Waziri Philip Mpango: Mambo Magumu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
MALALAMIKO ya wananchi kwamba, maisha yamekuwa magumu, sasa yamethibitishwa na serikali.

Dk. Philipo Mipango, Waziri wa Fedha na Mipango akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) katika mahafali ya 33 yaliyofanyika chuoni hapo mjini Dodoma, amethibitisha ugumu wa maisha wa sasa.

Amesema wanaoishi mijini, watu 100 kati ya watu 22 hawapati mahitaji yao ya msingi na katika Jiji la Dar es Salaam watu wanne kati ya 100 hawapati mahitaji yao ya msingi na mtu mmoja kati ya watu 100 Dar es Salaam hapati chakula cha kutosha.

Kutokana na hali hiyo, amewataka wahitimu wa chuo hicho kuhakikisha wanatumia elimu yao waliyoipata kwa ajili kuwapatia wananchi maendeleo hususani waishio vijijini.

Amesema, iwapo wahitimu hao watatumia elimu waliyoipata kwa manufaa ya wananchi, ni wazi wataondokana na msemo ambao unatumiwa na vijana kwa kukimbilia mjini kwa madai kwamba, watabanana huko huko (mjini).

Hata hivyo, amewataka wahitimu hao kufanya kazi kwa uamifu, kujiepusha na vitendo vya rushwa pamoja na mambo ambayo yanaweza kuliingiza Taifa katika machafuko.

Prof. Razack Lokina, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho amesema, chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa mabweni ya wanafunzi wa kike jambo ambalo linasababisha wanafunzi kupanga mitaani na kujikuta wakipoteza maadili.

Sambamba na hilo amesema kutokana na uhaba huo wa mabweni, chuo kinapanga nyumba za taasisi za serikali au watu binafsi jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa gharama kubwa za uendeshaji.

Changamoto nyingine ni kukosekana kwa jengo la utawala ambalo linakidhi viwango ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa uhaba wa wahadhiri.
 
Zaidi ya 68% ya Watanzania wanaishi chini ya Dola moja kwa siku na imekuwa hivyo kwa miaka mingi tu, sasa hizo takwimu unazolet zimetokea wapi? Maisha magumu ya Mtanzania hayajaanza jana!
 
38%.
Naunga mkono hoja yako. Lini ilikuwa afadhali?
 
Kama Maisha Yamekuwa Magumu Katika Awamu Hii Ya Tano Si Tuandamane Kuelekea Ikulu? Sasa kila siku Ni Kulalama Tu Bila Kuchukua Hatua?

Nadhani Tukikaribia Geti La Ikulu Ndo Tutaeleweka Vizuri.
Ukweli mtuphu. Haki haiji kilele mama. Ndio maana wanatuona mazuzu hawa watawala.
 
Ni kweli au wanaota? Kama ni ndoto tu wa wazi she kisongo ambapo kuna nguvu za kumzuia mtu kuota
 
Wana bahati mbaya kufanya kazi kwenye enzi za laana, rambirambi zikiwaacha ntaamini dunia haiko fair
 
Zaidi ya 68% ya Watanzania wanaishi chini ya Dola moja kwa siku na imekuwa hivyo kwa miaka mingi tu, sasa hizo takwimu unazolet zimetokea wapi? Maisha magumu ya Mtanzania hayajaanza jana!
Wasalimie lupango mnafiki
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom