Waziri Prof. Muhongo: Mpango wa kuchimba Uranium upo pale pale

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,975
4,264
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo amesema kuwa mpango wa serikali kuchimba madini ya Uranium eneo la Mkuju upo pale pale na hakuna mabadiliko. Licha ya kudai kuwa baadhi ya nchi zinataka Tanzania kusitisha mpango huo wa kuchimba madini hayo.

" Tanzania sio nchi ya kwanza kuchimba madini ya Uranium na kwa kuwa yanahitajika kwa matumizi mbalimbali kama kutoa nishati, kutengeneza silaha na matumizi mengine basi na sisi tutayachimba" alisema waziri.

Alisema pia uchunguzi wa kupima athari kwa mazingira (Social and environment risk assessment) vimeshafanyika na wamejiridhisha kuwa hakuna athari itakayotokea katika hifadhi ya Selous.

SOURCE; allafrica.com/stories
 
Ila ni vizuri wakafuata ushauri Wa kitaalamu zaidi wasijipeleke kichwa kichwa.
Na Tanzania inakawaida moja ya kusikiliza ushauribwa wanasiasa zaidi kuliko ule Wa kitaalamu.
 
Mipangooo miingiii bila vipaumbele!!aaahhhh
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo amesema kuwa mpango wa serikali kuchimba madini ya Uranium eneo la Mkuju upo pale pale na hakuna mabadiliko. Licha ya kudai kuwa baadhi ya nchi zinataka Tanzania kusitisha mpango huo wa kuchimba madini hayo.

" Tanzania sio nchi ya kwanza kuchimba madini ya Uranium na kwa kuwa yanahitajika kwa matumizi mbalimbali kama kutoa nishati, kutengeneza silaha na matumizi mengine basi na sisi tutayachimba" alisema waziri.

Alisema pia uchunguzi wa kupima athari kwa mazingira (Social and environment risk assessment) vimeshafanyika na wamejiridhisha kuwa hakuna athari itakayotokea katika hifadhi ya Selous.

SOURCE; allafrica.com/stories
 
Ubaya ni kuwa Dereva na Konda wake wanaendesha daladala letu kinyume na maumbile!!!
 
Hizo rasimali zote bila kua na uzalendo ni kazi bure watanzania tunahitaji kujitambua na tungepata kwanza akili kabla ya hizo rasilimali
 
Back
Top Bottom