PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,454
Waziri wa Mali asili na Utalii ameendelea kudhihirisha jinsi Rais JK asivyokuwa makini katika uteuzi wake. "The first method for estimating the intelligence of a ruler is to look at the men he has around him."
Niccolò Machiavelli, The Prince
Tumeona jaribio la haraka za Nyalandu kufungua mpaka wa Bologonja bila kufikiria athari za kiuchumi kwa taifa.
Pamoja na wabunge kadhaa kupinga mpango huu kwa sababu za kisayansi na kiuchumi, Nyalandu anasisitiza kwamba hili ni muhimu na tayari ameagiza independent study ifanyike. Athari hasi za kufungua mpaka huo ziko wazi na wala hakuhitajiki utafiti.
Huhitaji utafiti kuonyesha kuwa karatasi ni nyeupe! Tunaamini kuwa hicho anachodai kuwa ni independent study kinalenga kuhalalisha mchezo huu mchafu.
Wakati Nyalandu anafanya madudu huku akisimama kwenye vioo vya TV kutangazia umma kuwa ‘Tutawasaka, Tutawakamata Popote Walipo' anahakikisha kuwa pia anaongeza maneno haya Lakini siamini kuwa viatu vya kukabili ujangili vimemwenea Nyalandu, bila shaka vinapwaya, tena sana.
Vimepwaya kwa kuwa baada ya tambo hizi kwenye TV hukutana na wafanyabiashara hawa kwenye hoteli Arusha Hadi leo Nyalandu hajatuambia kuwa kwa kugoma kujibu hoja hii ya ‘kuuza' hifadhi kumemsaidia kuwakamata majangili wangapi.
Harakati zinazoendelea wizarani ni maandalizi ya kupeleka baadhi ya watu na wabunge Ethiopia, Chadi, Afrika Kati, Rwanda na Malawi eti kujifunza utendaji wa APN. Tujiulize, kama Serikali haina mpango wa kukabidhi mbuga yoyote kwa APN, Wizara inatumia mamilioni ya fedha (zaidi ya USD 120,000) kutuma watu kwenda huko kufanya nini? Je, huu ndio mkakati wa kuhakikisha kuwa falsafa yake ya "tutawasaka na kuwakamata" inatekelezeka?
Pengine ili kuwafurahisha wafanyabiashara kwenye tasnia ya uwindaji, alipuuza sababu za kisayansi na kutangaza kurefusha msimu wa uwindaji kutoka miezi sita hadi tisa.
Hili likafuatiwa na kituko kingine. Akatumia mamilioni ya walipa kodi kugharamia ziara ya Martin Fletcher (na mwenzake) kutoka Daily Mail on Sunday la Uingereza. Katika makala yake, Fletcher aliichafua Tanzania na kumdhalilisha Rais wetu.
Serikali ilikanusha vikali na kufikia hatua ya kulalamikia udhalilishaji huu kwenye ubalozi wa Uingereza.
Yaani Mwandishi wa habari wa Uk analetwa na Waziri kwa gharama za walipa kodi na mwandishi huyo anaitukana serikali bado waziri huyo amekalia ofisi ya umma.