wanastaff wachache sana ambao wanatisha kuwa wasimamizi na wakaguzi zaidi na sio wajenziBasically TBA walikuwa wasimamizi. Sasa Magu kawafanya wajenzi wakubwa. Hawakuwa tayari kwa hilo. Kati ya usimamizi na ujenzi wachague moja.
Hata hivyo msimamizi (regulayor) wa kanuni za ujenzi na majengo anapogeuka mjenzi nani atamsimamia yeye? Incase ikitokea kavurunda kwenye ujenzi huo nani atamwajibisha wakati yeye ndo msimamizi mwenyewe? Lakini huyu msimamizi (TBA) anayesimamia wajenzi na majengo kumbe yeye mwenyewe hana weledi wa taaluma hiyo huwa anawasimamiaje hao wajenzi? TBA ifumuliwe na kujengwa upya!Basically TBA walikuwa wasimamizi. Sasa Magu kawafanya wajenzi wakubwa. Hawakuwa tayari kwa hilo. Kati ya usimamizi na ujenzi wachague moja.
TBA ina staff wachache sana kama hujui mkuu, pia chama ndiyo kinapatia huko hela ya kununua wapinzani.Kwa hatua alizochukua waziri mkuu ....basi ile issue ya yule dogo aliyetoa picha za expansion joint kwenye hostel za udsm alikuwa sahihi kabisa.....TBA waliboronga
Ova