Waziri Pindi Chana ahimiza ubunifu na weledi kwa watumishi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
732
475
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa Watumishi wa Wizara hiyo waendelee kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza vipaumbele vilivyowekwa.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo jijini Dodoma akisisitiza kuwa licha ya watumishi wa Wizara hiyo kufanya mambo mengi mazuri wanatakiwa waendelee kuwa wabunifu ili kusaidia Sekta za Wizara hiyo ziendelee kufanya vizuri kwa kuwa zimeajiri vijana wengi na kutoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kufanyika kwa baraza hilo kuna umuhimu mkubwa katika kuleta ustawi wa watumishi wa umma pia kutoa fursa ya kujadili kwa kina changamoto, mipango na mikakati ya kuendeleza na kuleta ufanisi mahala pa kazi.

Awali akiwasilisha taarifa ya Wizara hiyo, Katibu Mkuu Ndg. Saidi Yakubu amesema kuwa Baraza hilo litapokea taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2022/23 na kutoa maoni kuhusu Bajeti ya mwaka ujao wa Fedha.

Aidha, amesisitiza kuwa kufanyika kwa Baraza hilo ni fursa inayoongeza uwazi na uwajibikaji mahala pa kazi na kuwawezesha watumishi wa Wizara hiyo kujadili hoja mbalimbali zinazowasilishwa na watumishi.

IMG-20230308-WA0027.jpg
 
Back
Top Bottom